Uchaguzi 2020 Mwenyekiti wangu Dkt. Magufuli kuna kitu ambacho haukukifanya kitakuangusha tu kwenye Uchaguzi huu

Uchaguzi 2020 Mwenyekiti wangu Dkt. Magufuli kuna kitu ambacho haukukifanya kitakuangusha tu kwenye Uchaguzi huu

Naomba na Kufunga kwa Mungu, ili amruhusu Yesu arudi tu. Inatosha. Naipenda nchi yangu, lakini mimi na watu mtaani tupo kwenye dhiki kubwa sana. Mungu amuamshe kiongozi wetu akumbuke wananchi wake, maana wote wema na wabaya wapo kwenye ugumu.
october ndo njia pekee iliyobaki ya kukomesha njaa
 
Bora hata angekuwa anaeleza haya kwa kauli ya ustalabu tungemwelewa.bali yeye anasema pesa IPO...tunanunua ndege KESHI...TANZANIA NI TAJIRI.hivi hata kama ni wewe unamdai mtu halafu hakulipi huku anajigamba kuwa anazo pesa utamuelewaje? Huyu magufuli hatufai kabisa amejaa misifa tu kwa kuwa yeye hana shida kama sisi tunaoitwa wanyonge
zipo tele za kununua wapinzani,kumshughulikia mbowe,kujenga kwao,kutoa rushwa makanisani,za kununulia jogoo na mapapai,na sio za kulipa wakulipa,kulipa fidia waliobomolewa nyumba zao,kuongeza mishahara,kulipa madeni ya ndani hizo hazipo kabisa.
 
Siongelei ndoto. Nasema Wana Kagera hawajasahau!
Wataendelea kukumbuka tu lakini kukumbuka kwao hakutasababisha dunia isimame hata kwa sekunde moja na maisha yataendelea kama kawaida
 
Ndugu fursa huwezi kuipata kwa kushinda kwenye FB, JF nk. Go out there and interact with those who have been successful, seek their advice, trust me you can gain more that can help to change your life
ukiuwa sekta binafsi hio succes chance utaipata wapi,umejaribu hata kulima mchicha uone hali au we kula kulala
 
Ambao wako taabani huko mitaani ni wale waliozeoa mishemishe na kuishi kisanii, sisi ambao tunajitambua na kuamini jasho lako ndio mkombozi namba moja tunaona maisha ni kawaida tu.

Changamoto haizwezi kukosekana katika maisha. Kama wewe ni mmoja wa wale walionufaika na ubabaishaji uliokiwepo awamu iliyopita, lazima awamu hii uone maisha magumu.

Changamsha akili, si Magufuli, Lisu, Membe n.k atakaebadilisha maisha yako.
Hili halisemi ila Mjinga.
Hali ipo wazi sitaki kuamini watu zaidi ya 2m waliotumbukia katika umasikini walikuwa wapigaji.
Tafakali Mkuu acha kutumia Tumbo kufikiri.
Hata kama kweli CCM ndo wamekuwa sababu ya kutononoka kwako
 
Magufuli hajawahi kudhamini utu na maisha ya mtu mwingine unless otherwise kuwe na political gains
Furaha yake ni kuona wengi wakilia,thus mwaka watano huu watz wanasota ndani wakisubiria ushahidi kukamilika hii ni again humanity then anaenda church kutoa rushwa akidhani kumnunua kiongozi wa dini ni kumnunua Mungu.
 
Endelea kuleta maneno ya mtaani na nadharia tu ukijifanya Eti unampamba au kumjenga huyo Magufuli kumbe unazidi kumuharibia.

Na marafiki zangu waliopoteza kazi Quality Group baada ya kampuni kufungwa kutokana na Mwenye kampuni kufirisiwa na serikali na kubambikiwa makesi na Serikali ya Magufuli nao unawaambiaje????

Na rafiki yangu ambae Ghala lake limeuzwa na bank baada ya kushindwa kurudisha mkopo baada ya serikali kuwapiga marufuku kununua korosho na kuchukua korosho kupitia jeshi nae unamwambiaje??? Tena kwenye kampuni yake alikuwa na watumishi 12 nao unawaambiaje????

