Uchaguzi 2020 Mwenyekiti wangu Dkt. Magufuli kuna kitu ambacho haukukifanya kitakuangusha tu kwenye Uchaguzi huu

Uchaguzi 2020 Mwenyekiti wangu Dkt. Magufuli kuna kitu ambacho haukukifanya kitakuangusha tu kwenye Uchaguzi huu

Aisee ukiendelea kuleta theories ulizosoma shuleni huwezi kufanikiwa katika maisha. Theories hizo zimetungwa na watu kama wewe, zitakusaidia tu kukupanua mawazo if you are smart kichwani. Hakuna taifa litakalokuletea maendeleo, nenda kasome economic diplomacy utaelewa ninachokuambia. Kasome how Europe underdeveloped Africa by Walter Rodney utaelewa ninachokuambia
WALTER RODNEY ameandika rubbish dhana zake zinapingana na hali halisi,za kuwalaumu wazungu juu ya kushindwa kwetu na alitumika na watawala wa kiafrica baada ya kushindwa kuwaletea waafrika maendeleo tarajiwa baada ya kuwadanganya waafrica wawape sapoti wawaondoe wakoloni watakula mema ya nchi, matokeo yakawa kinyume chake,wapigania uhuru ndo wakawa wakoloni weusi kwa kuwatendea waafrika mabaya na ukatili wa hali ya juu kuliko hata mkoloni mweupe alivomtendea mwafrika kwa kuwauwa waafrika wenzao,kufisadi kodi zao,kuendekeza ukabila,kuiba na kupora mali za waafrkia na kujigeuza miungu watu huku watawala wakiishi peponi hali wakiuwa chumi nzuri za nchi zao.
 
Awamu hii hata walimu wa shule za msingi hawana uhakika wa ajira huku baadhi ya shule zikiwa na walimu 3. Kumbuka ratiba ya masomo shule za msingi haiwezi kupangika kwa walimu chini ya 8 kwasababu ya idadi ya masomo na vipindi. Awamu zilizopita mwalimu akitoka chuoni anajua aenda fundisha shule iliyo mkoa gani...Awamu hii kipaumbele sio ajira. Hata wale wa vyeti feki nafasi zao hazijajazwa.
Hivi mbona hata wale wa feki vyeti hatukuona hata kama ilisaidia wengine waajiriwe au hata mishahara kupanda?
 
Hivi mbona hata wale wa feki vyeti hatukuona hata kama ilisaidia wengine waajiriwe au hata mishahara kupanda?
ZILE ZILIKUWA NI CHUKI KAMA KISASI CHA MALIPIZI KWA BASHITE KIPENZI KUSEMWA VIBAYA
 
Sijakuelewa mtoa mada maisha magumu watu hawana Milo kwa hiyo ulitakaje yaani..uletewe chakula? Vijana wanaojielewa wanapiga kazi mchana na usiku na maisha yanaenda ukipenda vya bure Sana Kama mwanaume utaolewa bure
 
Kiuhalisia Mh. Magufuli atashinda,tena kwa asilimia kubwa sana tofauti na ilivyowahi kuwa tangu multipartism ilipoanza tena hapa bongo.
 
Hoja zikipangiliwa historia itajianza kujiweka maktaba
 
2020 watanzania tutamchagua JPM kwa kura za kutosha.
Mazuri ya JPM ni mengi sana,changamoto huwa zipo tu.hata U.S kuna raia wanalalamikia changamoto za taifa lao.
ilhali tunaambiwa U.S ni kinara wa kila jambo la kimaendeleo.
Maendeleo siyo Hisani za CCM maendeleo hayaletwi na Pesa binafsi toka mfukoni mwa mtukufu, maendeleo ni pesa za walipa kodi
 
Ndugu Mahanju, ni kweli unayoyasema; Lakini, nawaomba Watanzania tutangulize uzalendo kwanza. Uzalendo ambao ndani mwake mna kujitoa (mhanga) kwa hali na mali kwa ajili ya Nchi; kuna kujikana nafsi na kutengeneza kwa ajili ya watoto wetu, watoto wa watoto wetu, watoto wa watoto wa watoto wetu, na kuendelea.

Hebu jiulize, lipi bora, kujinyima (kwa muda) ili kile tunachokusanya tukitumie kujenga kwanza miundombinu mbalimbali (SGR, Stiglers HEP, Barabara nzuri, hospitali na vifaa tiba, eropleni, mifumo ya maji, mashule na vyuo, n.k.); Au, tukitumie kuongeza mishahara ya watumishi, na kadhalika?

