Uchaguzi 2020 Mwenyekiti wangu CCM Taifa, Rais Dkt. Magufuli tafadhali achana na Kauli kama hii katika 'Kampeni' zako kwani zinakuharibia na zinachanganya

Uchaguzi 2020 Mwenyekiti wangu CCM Taifa, Rais Dkt. Magufuli tafadhali achana na Kauli kama hii katika 'Kampeni' zako kwani zinakuharibia na zinachanganya

Mkiwachagua hao wengine hawataweza kuendeleza miradi niliyoianzisha-Magufuli.

Apige picha akifa leo hakuna atakae we za kuingoza nchi? Hizi ni kauli za hovyo kutolewa na kiongozi.
Je, ni kauli ya hovyo kuliko ya huyo anayemdharilisha mama mzazi wa Rais, ati tu kampeleka nyumbani kwa ndege, akijua mama wa watu ni mgonjwa hadi leo yu kitandani mahtuti? Shame on you
 
Keshazoea kwao Burundi ni kutumia nguvu kuliko akili
 
Anathibitisha bila kujua kuwa yeye ndio anayepanga matumizi ya fedha za nchi, sio wabunge wala bunge!!

Anapaswa kuwa Rais wa waTanzania. Bado hajui asili ya binadamu ya kuwaza na kuamua tofauti! Atakuja kufahamu hilo mambo mengi yamekwishaharibika.

Lakini anatambua mambo mengi. Hayo anawaambia wananchi wa vijijini ambako kuna “wanyonge” wengi wanaochukuliwa poa. Hawezi kusema hayo mijini!!
 
Nadhani Hapa watu tumeshindwa kutofautisha JPM ni Nani na Kwa wakati Gani
Kwa sasa Magufuri ni Mgombea uraisi kupitia CCM, Ananadi Sera Kwa njia kichama lakin muda huo huo anaitumia kofia ya URais Ambayo Bado anayo Hadi sasa kuombea Kura!!
Kauli kama hiyo uliyo I note hapo!! Kama Una mihemuko yako ya kisiasa utakurupuka kuwa unafokewa
Lakini sivyo JPM kapeleka miradi mbalimbali ya maenndeleo Majimbo mengi Tu ya Upinzani!!
Unaweza kuniambia maendeleo aliyoyaleta kanda ya kaskazini miaka 5? Njtajie mawili tu
 
Mwisho wa siku tutawachagua hao hao halafu tuone anakufa nani barabara haijajengwa. Hakuna dawa na wataalamu hospitali za umma alizojenga "kibao" mbona hatufi sembuse barabara, kwani hatujawa nazo tangu lini ndio iwe miaka mitano tu hii ijayo!? Suala lingekuwa ni kuchagua viongozi toka CCM pekee ndio tunaendelea mbona tungeshakuwa Urusi!

Huyu mzee asijifanye ana hati miliki ya nchi hii na kwamba nj rais wa milele walikuwepo wenzake na yeye atapita. Fedha za umma sio mirathi toka kwao wala sio MALI YA CCM eti kwamba iwe ni privilege kupeleka huduma kiasi fulani kana kwamba eneo hilo hakutoki kodi. Ushamba tu na ulimbukeni wa kisiasa.
 
Wapinzani hawataki maendeleo ya vitu sasa asingekuwepo Kapuya mbunge wa CCM mdai maendeleo ya barabara hiyo barabara isingejengwa.Kasome sera ya Chadema hawana mpango na maendeleo ya vitu ina maana ukichagua mbunge wa Chadema sabau maendeleo ya vitu sababu hatayatafuta sera yake hairuhusu
Wala Dr Magufuli hajakosea
Walipo wabunge wa Chadema apeleke maendeleo ya vitu ya nini? Kuchagua mbunge wa Chadema ni kuchagua sera kuwa watu wa eneo hilo hawataki maendeleo ya vitu sasa kama hawataki unawalazimisha kuwapelekea?
Yaani wewe hata ukiambiwa haya ni mavi utabisha Hadi uonje ndo uamini huna akili
 
Magufuli anachofanya sio sahihi alitakiwa ajiulize kwanini wabunge wa chama chake hawachaguliwi na sio kulazimisha wachaguliwe. Kila mtu ana uhuru na sababu kwanini amefanya maamuzi ya kuchagua kiongozi fulani.

Kama serikali ilinifanyia dhuruma kwanini niichague au kama imeleta kiongozi mbovu kwanini nichague lakini kitendo chake cha kukataa kuleta maendeleo kisa wamechaguliwa upinzani mbona kodi zao anachukua
Well said. 🙏 🙏 🙏
 
Back
Top Bottom