Magufuli is a failure ndugu. Habebeki huyo mtu wenu. Kaharibu uchumi wa nchi!!
tukirudia kosa again tumekwisha atavurunda zaidi awamu ya pili,mkapa alituuzia foolish gold rangi halisi kila mtu anajua
 
Ambao wako taabani huko mitaani ni wale waliozeoa mishemishe na kuishi kisanii, sisi ambao tunajitambua na kuamini jasho lako ndio mkombozi namba moja tunaona maisha ni kawaida tu.

Changamoto haizwezi kukosekana katika maisha. Kama wewe ni mmoja wa wale walionufaika na ubabaishaji uliokiwepo awamu iliyopita, lazima awamu hii uone maisha magumu.

Changamsha akili, si Magufuli, Lisu, Membe n.k atakaebadilisha maisha yako.
sera mbovu uleta umasikini nchini.Hawa graduate wasio na ajira walipiga dili gani,wakulima wa korosho na mbaazi nao walipiga dili gani,waliokosa ajira baada ya matajiri kushughulikiwa walipiga dili gani.
ukiwa kula kulala huwezi yaona haya
 
Hili halisemi ila Mjinga.
Hali ipo wazi sitaki kuamini watu zaidi ya 2m waliotumbukia katika umasik9ini walikuwa wapigaji.
Tafakali Mkuu acha kutumia Tumbo kufikiri.
Hata kama kweli CCM ndo wamekuwa sababu ya kutononoka kwako
Well, kwanza tuelewane. Mjinga ni yule aliyewazaa wajinga waliokuzaa wewe na wakakulea katika mazingira ya ujinga. Ndio mana neno ujinga ndio pekee lililojaa kwenye akili yako. Now, nieleze ni nchi gani unayoijua wewe ambayo hakuna watu masikini?
 
Wapo walio graduate mwaka huo huo wakaanzisha ufugaji wa kuku kwa msingi wa TZS 2,000,000 sasa hivi they are talking of 3 - 4mil a month. Msubiri Lisu, wengi wenu mnaamini nyumbani kwake amefunga bomba la ajira ambalo anasubiri achaguliwe ili alifunguwe ambao hamna ajira mpate ajira.
hizo ni hesabu za motivation speaker,sera nzuri kuinua kilimo,kujenga mahusiano mazuri ya kimataifa uchochea wawekezaji ambao utoa ajira,mipaka ikiwa wazi wakulima uuza nje na kupata pesa kilimo kikiinuka viwanda vinaongezeka na idadi ya machinga na bodaboda inapungua mijini wote watarudi kuzalisha vijijini sababu kilimo kinalipa.
indictor ya shida ya ajira ni kubwa unachek idadi ya machinga na bodaboda mijini
 
ukiuwa sekta binafsi hio succes chance utaipata wapi,umejaribu hata kulima mchicha uone hali au we kula kulala
Tuanzie hapa, nieleze sekta binafsi uliyokuwa unafanya kazi ambayo imefilisika na sababu za kufilisika kwake. Nataka uweke hapo uzoefu wako binafsi sio ulete stori za kufikirika
 
Well, kwanza tuelewane. Mjinga ni yule aliyewazaa wajinga waliokuzaa wewe na wakakulea katika mazingira ya ujinga. Ndio mana neno ujinga ndio pekee lililojaa kwenye akili yako. Now, nieleze ni nchi gani unayoijua wewe ambayo hakuna watu masikini?
kuna masikini wa kusababishwa na mfumo mbovu na masikini sababu ya factor zingine mfano ulemvu,nk.Wakomunisti wote akiwemo huyo mungu wako wao wanaimba uzalendo mbele ya camera lakini kivitendo ni kinyume chake,wao wanaamini katika falsfa ya kuwafanya watu wawe masikini ili wawatawale hizi ni nadharia za kijamaa na kikomunist thus kawasomesha watu namba ili aweze kuwatawala wamuabudu thus bila kusifu hakuna teuzi.
 
