Mwenyekiti wa Walimu Wasio Na Ajira (NETO) Joseph Paulo anadaiwa kukamatwa na polisi mkoani Geita

Mwenyekiti wa Walimu Wasio Na Ajira (NETO) Joseph Paulo anadaiwa kukamatwa na polisi mkoani Geita

Mwenyekiti wetu wa NETO Joseph Paulo Kaheza amekamatwa na police mkoani Geita. Tumethibitisha hizi taarifa kutoka kwa mjomba wake ambaye alifika katika kituo hicho cha Central Geita Mjini na kutaka kumwekea dhamana kitu ambacho kilishindikana.

Soma Pia: Umoja wa Walimu Wasio Na Ajira (NETO) wakubali wito wa Simbachawene lakini wataka kuwepo na Ulinzi kwenye kikao

View attachment 3248480
Mkuu msiache kufuatilia hii issue na kutupa updates humu humu jf hii serikali ni ya Kise... Sana.
 
Huyu jamaa angekuwa selected au kaajiriwa hata wazo la kuanzisha NETO lisingekuwepo

Vijana kazeni ajira miaka hii za ushindani sana si lelemama

Hakuna serikali itakayoweza kuajiri walimu wote 200k mlio mtaani

Ni mwendo wa mchujo. Mbona kada zingine hatuwaoni kulalamika na kuanzisha vyema vya kihuni huni
 
Kwahiyo wanataka kumuua??? Huyo mwl itakuwa ajabu sana mwlimu kuuwawa na serikali ya JMT chini ya uongozi wa samia kwa kukulalamika kukosa ajira na mwenendo mbaya wa ajira zinatolewa na serikali kwa usimamizi wa taasisi iliyojaa upendeleo undugu na rushwa, ucheleweshwaji wa mchakato bila sababu wala maelezo ya hali juu secretariat

Maza kwa sasa anachotaka kusikia ni sifa tu. Inaelekea sifa zinamlewesha.
 
Labda kuzua taharuki na kusambaza taarifa za uongo mtandaoni. Unajua ukitamka jambo la kitakwimu inabidi uwe makini sana.

Hawa walitakiwa hizo hotuba na maelezo yao yote wapitishe kwenye jopo la mawakili, ili kuangalia madhara na matokeo yake. Hivyo ndio mambo yanapaswa kwenda na sio hivi kwenda kiholela, lazima uzingue tu na unajua Jamhuri haina time na raia mwema (mfuata sheria) tatizo lipo ukijichanganya pahali tu wana wewe.

Huyu jamaa nilimsikiliza kidogo ila nikajua hapa na hapa kazingua na wameruka naye tayari.

Vijana tunataki tujue kuwa tufanye yote ila kamwe tusijaribu kusababisha kitisho kwenye usalama wa hili taifa, utapotea na hakuna atakayejutia. Sasa kutaka kuinua hasira za graduates ni big move inayoitaji akili sana, sio jambo la mchezo au masihara.
Umejitahidi kuandika Big Up japo nawe ni wa mlengo ule
 
Kunyimwa dhamans kuna sababu nyingi ila za moja kwa moja huwa ni ama hajakamatwa kwa kosa lolote, hapo hawezi kupewa dhamana sababu hana kosa alilokamatwa nalo.

Sababu nyingine inaweza ikawa kwa ajili ya kuulinda usalama wake yeye mwenyewe. Baada ya intelijensia ya polisi kuona ipo hiyo sababu.

Sasa usiniulize mtu anakamatwaje bila kosa, hilo linawezekana na limeruhusiwa na sheria zetu wenyewe. Kukamatwa sio kosa kosa ni lile lililofanyika tu.

Hiyo sababu ya pili ni ya Ukandamizaji tu. Nsons kwa awamu hii ndiyo imeanza kuwa sababu ya kuwashikila watu kinyume cha sheria.

Watu wanaotoka hadharani kuomba ulinzi kuwa maisha yao yako hatarini huwa hawapewi huo ulinzi.
 
Nilisema mie, kuitwa ofisi ya waziri ni alarm, haya Leo Kakamatwaa M/kiti wa chama. Lol
 
Nchini Zaire (DRC)! ilikuwa ni Kosa kubwa sana kwa kufanya Kitendo cha Kumkosoa mtawala wa nchi hiyo Dikteta Mobutu Sese Seko au kuukosoa Utawala wake. Hali ipo hivyo pia nchini Urusi kwa Putin na nchini China.

