MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,252
- 8,003
Kama ambavyo siku zote nimekua nikisema kua mimi ni mkweli daima na fitina kwangu mwiko. Ni MwanaCCM hai niliyekitumikia muda mrefu na bado naendelea. Rais wangu ulikosea mambo machache sana pamoja na mengine mengi makubwa uliyofanya.
MAISHA MAGUMU KWA WATANZANIA
Mwenyekiti wangu, maisha ni magumu sana kwa watanzania wote hata mtu kupata milo miwili kwa siku ni shida. Kama wasaidizi hawasemi ukweli mkuu huko mitaani watu taabani kuliko awamu iliyopita. Watu walioko vijijini hawataki kujua Dar es salaam kuna marababara za juu au kuna Airport, hawajui kama kama kuna makubwa yamefanyika. Wao wanataka maisha mazuri.
Kiukweli akitokea mgombea atakayewaambia vizuri walalahoi hawa kura zote atapewa.
BIASHARA KUWA NGUMU
Kwa sasa maisha ya wafanyabishara yamekua magumu kabisa kila mahali kuliko awamu iliyopita, lipo tatizo kubwa ambalo kama tusiposema ukweli CCM hakuna mfanyabiashara atakayetupatia kura.
MAISHA MAGUMU KWA WAFANYAKAZI WA UMMA
Ni muda sasa wafanyakazi wa umma wanalia na maslahi duni, wengi hawana amani.
Hapa kura hatupati kabisa katika kundi hili tupende tusipende. Akitokea mgombea atakayeongea vizuri na kundi hili anaweza kuvuna kura nyingi sana na atapewa ushirikiano mkubwa .Wao wanaangalia mtu atakayewajali vizuri.
Mimi najaribu kusema msije mkasema hatukurlshauri.