Pre GE2025 Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Mohammed Kawaida: Uchunguzi ufanyike kufuatia vitendo vya utekaji na mauaji

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Huyu mpuuzi ameibuka baada ya watu wa CCM nao kuanza kupotea na watekaji kuanza kuuwawa.

Mzee Kibao inaenda mwezi wa 3 tangu atekwe na kuuwawa, Soka na wenzake mwezi wa 4 leo hawajulikani walipo, Edgar Mwakabela leo ni miezi 6 waliomteka hawajajulikana halafu tukio la Tegeta tu limetokea juzi watu jana wamekamatwa hapo kuna usawa?

Ni wakati sahihi raia kuanza kutumia haki yako kikatiba kujilinda baada ya polisi kushindwa kutekeleza majukumu yao [ulinzi wa raia na mali zao] na badala yake kuhamia kwenye utekaji, wizi wa kura kuibeba CCM na kuzuia maandamano ambayo ni haki kikatiba.

Nawapongeza wananchi kwa kuonyesha nguvu yao katika kujilinda pale Tegeta kwa ndevu, natarajia matukio mengi ya kufurahisha na ushindi kwa wananchi mpaka tabia hii ya kuteka watu itakapoisha.
 
Hajamuuliza yule uvccm wa Bukoba? Na yule DC wa Longido kuhusu mambo wanayofanya porini?
 
Uchunguzi wa nini ni kupoteza muda, tujifunze kuzoea vifo.
 
UVCCM walishalipa maelekezo Jeshi la Polisi kutowatafuta!
 

Attachments

  • YouCut_20241208_155127346.mp4
    1.6 MB
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…