FRANC THE GREAT
JF-Expert Member
- May 27, 2016
- 5,500
- 8,060
Habari!
Mara nyingi tumekuwa tukijiuliza maswali mengi kuhusiana na masuala mbalimbali yahusuyo Mwezi. Sio ule wa kwenye kalenda bali huu tuuonao angani karibu kila iitwapo leo hasa nyakati za usiku. Yeah, huohuo kama duara fulani linalong'aa.
Kwa muda mrefu sasa tafiti mbalimbali zimekuwa zikifanyika ili kuweza kubaini mambo mbalimbali kuhusiana na Mwezi na tafiti zimekuwa zikileta majibu tofauti tofauti. Utafiti mpya uliofanyika hivi karibuni umebaini kuwa, Mwezi una umri mdogo sana kuliko tulivyofikiria ama tulivyokuwa tukifahamu hapo awali, pungufu ya miaka takribani milioni 85 hivi. Je, unaamini hilo?
Subiri hapohapo!
Kulingana na nadharia inayokubalika na watafiti mbalimbali, Mwezi uliumbwa kutoka katika vipande vipande vilivyotokana na mgongano kati ya Dunia na sayari ndogo inayoitwa Theia, nadharia inayofahamika kama The Giant Impact Hypothesis pia ikijulikana kama Big Splash. (Tazama mfano katika mchoro uliopita).
Vipande hivyo vilivyo katika myeyuko hatimaye viliungana na kuwa mwili mmoja ambao ulianza kuzunguka dunia, ndio huo Mwezi unaouona angani karibu kila siku ndugu msomaji wa bandiko hili.
Maana yake ni kwamba, sehemu ya mwamba ambao ulifanikisha kufanyika ama kuumbwa kwa Mwezi ulitokea duniani, na unaweza kutumika hadi leo kuweza kubaini umri wake. Utafiti unaonesha kuwa Mwezi uliumbwa wakati ambao Dunia ilikuwa ikikaribia kuumbwa kikamilifu. Tazama mchoro ufuatao jinsi ambavyo mchakato huo wa kufanyika kwa Mwezi unavyoaminika kutokea kama inavyoonekana katika matukio hayo manne.
Researchers have long believed the Moon formed as a result of a cosmic collision between an Earth that was still forming and another planetoid, commonly known as Theia.
Utafiti huu mpya kuhusu umri wa Mwezi umefanyika nchini Ujerumani kupitia shirika la anga za juu la nchi hiyo Deutsches Zentrum für Luft- und Raumfahrt ama kwa kifupi DLR.
Kabla sijaendelea mbele zaidi,
Nikupe pole ndugu msomaji uliyekumbana na changamoto pale ulipojaribu kulitamka hilo jina la hilo shirika la Ujerumani ila kwa lugha nyingine unaweza kuliita, German Aerospace Center.
Kulingana sasa na huu utafiti 'wetu' mpya, Mwezi una umri wa miaka takribani bilioni 4.425, miaka ambayo ni milioni 85 pungufu kutoka umri uliokuwa ukidhaniwa ama kufahamika hapo awali wa miaka bilioni 4.51. Are you there?!
Watafiti 'wetu' pia walibaini kuwa Mwezi ulikuwa na bahari ya magma wakati mchakato wa kuumbwa kwake ukiendelea.
BAHARI YA MAGMA
Hili ni tabaka la mwamba myeyuko linaoaminika kuwepo katika umbo la dunia na sayari nyinginezo wakati uumbwaji wa sayari hizo unapokuwa ukikamilishwa.
Magma oceans exist during periods of Earth's or any planet's accretion when the planet is completely or partly molten. A magma ocean also occurred on the Moon during and following its formation. [Wikipedia]
PICHA: Mfano wa mwezi ukiwa na bahari ya magma.
Katika harakati za kulibaini hilo pengo la miaka milioni 85, watafiti walitumia miundo ya kimahesabu kuweza kuubaini muundo wa Mwezi katika kipindi chote cha uwepo wake, wakitumia bahari ya magma niliyoielezea hapo awali kama msingi katika utafiti wao.
Kulingana na wazo hilo kwamba Mwezi ulikuwa na bahari kubwa ya magma, watafiti walihesabu jinsi madini yaliyofanyika kutokana na kupoa na kuganda kwa magma yalivyokuwa yakibadilika kuendana na muda. Kwa kufuata mbadiliko wa bahari ya magma, wanasayansi waliweza kuufuatisha na kubaini muda na wakati wa uumbwaji wa Mwezi.
Nisiwachoshe ila haya ni kati ya yale yaliyojiri katika utafiti huu mpya pia ni machache tu katika yale yaliyokusanywa katika tafiti zingine kadha wa kadha zilizowahi kufanyika katika miaka ya nyuma zinazohusiana na umri sahihi wa Mwezi. Zaidi yaliyojiri katika tafiti tutapata kuyajua hapo baadaye. Asante na karibu kwa maoni yako kuhusiana na hili!
FRANC THE GREAT,
Semper magnas.