Mwenyezi Mungu, nifanye lipi ili ujibu ombi langu, niwe vipi ili unitue mzigo huu? Mbona ni kama umenifumbia macho hunioni

Usichoke endelea kupambana na kusali, hata ukifa Leo, utasema nilikuwa mwaminifu mpaka mwisho.
 
Ndg, salaam!
Pole kwa changamoto za dunia.
Nakusihi usikate tamaa,ukikata tamaa umekubali kushindwa.
Soma kitabu cha Habakuki katika Biblia,sali sana na sikiliza nyimbo hii;
Shida za Dunia-ya Josee Chameleon
Zikutie moyo, never give up bro!
 
Kitabu cha Wafilipi kinatuasa kushukuru kwa kila jambo.
 
Embu ngoja.
 
Nikufundishe dua bora? Sema
Rabbi ini lima anzalta ilayha min khairin faqir

Kwa kiswahili " Eeh Mwenyezi Mungu hakika mimi ni muhitaji wa kila kheri utakazonipa"
Yule shehe anapiga hii na bado analalamika Waislam hawatoi sadaka.
 
Yule shehe anapiga hii na bado analalamika Waislam hawatoi sadaka.
Hiyo siyo dua ya kuombea Sadaka na pia katika uislam sadaka siyo lazima itolewe msikitini, kama unataka ya kuombea sadaka kawaone wachungaji katika uislam hamna dua hiyo
 
Ndugu nimefanya kwa siku 30

Na siku nyingine pia
😢😢😢
Unasoma neno biblia kila siku asubuhi, mchana, na jioni ? Mungu anasikiliza mateso ya wengi jitahidi kuombea makundi mengine Kuna watu wanaoteseka kuliko wewe
Jifunze Mungu anavyotoa baraka nimeandika hapa kwenye Uzi huu post ya mwisho
 
Shirki hiyo, unamshirikisha Mungu kwenye huo ulozi wa chumvi?
Chumvi ni ya kuweka kwenye chakula siyo kujipata ili Mungu akusikie.
 
Tumchangie mawazo na kiuchumi mbona kama unawaza kujiua.....
 

View: https://youtu.be/Oba3O_6X02U?si=ExyZWHTXZJs2xwWN
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…