Ni wazi huwezi fanya mambo yote kwa wakati mmoja. Hakutokuwa na efficiency. Lazima uwe na priority and options.
"Roma haikujengwa kwa siku moja"; hali kadhalika Ulaya magharibi au Asia. Watu walijifunga vibwebwe na leo hii vitukuu wa vitukuu ndio wanafaidi jasho la babu zao
Kwa hiyo, JPM yuko sawa. Watumishi wa Serikali na Watanzania kwa jumla, tunapaswa kujifunga mkanda na kuridhika na hiki kidogo tunachopata sasa.

Ni dhiki ya muda tu kwani tukiisha kamilisha kutengeneza miundombinu hii, Pesa inayokusanywa kutoka vyanzo mbalimbali itatumika sasa kuboresha maisha ya watu.

Tena kwa ulaiini kabisa. Serikali itakuwa na uwezo wa hata kufanya KCCCM kuwa zaidi ya 2,000/= kwa mwezi!
Mungu ibariki Tanzania.
Mungu mbariki JPM.
Mkuu nimekuelewa na ni sawa kabisa
Tatizo kwenye nchi hii wakubwa wanapokea mishahara mikubwa Sana. Mfano wabunge, hawa mishahara ,viinua mgongo na marupurupu yangepunguzwa kabisa.

Huku kada za chini ualimu na afya ambako kazi ni ngumu Maisha ni magumu Sana.

Hakuna usawa katika vipato mpaka najiuliza hivi TZ ni ya mfumo wa KIJAMAA au KIBEPARI?

JPM awamu ya pili ajitahidi pia kuboresha vipato vya wa watumishi . Hii ndio njia pekee ya kuongeza MZUNGUKO wa FEDHA nchini.
 
Ukada wa aina hii ni zaidi ya upumbavu na ulofa uliousema Mkapa.

Hao kuku unamuuzia nani watu hawana pesa. Mimi ni Daktari nimejiari,imeshatokea mara tatu kuna jamaa wametoka kijijini huko na wagonjwa wao wakabeba kuku ili wauze wapate pesa kwa ajili ya matibabu. Wamezinguka na kuku wao tena wa kienyeji hawajapata mtu wa kumuuzia mwisho wa siku wakaja kuomba niwatibu wagonjwa wanipe kuku ukabidi niwasaidie tu.
Wewe kama ni daktari basi ni wa kutibu vinyesi! Unaishi dunia gani ambayo huoni watu wakila kuku?
 
2020 watanzania tutamchagua JPM kwa kura za kutosha.
Mazuri ya JPM ni mengi sana,changamoto huwa zipo tu.hata U.S kuna raia wanalalamikia changamoto za taifa lao.
ilhali tunaambiwa U.S ni kinara wa kila jambo la kimaendeleo.

Kuna maendeleo gani ambayo JPM ameyaleta katika miaka yake mitano ya utawala? Hebu tutajie machache hapa tuweze kuyatafakari.
 
Aisee ukiendelea kuleta theories ulizosoma shuleni huwezi kufanikiwa katika maisha. Theories hizo zimetungwa na watu kama wewe, zitakusaidia tu kukupanua mawazo if you are smart kichwani. Hakuna taifa litakalokuletea maendeleo, nenda kasome economic diplomacy utaelewa ninachokuambia. Kasome how Europe underdeveloped Africa by Walter Rodney utaelewa ninachokuambia
Kwa anayetaka hicho kitabu cha Walter Rodney anicheki inbox au hats kitabu chochote kile ila siyo cha kibongo,bei ni buku tano hadi kumi,kitabu chochote kile unapata
 
2020 watanzania tutamchagua JPM kwa kura za kutosha.
Mazuri ya JPM ni mengi sana,changamoto huwa zipo tu.hata U.S kuna raia wanalalamikia changamoto za taifa lao.
ilhali tunaambiwa U.S ni kinara wa kila jambo la kimaendeleo.

Wako kabisa wengine barabarani
 
Ndugu ni wapi nimemsifia mwanasiasa hapo? Mwansiasa husifiwa na mwanasiasa mwenzake, mm sio sehemu yao. Mimi ni mpambanaji kuhakikisha naishi maisha mazuri na watoto wanasoma shule zinazoeleweka na zinazowaandaa kujitegemea badala ya kutegemea hisani za wanasiasa. By the way, unaijua historia ya Ethiopian airline au unaongea tu?

Wanasiasa ndiyo wanatunga sera,na sera ndiyo zinaweza kufanya maisha kuwa magumu au mepesi. Na wasiasa wengine wanatoa matamko tu na kuhatibu maisha ya watu. Mfano wa matamko ni lile la sukari,korosho,kahawa nk ambayo yameharibu maisha ya mamilioni ya wananchi.

Mpaka hapa nimejiridhisha ya shaka wewe ni mkuu wa vilaza hapa Jf.
 
