Hilo bonde limetokeaje pasipo kuumbwa na maji? Na kabla ya hapo, kwanini liitwe "bonde" kama si umbo fulani linalopelekea kuitwa jina hilo? Je, hilo bonde limewekwa na kitu chenye zile tabia ulizozitaja pale awali?
Labda nikusaidie hapa, unaweza kunips sifa za muumbaji ? Mathalani kwako wewe unakusudia muumbaji ni "Maji". Yaani mathalani wewe unaweza kumuita 'mchora tattoo" ni muumbaji kisa amekuwa sababu ya kuwepo kwa tattoo kwa mtu husika, na hivi ndivyo ilivyo kwa maji, yaani maji yameleta athari kwenye jambo ambalo lipo tayari, na huku hapaitwi au hakuitwi "uumbaji" ,mathalani tunaposema "Binadamu ameumbwa ujue hapakuwa kabla yake na mfani wake".
Bila shaka kabisa, bonde hilo limewekwa na msabishaji mkuu, ambae ameruhusu maji yawe ni sehemu ya sababu ya kutokea jambo hilo, huku akiwa na uwezo, ufahamu na lengo juu ya kuwepo kwa bonde hilo.
Kabla ya hapo halikuitwa bonde, ila baada ya athari ya kupita kwa maji mara kwa mara pakatokea bonde hilo, na kuitwa bonde.
Mimi wala silazimishi mambo bali nakujibu kuendana na hoja zako. Hoja yako kuhusiana na "muumbaji" ina mapungufu ambayo mtu yeyote makini anaweza kuyatumia mapungufu hayo kuku-challenge
Kwa hili huwezi kuni "Challange" sababu udhaifu wako upi wazi na nimeuona mapema sana, kwa wewe kutokujua maana ya tamko "uumbaji" na ni yapi masharti au sifa za tamko hilo.
Upepo hauwezi kufanya hilo kivipi? Upepo ndio chanzo cha maumbo hayo ya kijiografia kutokea. Kabla ya upepo kufanya kazi yake, maumbo hayo hayakuwepo. Kweli, si kweli?
Wewe nithibitishie tu, ili tuone kwamba hili unalo liandika ni kweli au si kweli.
Upepo wenyewe umeumbwa au haujaumbwa na kipi kinafanya upepo uwepo na uwe sababu ya kuwepo kwa maumbo yote haya ?
Maumbo hayo yamekuwepo kwa sababu yameumbwa na upepo. Je, upepo una zile sifa zote ulizozitaja?
Kaka inakuwaje unafikia hitimisho kabla hujatuthibitishia ukweli wa unacho dai ya kuwa upepo ndiyo umeumba haya maumbo ?
Ndio! Naendelea kuuonesha huo wepesi.
Mpaka muda huu hujaonyesha hilo, sababu kadiri unavyo elezea ndiyo unazidisha maswali ambayo hayana majibu.
Sizungumzii chanzo ama kisababishi cha upepo kuwepo..la hasha! Bali nazungumzia chanzo cha maumbo hayo mbalimbali ya ardhini kuwepo.
Hili haliepukiki, sababu huwezi kuelezea hili bila kujua upepo ni nini na umetokana na nini na kwa lipi uwe chanzo cha uwepo wa maumbile haya. Mathalani nikikuuliza wewe ni ipi kazi ya Milima katika mgongo wa ardhi bila shaka utaniambia, nitakuuliza swali je kwanini au kwa vipi kile ambacho ndiyo sababu kisiwe na malengo na ufahamu wa kufanya milima iwepo ? Kwako wewe hapa una dai ni UPEPO.
Je, maumbo mbalimbali ya kijiografia katika ardhi yetu hii yametoka wapi pasipo kuumbwa?
Mimi sikatai kama hayajaumbwa ila tunapingana juu ya nani ambaye ameyaumba haya maumbile. Wewe unasema ni upepo, na hapa nasubiri unipe ushahidi wa hilo.
Na si hapo tu bali maumbo hayo yamepewa mpaka na majina kuonesha utofauti wa umbo moja na jingine. Je, yameumbwa na kitu gani?
Suala la majina ni suala lingine ambalo kiuhalisia upepo wenyewe ndiyo ungetupa majina ya kile ilicho kiumba, lakini ajabu majina ya hayo maumbo yametolewa na mwanadamu.