Pre GE2025 Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Mohammed Kawaida: Uchunguzi ufanyike kufuatia vitendo vya utekaji na mauaji

Pre GE2025 Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Mohammed Kawaida: Uchunguzi ufanyike kufuatia vitendo vya utekaji na mauaji

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Huyu mpuuzi ameibuka baada ya watu wa CCM nao kuanza kupotea na watekaji kuanza kuuwawa.

Mzee Kibao inaenda mwezi wa 3 tangu atekwe na kuuwawa, Soka na wenzake mwezi wa 4 leo hawajulikani walipo, Edgar Mwakabela leo ni miezi 6 waliomteka hawajajulikana halafu tukio la Tegeta tu limetokea juzi watu jana wamekamatwa hapo kuna usawa?

Ni wakati sahihi raia kuanza kutumia haki yako kikatiba kujilinda baada ya polisi kushindwa kutekeleza majukumu yao [ulinzi wa raia na mali zao] na badala yake kuhamia kwenye utekaji, wizi wa kura kuibeba CCM na kuzuia maandamano ambayo ni haki kikatiba.

Nawapongeza wananchi kwa kuonyesha nguvu yao katika kujilinda pale Tegeta kwa ndevu, natarajia matukio mengi ya kufurahisha na ushindi kwa wananchi mpaka tabia hii ya kuteka watu itakapoisha.
 
Mwenyekiti Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mohammed Ali Kawaida (MCC) amesisitiza jeshi la polisi kuwa wafanye uchunguzi kufuatia vitendo vya mauaji na utekaji na pale wanapopata taarifa watoe kwa jamii ili wajue kinachoendelea.

Mwenyekiti ameyasema hayo tarehe 04 desemba 2024 akitoa salamu za rambirambi kwenye ibada fupi ya kumuaga aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM tawi la Machinjioni wilaya ya Chunya - Mbeya ambaye aliuawa usiku wa kuamkia tarehe 03 desemba 2024.
View attachment 3171964
Hajamuuliza yule uvccm wa Bukoba? Na yule DC wa Longido kuhusu mambo wanayofanya porini?
 
Mwenyekiti Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mohammed Ali Kawaida (MCC) amesisitiza jeshi la polisi kuwa wafanye uchunguzi kufuatia vitendo vya mauaji na utekaji na pale wanapopata taarifa watoe kwa jamii ili wajue kinachoendelea.

Mwenyekiti ameyasema hayo tarehe 04 desemba 2024 akitoa salamu za rambirambi kwenye ibada fupi ya kumuaga aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM tawi la Machinjioni wilaya ya Chunya - Mbeya ambaye aliuawa usiku wa kuamkia tarehe 03 desemba 2024.
View attachment 3171964
Uchunguzi wa nini ni kupoteza muda, tujifunze kuzoea vifo.
 
UVCCM walishalipa maelekezo Jeshi la Polisi kutowatafuta!
 
Attachments

  • YouCut_20241208_155127346.mp4
    1.6 MB
Back
Top Bottom