KALINZI NYUMBANI
JF-Expert Member
- Jan 7, 2015
- 1,797
- 1,594
Huwa nachukia watu wanaowasema vijana wakibongo hivi, vijana wakibongo vile. Kwani ni raia wa nchi gani ambao sio wapigaji?. Kwenye Kila taifa lazima liwe na hao watu. Au kwa vile mnaajiri wahindi wanawaibia kisha wanaenda kujenga magorofa kwao kwa vile hampajui wanapotoka basi mnadhani wao sio wapigaji?. Na kama nihivyo mbona tunaona baadhi ya wabongo wameshika nyadhifa nzuri tu kwenye baadhi ya private company?.Kijana wa kitanzania akiajiriwa sehemu yoyote ile kitu Cha kwanza kinachomuijia akilin ni namna gani atatimiza malengo yake binafsi kwa haraka kupitia kazi hiyo na atafanya juu chini hili ajue kama Kuna mwanya wowote wa kujiingizia pato la ziada kinyume na utaratibu(ubadhirifu) nje na mshaara anaolipwa..... Na ikitokea amekosa loophole yoyote ya upigaji anajikuta ghafla anauchukia hiyo kazi.
Ni wachache sana ambao huwa wanafikiria kuleta ufanisi wao kwa 100%, wao vipaumbele vyao ni mishaara na upigaji.
Muda wa kazi wenyewe hawautumii ipasvyo, unakuta wakienda kunywa chai wanatumia masaa 2 na Bado wakiwa wanafanya kazi concentration hamna, muda mwingi simu ziko mkononi anaangalia nini kinatrend mjini,
Boss yeyote anaejielewa atahakikisha mfanyakaazi wake hawazi chakula na maradhi hivyo inakua ni uhakika Ili kumpa utulivu wa akili afanye kazi vizuri.
Mtu anafanya kazi wamlipa let's say mil 7 per month au 10. Chakwanza atakachokiwaza nikutimiza majukumu yake Ili asipoteze hio kazi.
Wewe unalipa mtu laki Tano, sijui laki 8 unataka asikuibie?. Huku wewe unaingiza mabilion ya Fedha?. Waajir lipen wafanyakazi wenu kadri ya mapato yenu. Otherwise mtaibiwa mbaki mnalialia.