Kilaza ni wewe na wengine aina yako ambao bado fikra zenu ni kufanyiwa kila kitu na serikali. Utaolewa usipokua makini
 
WALTER RODNEY ameandika rubbish dhana zake zinapingana na hali halisi,za kuwalaumu wazungu juu ya kushindwa kwetu na alitumika na watawala wa kiafrica baada ya kushindwa kuwaletea waafrika maendeleo tarajiwa baada ya kuwadanganya waafrica wawape sapoti wawaondoe wakoloni watakula mema ya nchi, matokeo yakawa kinyume chake,wapigania uhuru ndo wakawa wakoloni weusi kwa kuwatendea waafrika mabaya na ukatili wa hali ya juu kuliko hata mkoloni mweupe alivomtendea mwafrika kwa kuwauwa waafrika wenzao,kufisadi kodi zao,kuendekeza ukabila,kuiba na kupora mali za waafrkia na kujigeuza miungu watu huku watawala wakiishi peponi hali wakiuwa chumi nzuri za nchi zao.
Wenye akili wanamuheshimu Walter Rodney, mburula kama wewe lazima wawe na mawazo ya kipunguani yanayoshabihiana na muhanga wa risasi 16, kama mnavyodai
 
[SUB]CCM hawataki kuambiwa ukweli. "Uchaguzi huu utapaleka balaa CCM. CCM hawata amini kitakachotokea October 28. Mda ndio utasema.[/SUB]
 
Kama ambavyo siku zote nimekua nikisema kua mimi ni mkweli daima na fitina kwangu mwiko. Ni MwanaCCM hai niliyekitumikia muda mrefu na bado naendelea. Rais wangu ulikosea mambo machache sana pamoja na mengine mengi makubwa uliyofanya.

MAISHA MAGUMU KWA WATANZANIA
Mwenyekiti wangu, maisha ni magumu sana kwa watanzania wote hata mtu kupata milo miwili kwa siku ni shida. Kama wasaidizi hawasemi ukweli mkuu huko mitaani watu taabani kuliko awamu iliyopita. Watu walioko vijijini hawataki kujua Dar es salaam kuna marababara za juu au kuna Airport, hawajui kama kama kuna makubwa yamefanyika. Wao wanataka maisha mazuri.
Kiukweli akitokea mgombea atakayewaambia vizuri walalahoi hawa kura zote atapewa.

BIASHARA KUWA NGUMU
Kwa sasa maisha ya wafanyabishara yamekua magumu kabisa kila mahali kuliko awamu iliyopita, lipo tatizo kubwa ambalo kama tusiposema ukweli CCM hakuna mfanyabiashara atakayetupatia kura.

MAISHA MAGUMU KWA WAFANYAKAZI WA UMMA
Ni muda sasa wafanyakazi wa umma wanalia na maslahi duni, wengi hawana amani.
Hapa kura hatupati kabisa katika kundi hili tupende tusipende. Akitokea mgombea atakayeongea vizuri na kundi hili anaweza kuvuna kura nyingi sana na atapewa ushirikiano mkubwa .Wao wanaangalia mtu atakayewajali vizuri.

Mimi najaribu kusema msije mkasema hatukurlshauri.
Ni kweli umesema na watu wamekusikia na kukusoam humu JF vizuri; lakini yote uliyosema ni kama unazungumzia na kuwasemea Watanzania wasioziona fursa za kazi (hapa nina maana ya kazi za kujiajiri siyo KUAJIRIWA), wasio ziona fursa za biashara, ziwe ndogo au kubwa au wasio ziona fursa huko kwenye ARDHI HII YA AJABU tuliyopewa na Mungu ambayo majirani zetu na wageni kutoka nje wanaimezea mate kufa na kupona. Anyway nadhani ni suala la mtazamo na MINDSET ya kila mmoja wetu kwenye hoja hizo. Ila binafsi nadhani hata wasomi wa ngazi ya elimu ya juu wameanza kuuona ukweli wa ulazima wa KUJIARI, na hata watu wa kawaida siku hizi wameelewa kuwa Tanzania hii ya +255 SIYO MASKINI na suala la watu kujituma na kuchangamkia fursa zilizopo hapa nchini limeeleweka kwa wengi. Hoja hizo hizo zinawahusu pia wafanyakazi wa umma, siku hizi wana fursa nyingi za mikopo ya kuwawezesha kujijasiriamali na hivyo kupunguza makali ya mshahara. Halafu hakuna mahali popote duniani, ambapo MSHAHARA ULISHAWAHI KUMUONDOA MTU KWENYE UMASIKINI WA KIPATO. HAKUNA. Tujitume tushinde vita hii ya umasikini.
 
Back
Top Bottom