Kuwakosoa Madikteta ni sawa sawa na kujikatia tiketi ya kifo.
At least Madikteta wa urusi na china wameleta maendeleo makubwa mnoo kwenye mataifa yao, sio hawa wa TANZAGIZA
 
Aise, achana na taasisi inayoitwa serikali. Sio ndogo hivyo unavyowaza. Sawa hautakiwi kuiogopa serikali ila amini nakuambia unatakiwa kuiheshimu kwa.adabu zote ulizofundishwa kwenu.

Hapa unaweza ukafikiri hawakujui ila na jina lako hili wakikuamulia ni haraka sana wanakujua, na kukuchukua itakuwa ni uamuzi wao tu wala sio wako 😂😂

Unless uwe ni keyboard worrior au ubishe tu kutokana na uelewa mdogo.
Itakes mtu ambae yupo serikalini or ambae alishapita huko tena kwenye vyombo husika kujua weakness ya hao watu na namna wana operate.
Wako watu walikuwa huko they know how to avoid them because walikuwa huko so mbinu wanazifaham

Ila kwa raia wa kawaida is another story
 
Nchini Zaire (DRC)! ilikuwa ni Kosa kubwa sana kwa kufanya Kitendo cha Kumkosoa mtawala wa nchi hiyo Dikteta Mobutu Sese Seko au kuukosoa Utawala wake. Hali ipo hivyo pia nchini Urusi kwa Putin na nchini China.

Kuwakosoa Madikteta ni sawa sawa na kujikatia tiketi ya kifo.
Unataka kusema Tz kuna udictator?
 
Wanapokosea namna ya kushinikiza madai yao lazima tuseme, hilo ni swala la lazima kabisa.
Unaweza kuwa na haki lkn usijue namna yakuzidai, au unajua kuzidai na bado usizipate, au ukazipata lkn usijue namna yakuzitumia. Nmeisikiliza clip ile vizuri. Yule kijana ameongea pointi za msingi sana Sana. Tena ilitakiwa apewe ajira mapema maana Ni nguvu kazi nzuri inayorandaranda mtaani kulingana na uwezo wake.
 
Ratio ya graduates na ajira zinazotolewa ni mbingu na nchi...hizo nafasi zote zinajazwa na vyuo vya UDSM, UDOM na SAUT tu, sasa wengine waende wapi, shule za private kutokana na usimamizi mbovu wa serikali wanalipa mpaka laki na nusu, haya ni Matatizo, na hizi Ajira kiduchu kiduchu ndio zinazidi kutia watu Hasira.
Kwan unasoma ili upate ufahamu au ili uajiriwe?
 
Kwan unasoma ili upate ufahamu au ili uajiriwe?
Siku utaelewa kwann watoto wa maskini wanasoma na wali major kwenye education kwa sasa....Endelea kugombea remote kwa shemeji huku usiku ukisikilizia miguno ya dada ako anavyopigwa miti.
 
Kunyimwa dhamans kuna sababu nyingi ila za moja kwa moja huwa ni ama hajakamatwa kwa kosa lolote, hapo hawezi kupewa dhamana sababu hana kosa alilokamatwa nalo.

Sababu nyingine inaweza ikawa kwa ajili ya kuulinda usalama wake yeye mwenyewe. Baada ya intelijensia ya polisi kuona ipo hiyo sababu.

Sasa usiniulize mtu anakamatwaje bila kosa, hilo linawezekana na limeruhusiwa na sheria zetu wenyewe. Kukamatwa sio kosa kosa ni lile lililofanyika tu.
Kwa scenario ya jamaa ambaye amekamatwa siku chache baada ya kuilalamikia serikali

Hivi unadhani kama hoja ya kukamatwa kwake na kunyimwa dhamana ni pamoja na kuwepo kwa viashiria vya yeye kuwa hatarini, unafikiri odds zinaonesha ni nani wanaopewa nafasi ya kuhatarisha maisha ya jamaa?

Jamaa hakuwatukana majambazi, hakuwa expose wauza madawa ya kulevya kiasi cha polisi kumuweka kizuizini kulinda usalama wake.

Sasa kama kuikemea serikali kuhusu tatizo la ajira jambo hilo liende kuhatarisha maisha yake basi sioni usalama wake wowote hata akiwa hapo polisi kwasababu nao pia ni sehemu ya serikali na inaweza kupokea maagizo na ikafanya kama ilivyo tumwa.
 
Back
Top Bottom