Mwenyekiti yupo Mahabusu, Makamu Mwenyekiti anaugulia risasi 16, viongozi wakaunga juhudi mkono lakini bado chama kipo imara. MUNGU ana makusudi

Mwenyekiti yupo Mahabusu, Makamu Mwenyekiti anaugulia risasi 16, viongozi wakaunga juhudi mkono lakini bado chama kipo imara. MUNGU ana makusudi

Naamini kabisa kwamba CCM wanajua akina halima ni wahanga waliotetea uhai wao baada ya kuona madhila waliyopata wapinzani webgine. Tuliona walivyofikishwa kwenda kuapa na eneo walipokaa wakaapa utabaini kabisa walikuwa mateka. Hakuna anayejua walipewa madharti Gani wakati
Hiki ndicho tunachoamini. Wale ni mateka. Ni wahanga. Ndio maana hata chama hakihangaiki nao.
 
Hakika. Ni swala la muda tu. Mbowe kuwa ndani ni kazi ya system, Lissu amepona kwa sababu system haikutaka afe!

Punde si Punde, Historia itabadilika
Kazi ya system.....imaginary system vs Karma
 
Hakika. Ni swala la muda tu. Mbowe kuwa ndani ni kazi ya system, Lissu amepona kwa sababu system haikutaka afe!

Punde si Punde, Historia itabadilika
Akili yako mbovu sana kaka,
 
Wait a minute!!
Chama gani kipo imara dada?!!!!!!!!

Mi ndo huwa maeneo haya tu yanayonipa raha ya kuendelea na kufuatilia siasa.....utasikia;
'Tuna wafuasi milioni 12!'
'Subirini 2015', ikifika utasikia, 'subirini 2020'!
'Sisi tunaanza na Mungu na tunamaliza na Mungu', huku michango ya wztu inaliwa na nafasi kuminywa!
 
N
Hivi nani aliyekudanganya chadema kipo?
Wale wabunge 19 wameidhinishwa na mbowe,hivi unajua kuwa mfano ester matiko ni mzazi mwenzie na salum mwalimu,unadhani salum mwalimu atakubali mkewe afukuzwe bungeni,watoto wakose maisha?

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
Na wewe unatakiwa uwe replaced na kichwa kimoja kutoka Cdm. Ukute Ni kiongozi wa ccm ndo mwenye akili ya hivi!!!
 
Chama cha CUF kimekufa bila mwenyekiti wala kiongozi wao kunyanyaswa waziwazi, walishughulika na matumbo ya viongoz chama kikafa.

NCCR ilisambaratishwa bila viongozi kupitia magumu ya Chadema.

ACT inajijenga kwa kujimomonyoa kwasababu Toka mwanzo ilianzishwa kupambana na Chama alichotoka mwasisi wake na siyo kupambana mfumo kwa lengo la kushika dola.

Chadema imepoteza makatibu wakuu wawili Hawa ndio walikuwa waandaaji wa kila kitu kwenye chama wote leo wapo CCM. Tuliamini wakienda huko wataenda na Siri za chama kumbe chama hakina Siri kubwa zaidi ya kusimama na wananchi. Hii NDIYO Siri pekee ya Chadema na inaimarika kwasababu pamoja na kuwa na Watu wenye njaa Lakini wapo wachache wasiojali ukubwa wa njaa.

Leo hii kutokana na ukubwa wa Chadema wapo watu waliamini Chadema ni lisu wakaangaika naye lakini akiwa kitandani na nje ya Nchi chama kiliendelea.

Wapo walioamini chadema ni Mbowe, wakamweka ndani mwaka sasa lakini chadema Bado kipo imara. Maana yake ni kwamba ; lipo tatizo la watafiti nchini.

Ninachokiona Mimi ni kwamba, mfumo umekichoka Chama tawala hivyo umewekeza kuitengeneza Chadema iwe imara Ili watu waliopo Chadema watakapopewa madaraka na kukabidhiwa Nchi basi Nchi isonge. Tumeona mfumo ulivyomtumia JPM kutafuta watu wenye akili kutoka Chadema na kuwapa teuzi, tumeona mfumo ulivyopeleka wamama wenye akili 19 Bungeni wakalisaidie taifa baada ya kuona hakuna mbunge wakutoa hoja aliyepelekwa Bungeni na CCM, tuone mfumo ulivyowanunua akina badhiru wakairarue CCM nk

Nasema hivi Kwa sababu ni dhairi kwamba watu wanaofikiri sawasawa nchini wapo Chadema na ukitaka upate watu wa kukusaidia lazima ukawanue Chadema uwakumbatie huku ukujua kabisa kwamba moyoni mwao ni wanachadema na si wana CCM.

Naamini kabisa kwamba CCM wanajua akina halima ni wahanga waliotetea uhai wao baada ya kuona madhila waliyopata wapinzani webgine. Tuliona walivyofikishwa kwenda kuapa na eneo walipokaa wakaapa utabaini kabisa walikuwa mateka. Hakuna anayejua walipewa madharti Gani wakati wanatekwa na kupelekwa kwa Ndugai. Waliapishwa sehemu ambayo haijawahi kutumika kuapisha wabunge katika uhai wa nchi hii. Lakini pia kati yao akaapishwa hata aliyetolewa mahabusu you can imagine walikuwa wana Hali gani na walikuwa ni watu muhimu kiasi gani katika kulitetea bunge lisipitishe mambo ya hovyo. Let assume mfumo umetumia plan B kutafuta viongozi nje ya plan A ambayo imefeli.

Tukumbuke mfumo Siku zote unakuaga na wivu uliojichimbia chini ambao nivigumu kuonekana kwa macho. Tukumbuke mfumo una watu wa kila kariba. Unaweza ukadhani unaongozi kumbe unaongozwa. Unajiweka busy kupngoza watu wanakaa busy kukuongoza
Kweli tupu
 
Chadema inapambana na dola iliyojivika siasa siku dola ikiichoka ccm mtajua hamjui
Wait a minute!!
Chama gani kipo imara dada?!!!!!!!!

Mi ndo huwa maeneo haya tu yanayonipa raha ya kuendelea na kufuatilia siasa.....utasikia;
'Tuna wafuasi milioni 12!'
'Subirini 2015', ikifika utasikia, 'subirini 2020'!
'Sisi tunaanza na Mungu na tunamaliza na Mungu', huku michango ya wztu inaliwa na nafasi kuminywa!
 
Kamwe hawawezi kuua chadema kwa kuwaumiza au hata kudhulumu maisha ya wengine!
Bado watazaliwa mbowe 30 na Lissu 30 wengine, Tulianza na Mungu na tutakuwa na Mungu milele.
 
Back
Top Bottom