GE2025 Mwenyekiti wa UVCCM Taifa: Wanalipwa kuchochea vurugu, nchi yetu wameichoma moto

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Mohamed Ali Kawaida amevunja ukimya na kuzungumza kwa mara ya kwanza kuhusu matukio ya uvunjifu wa amani yaliyotokea tarehe 29 na 30 Oktoba 2025, akisema kwa masikitiko kuwa vurugu hizo zimefanywa kwa kiasi kikubwa na vijana kundi analowajibika kuliongoza na kulisemea ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Mwenyekiti huyo amesema uchaguzi mkuu wa mwaka huu ulioipa CCM ushindi mkubwa, umeacha alama ya huzuni kutokana na vitendo vya fujo na uharibifu vilivyotekelezwa na baadhi ya vijana. “Nimesimama mbele yenu leo si kwa furaha, bali kwa maumivu makubwa. Uchaguzi uliopita ulikuwa ushindi kwa chama chetu, lakini pia ulikuwa somo zito kwa taifa,” amesema kwa hisia.

Amesema kuwa sehemu kubwa ya vurugu hizo zilichochewa na watu walioko nje ya nchi, ambao kwa kutumia mitandao ya kijamii waliwashawishi vijana walio ndani ya Tanzania kufanya vurugu huku wao wakiwa salama na wakifadhiliwa na watu wasioitakia mema nchi. “Ni jambo la kuhuzunisha kuona vijana wenye nia njema wakitumiwa vibaya na watu wanaotaka kuivuruga Tanzania,” amesema Mwenyekiti huyo.

Ameeleza kuwa vitendo hivyo vimesababisha uharibifu mkubwa wa mali za umma na binafsi, vikiwemo vituo vya polisi, vituo vya mabasi, zahanati, maduka na miundombinu ya barabara. “Cha kusikitisha zaidi, baadhi ya waliojeruhiwa katika vurugu hizo walishindwa kupata matibabu kwa sababu walikuwa tayari wamechoma zahanati walizotegemea kwa huduma za kwanza,” amesema kwa uchungu.

Mwenyekiti huyo amekemea vikali vurugu hizo, akisema hazikuwa maandamano halali kwa mujibu wa sheria za Tanzania, bali ni vitendo vya uhalifu vilivyoleta hasara kubwa kiuchumi na kijamii. Ameongeza kuwa vurugu hizo ziliathiri biashara nyingi, kuathiri kipato cha wananchi, na hata kuzuia shughuli za bandari zinazohudumia nchi jirani.

“Vijana wenzangu, amani ndiyo msingi wa maendeleo. Tanzania imejengwa juu ya misingi ya umoja, amani na upendo. Tukicheza na amani, tunacheza na uchumi wetu, na ajira zetu,” amesema Mwenyekiti huyo.

Kwa hiyo hajui kama kuna watu maelfu wameuawa?
 
Qmlmmyk anajua kitaulo hichi qmmk vijana wameuwawa hasikitishwi asome alama za nyakati
 
Uyo km la mama ake kaona vitu tu ndo vimeharibiwa hakuna aliekufa hii ni level kubwa ya unafiki unaachaje kutamka watu wameuwawa hii ndo utu sio tutafika tu na bado

Tena hawakufa ila walijeruhiwa tu🙆‍♂️🙆‍♂️🙆‍♂️
 
Mnapozungumzia Amani msisahau ni matokeo ya Haki.

Hayo maandamano yanayofuata sheria labda yawe ya kumpongeza mtu ndiyo yataruhusiwa! Unategemea nini?

Wasioitakia mema nchi hii ni wale wasiotenda haki.
 
Uyo km la mama ake kaona vitu tu ndo vimeharibiwa hakuna aliekufa hii ni level kubwa ya unafiki unaachaje kutamka watu wameuwawa hii ndo utu sio tutafika tu na bado
Imagine katika maneno yoote aliyoyatoa kinywani mwake karibu elfu moja hakuna sehemu hata moja alipongelea uhai wa maelfu ya binadamu wasiokuwa na hatia uliopotea, yeye anaongelea mali na miundo mbinu tu kwamba ndio vinavyomuuma sana.. haya majitu kutoka visiwani nafsi zao zimejaa ushetani na sijui kwanin mpaka muda huu tumekubali watuongoze!
 
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Mohamed Ali Kawaida amevunja ukimya na kuzungumza kwa mara ya kwanza kuhusu matukio ya uvunjifu wa amani yaliyotokea tarehe 29 na 30 Oktoba 2025, akisema kwa masikitiko kuwa vurugu hizo zimefanywa kwa kiasi kikubwa na vijana kundi analowajibika kuliongoza na kulisemea ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Mwenyekiti huyo amesema uchaguzi mkuu wa mwaka huu ulioipa CCM ushindi mkubwa, umeacha alama ya huzuni kutokana na vitendo vya fujo na uharibifu vilivyotekelezwa na baadhi ya vijana. “Nimesimama mbele yenu leo si kwa furaha, bali kwa maumivu makubwa. Uchaguzi uliopita ulikuwa ushindi kwa chama chetu, lakini pia ulikuwa somo zito kwa taifa,” amesema kwa hisia.

Amesema kuwa sehemu kubwa ya vurugu hizo zilichochewa na watu walioko nje ya nchi, ambao kwa kutumia mitandao ya kijamii waliwashawishi vijana walio ndani ya Tanzania kufanya vurugu huku wao wakiwa salama na wakifadhiliwa na watu wasioitakia mema nchi. “Ni jambo la kuhuzunisha kuona vijana wenye nia njema wakitumiwa vibaya na watu wanaotaka kuivuruga Tanzania,” amesema Mwenyekiti huyo.

Ameeleza kuwa vitendo hivyo vimesababisha uharibifu mkubwa wa mali za umma na binafsi, vikiwemo vituo vya polisi, vituo vya mabasi, zahanati, maduka na miundombinu ya barabara. “Cha kusikitisha zaidi, baadhi ya waliojeruhiwa katika vurugu hizo walishindwa kupata matibabu kwa sababu walikuwa tayari wamechoma zahanati walizotegemea kwa huduma za kwanza,” amesema kwa uchungu.

Mwenyekiti huyo amekemea vikali vurugu hizo, akisema hazikuwa maandamano halali kwa mujibu wa sheria za Tanzania, bali ni vitendo vya uhalifu vilivyoleta hasara kubwa kiuchumi na kijamii. Ameongeza kuwa vurugu hizo ziliathiri biashara nyingi, kuathiri kipato cha wananchi, na hata kuzuia shughuli za bandari zinazohudumia nchi jirani.

“Vijana wenzangu, amani ndiyo msingi wa maendeleo. Tanzania imejengwa juu ya misingi ya umoja, amani na upendo. Tukicheza na amani, tunacheza na uchumi wetu, na ajira zetu,” amesema Mwenyekiti huyo.

Ajira na uchumi gani anaouzungumzia
 
Hivi katoto kazuri kama haka kana threat Gani?
20251107_210244.jpg
 
Back
Top Bottom