Haupo huko wakati maji yanafanya athari ?Kuruhusu maji kufanya hivi ama vile ni jambo jingine. Mimi siko huko bali niko hapa; hilo bonde limetoka wapi? Nani kalileta hapo? Kwanini liitwe bonde?
Why "bonde"?
Yameumbwa na Mola muumba mwenye hizo sifa zote hapo juu nilipo kutajia. Mwenye uwezo, mwenye kujua, mwenye malengo, mwenye hekima.Sifa ya muumbaji nimekwisha kukutajia hapo. 'Uwezo wa kuumba'. Kukifanya kitu fulani ambacho hakikuwepo na kukiunda kikawepo katika muonekano fulani ndio huo uumbaji. Hayo maumbo ya kijiografia niliyoyasema hapo awali yenye majina tofauti tofauti kutokana na muonekano wake yameumbwa na kitu gani?
Swali langu liko pale pale na hulikwepo,nithibitishie tu ya kuwa hayo maumbo yamesababishwa na UPEPO usipate tabu. Hili ndiyo swali la msingi.Mimi sipo hapo kwenye sababu ya kuwepo kwa upepo.
Narudia:
Mimi sizungumzii kuhusu chanzo cha upepo wala chanzo cha kuwepo maji. Ninachokisema hapa ni sababu ya kuwepo kwa hayo maumbo mbalimbali ya kijiografia yenye majina tofauti tofauti na muonekano tofauti tofauti. Hayo maumbo yamekuwepo kutokana na kitu gani?
Kwamba UPEPO ndiyo umesababisha haya maumbile, au unasoma bila kuelewa nini mzee ? Halafu natumia lugha rahisi sana. Mfano, naomba unithibitishie ya kuwa Mlima Kilimanjaro umesababishwa na UPEPO ndiyo maana ukawepo.Unahitaji uthibitisho upi kuhusiana na kuumbika kwa maumbo hayo?
Nafahamu kuhusu Jiografia ni kuwa wanajaribu kuelezea maumbo ambayo yapo na ilikuwaje yakawepo, kwa kutumia mawazo yao binafsi bila ushahidi wowote wa kielimu.Unafahamu uwepo wa maumbo ya kijiografia? Unafahamu maana ya 'umbo'?
Nina fahamu vizuri sana maana ya umbo.
Hakuna aliyesema yanatokea out of nowhere" ila tunataka ututhibitishie ya kuwa haya unayo sema ni ya kweli au huwa mnasema ili kujifurahisha tu ?Ushahidi ni kupitia maumbo ya kijiografia ambayo yapo katika mazingira yetu hayahaya tunayoishi kila siku. Hayo maumbo yanatokea tu papo hapo, out of nowhere?
Hii ni hoja tena hoja ya msingi sana, na huthibitisha ukweli wa muumbaji, vipi aumbe pasi na kujja alichokiumba ? Ndiyo maana nilikwambia uwezo siyo tu sifa pekee ya muumbaji, bali ufahamu na lengo hazikwepeki, ona sada hiki kidogo tu cha majina kina kushinda na kinaonyesha lazima muumbaji ajue hili.Mtoa majina ya maumbo hayo si hoja bali hoja ni kile kilichosababisha kuwepo kwa maumbo hayo mbalimbali katika mazingira yetu.