Uchaguzi 2020 Mwenyekiti wangu Dkt. Magufuli kuna kitu ambacho haukukifanya kitakuangusha tu kwenye Uchaguzi huu

Tunataka free of speech sio kuogopa kutekwa
 
SGR, Stiglers HEP, Barabara nzuri, hospitali na vifaa tiba, eropleni, mifumo ya maji, mashule na vyuo, n.k.); Au, tukitumie kuongeza mishahara ya watumishi, na kadhalika?
Tatizo la watu wengi ni kuongozwa na mukhtadha wa fikra binafsi kwenye masula yanayohitaji sera za umma.

Tanzania ni 'going concern', maamuzi yote ya maendeleo yanatakiwa kufuata kanuni ya balancing act.

Maendeleo ya miundo mbinu siyo jukumu la kukamilisha na awamu hii pekee. Aidha, maendeleo ya miundombinu hayapaswi ku-sacrifice maisha ya wananchi.

Kuweka maisha ya wananchi rehani kwa ajili ya kujenga miundombinu pekee ni poor planning.

Kulikuwa na haja ya kuwa na economic and social linkages kati ya miradi ya kimkakati na maisha ya watu ya kila siku.

Viongozi wapya watakaochaguliwa uchaguzi Mkuu wa 2020 watamalizia hiyo miradi ya maendeleo inayojengwa kwa sasa. Si lazima Magufuli achaguliwe (aendelee kutesa watu) tena eti, ili amalizie ujenzi wa miradi yake. Hii si miradi ya Magufuli bali ni miradi ya Tanzania na wananchi wake.

Kwa kuwa hata yeye alipoingia madarakani aliikuta miradi hiyo imekwisha kuanzishwa ila Serikali yake ilitoa kipaumbele kuitekeleza, watakao chaguliwa wataimalizia.

Magufuli alitakiwa kuwasikiliza watu. Hakufanya hivyo, bali alisikiliza hisia zake. Atusaidie kuondokana na mythical politics za CCM.

Bye bye Magufuli
 
Mbona hakupunguza mishahara ya mawaziri na wateule wake ?? Mbona kajenga kwao kiwanja cha. Ndege na kuanzisha mbuga?? Mbona kawapa ulaji ndugu zake ?? Acha unafiki ndugu yangu tulioteseka ni sisi wala sio wewe.
 
Sijui atajiteteaje kwa watumishi wa umma, wafanya biashara.
 

Hata asipotoa ajira hatuwezi kuendelea na hiyo dhiki tumechoka sana hata likigombea jiwe tutalichagua kuliko kuendelea na hii awamu enough is enough
 
Hatuli uzalendo ujue.
 

Umesema kweli kabisa itakuwa vema aondoke tu mwenyewe kama ni muelewa badala kuanza kuhangaika sijui kuzuia vyombo vya habari sijui kuiba kura mwaka huu hakuna hiyo nafasi
 
hapo mimi ndio nashangazwa na watz,SGR,STIGLERS n.k zitatuaje moja kwa moja changamoto za mkulima wa nanyumbu?, au mfanyakazi wa tz?, wakati wa gesi ya mtwara habari ilikuwa hiyohiyo!!!!, kwani mabarabara na miradi mikubwa imeanza mwaka awamu hii tu? tangu ukoloni barabara zinajengwa. wakati Nyerere anakabidhiwa nchi na wakoloni basi tungefunga mikanda mpaka viuno vikakatika lakini mikanda ilifungwa wakati wa vita ya kagera. kwenye biashara kumeathirika sana si kwa sababu yamishemishe kufa ni kwa sababu ya kodi
 
Mkuu ni sehemu gani ambayo hata Milo miwili kwa siku ni shida!?, Hapa tunahitaji references mkuu tusije rishana matango pori, maana najua mwaka huu almost nchi mzima wamelima Sana Sana kwahiyo availability ya chakula ni kubwa Sana.

Reference please.
 
[/QUOTE]
Bring facts and figures kuthibitisha magufuli ameharibu uchumi, usikariri maneno ya wengine.
Facts na figures za Lumumba ndiyo zimetufikisha hapa.

Na kwann tusikariri maneno ya wengine kama ndiyo wengi?
 

Simply wewe ni ki/laza 100%. Sera ya nchi inachangia kwa kiwango kikubwa kufaulu au kufeli kujenga utajiri kwa mtu mmoja mmoja. Watanzania si kwamba hawajitumi.. la hasha. Shida ni mfumo mbovu wa utawala, mfumo unakwamisha watu kufanya kazi na kupata mafao ya kazi zao kwa kiwango cha juu.. uliza mtu mwenye lori anasafirisha mizigo mikoani au nje ya nchi anapata faida au hasara wakt wa Jiwe.. Jiwe kafanya biashara ya hospitality kufa.. watu kibao wamepoteza ajira..

Unless hujui jukumu la serikali katika kuweka mazingira ya watu kupambana na maisha basi kaa kimyaa..

#NiYeye
#TunduLissu
 
Naomba na Kufunga kwa Mungu, ili amruhusu Yesu arudi tu. Inatosha. Naipenda nchi yangu, lakini mimi na watu mtaani tupo kwenye dhiki kubwa sana. Mungu amuamshe kiongozi wetu akumbuke wananchi wake, maana wote wema na wabaya wapo kwenye ugumu.
 
usidhan kila mmoja anayo iyo pesa unayoizungumzia
 

Umeenda shule angalau? Je umetembea nchi zingine angalau? Unasema huitegemei serikali inamaana hufahamu hata wajibu wa serikali yako kwa ustawi wa mtu mmoja mmoja na nchi kwa ujumla! Inamaana wewe hufahamu sera nzuri za serikali kuhusu biashara ndio zitasababisha wananchi wafuge hayo makuku unayoyasemea na kupata masoko ya uhakika ya kuyauza?

Unafahamu ni kiasi gani sera mbovu za biashara nchi hii ndio zinakwamisha Tanzania kutokuwa na wafanyabiashara wengi na badala yake kuna utitiri mwingi wa wachuuzi ambao hata kuchangia kwao kodi serikalini ni kwa kiasi kidogo sana?

Unazungumzia vijana wanaomaliza shule wafuge kuku, hebu waelekeze ni wapi watoto wa maskini wanaograduate maelfu kwa maelfu ni wapi wanaweza kwenda kupewa mitaji hata angalau kama mikopo tu ikiwa hawana cha kuweka dhamana, hebu eleza hapa tukusikie.

Unafahamu kupungua kwa pesa mtaani kunawaathiri vipi wafanyabiashara na kupelekea kufunga biashara zao sio kwa sababu ya hiyo propaganda ya “wapiga dili” Mliyozoea kuihubiri.

WaTz tuache ubinafsi kushindwa kuwasemea wengine kwasababu ya kujiona tuna unafuu wa maisha, ukiona watu humu wanahubiri kuhusu mishahara ya watumishi wa umma usidhani wote ni watumishi wa umma, ila ni uelewa kuwa nyongeza ya mshahara ni takwa la kisheria hivyo ni wajibu wa serikali kulifanya bila excuses.
 
2020 watanzania tutamchagua JPM kwa kura za kutosha.
Mazuri ya JPM ni mengi sana,changamoto huwa zipo tu.hata U.S kuna raia wanalalamikia changamoto za taifa lao.
ilhali tunaambiwa U.S ni kinara wa kila jambo la kimaendeleo.
Utamchagua wewe na familia yako mwenyewe wengine wamechoka kuishi kwa shida
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…