Bujibuji Simba Nyamaume
Platinum Member
- Feb 4, 2009
- 78,914
- 168,320
Mwezi wa March ni mwezi wa haki kwa taifa la Tanzania.
Mwezi March Mungu amekuwa akiwapa kicheko Watanzania wanaoonewa na kukandamizwa na udhalimu wa watawala dhalimu.
Mwezi March mwaka jana taifa lilijawa na milango wazi ya haki, usawa, na furaha kwa watu wengi.
Waliofungwa kwa kusingiziwa walifurahi, waliobambikiwa mzigo wakodi wakafurahi, waliokuwa wamepewa kesi za uhujumu uchui na utakatishaji wakafurahi.
Mwaka huu mwezi March tena, Mungu ametufurahisha wapenda haki.
Aliyekuwa ndani kwa kesi ya mchongo ya ugaidi yuko huru. Yuko huru kwelikweli.
Unamsingizia mtu ugaidi, eti anataka kulipua nchi, hujamkamata na vilipuzi.
Eti anataka kukata miti kutoka Dar hadi Mbeya, hujamkamata na msumeno, panga wala shoka, je hiyo miti angeikata kwa Bluetooth?
Mungu endelea kutufurahisha mwezi March