Afadhali kumjaribisha Lissu ambaye ni mwanasheria kuliko kurudia kosa kwa kumchagua Magufuli!!! Sitasahau kauli na attitude yake tulipokumbwa na tetemeko kule Kagera.
Niliumia sana, zile sio kauli ambazo zilipaswa zitolewe na kiongozi mkuu wa nchi tena baada ya kukusanywa kwa michango ya ndani na baadhi ya nchi rafiki nao kuchangia.
A lot of people were disappointed
 
hizo ni hesabu za motivation speaker,sera nzuri kuinua kilimo,kujenga mahusiano mazuri ya kimataifa uchochea wawekezaji ambao utoa ajira,mipaka ikiwa wazi wakulima uuza nje na kupata pesa kilimo kikiinuka viwanda vinaongezeka na idadi ya machinga na bodaboda inapungua mijini wote watarudi kuzalisha vijijini sababu kilimo kinalipa.
indictor ya shida ya ajira ni kubwa unachek idadi ya machinga na bodaboda mijini
Aisee ukiendelea kuleta theories ulizosoma shuleni huwezi kufanikiwa katika maisha. Theories hizo zimetungwa na watu kama wewe, zitakusaidia tu kukupanua mawazo if you are smart kichwani. Hakuna taifa litakalokuletea maendeleo, nenda kasome economic diplomacy utaelewa ninachokuambia. Kasome how Europe underdeveloped Africa by Walter Rodney utaelewa ninachokuambia
 
Tuanzie hapa, nieleze sekta binafsi uliyokuwa unafanya kazi ambayo imefilisika na sababu za kufilisika kwake. Nataka uweke hapo uzoefu wako binafsi sio ulete stori za kufikirika
sekta za mabenki,chain nzima ya zao la korosho,bureau de change,nenda quality group uone magofu yamebakia je ni ajira ngapi pale zimepotea sababu tu ya bifu za kitoto toto,nenda kwenye sekta ya mbao na viazi njombe,dagaa na samaki mwanza,kwa uchache.
 
Jpm anasema hapangiwi, safari hii akapumzike tu, wacha aingie kijana wa singida, mzalendo lissu
 
kuna masikini wa kusababishwa na mfumo mbovu na masikini sababu ya factor zingine mfano ulemvu,nk.Wakomunisti wote akiwemo huyo mungu wako wao wanaimba uzalendo mbele ya camera lakini kivitendo ni kinyume chake,wao wanaamini katika falsfa ya kuwafanya watu wawe masikini ili wawatawale hizi ni nadharia za kijamaa na kikomunist thus kawasomesha watu namba ili aweze kuwatawala wamuabudu thus bila kusifu hakuna teuzi.
You are crossing the line! Kama umelelewa katika mazingira ya kumfanya binadamu kuwa mungu usifikiri kila mmoja amelelewa hivyo. Huyo ni mungu wako na familia yako
 
Wapo walio graduate mwaka huo huo wakaanzisha ufugaji wa kuku kwa msingi wa TZS 2,000,000 sasa hivi they are talking of 3 - 4mil a month. Msubiri Lisu, wengi wenu mnaamini nyumbani kwake amefunga bomba la ajira ambalo anasubiri achaguliwe ili alifunguwe ambao hamna ajira mpate ajira.
Awamu hii hata walimu wa shule za msingi hawana uhakika wa ajira huku baadhi ya shule zikiwa na walimu 3. Kumbuka ratiba ya masomo shule za msingi haiwezi kupangika kwa walimu chini ya 8 kwasababu ya idadi ya masomo na vipindi. Awamu zilizopita mwalimu akitoka chuoni anajua aenda fundisha shule iliyo mkoa gani...Awamu hii kipaumbele sio ajira. Hata wale wa vyeti feki nafasi zao hazijajazwa.
 
Watu wamethubutu, pita Quality Center sasa hivi frem zipo tupu maduka yamefungwa.
Kariakoo fremu na nyumba mpaka zinaandikwa nambari za simu za wenye majengo zinatafuta wapangaji! Wakati wa JK ilikuwa kuipata fremu Kariakoo umtafute dalali akutongozee mpangaji akubali kuchukuwa kilemba!
 
Back
Top Bottom