Hili tamko umelitumia kimakosa, sababu maelezo yako yanaashiria kilicho husika hapo, hakina ufahamu, hakina utashi, hakina lengo, hakina uwezo na hakina hekima.
Nini, nakusudia hapo, ni kuwa ili kitu kiumbwe lazima awepo muumbaji na muumbaji awe na sifa hizo tano nilizo zitaja hapo juu. Namaanisha ya kuwa tafuta neno muafaks uliweke hapo ila tamko "kuumbwa" halikai hapo kwa vyovyote vile.
Naendelea....
Neno hilo linafaa kabisa kuwa hapo kama kiashirio cha mchakato wa kufanyika kwa kitu fulani. Kwa lugha nyingine naweza kusema "formed". Ukizipitia hizo nadharia mbalimbali utapata kufahamu jinsi neno hilo lilivyotumika.
Pia neno "kuumbwa" si lazima lihusishwe na mtu ama kitu chenye hivyo vitu ulivyovitaja hapo bali linaweza pia kutumika kwa namna nyingine. Mfano; maji yana uwezo wa kuumba vitu mbalimbali katika mazingira yetu tunayoishi kila siku. Kwenye Geography huko kuna vitu kama vile gullies pia kuna masuala ya water erosion na matokeo yake ya kufanyika kwa landforms mbalimbali.
Upepo pia unaweza kufanya vivyo hivyo. Kuna vitu kama vile mushroom rocks, sand dunes na kadhalika.
Kutumia vitu hivyo vitano ulivyovisema; ufahamu, utashi, lengo, uwezo pamoja na hekima kama sifa za muumbaji ni hoja nyepesi ambayo kwa kawaida inaweza kuwa challenged kirahisi sana.
Katika mfano niliyoutoa hapo kuhusiana na masuala ya kijiografia, sidhani kama maji pamoja na upepo vimekithi vigezo vyote hivyo ulivyovitaja lakini vitu hivyo viwili vinaweza kuumba maumbo mbalimbali ya kimazingira. Je, upepo au maji yana ufahamu? Je, yana utashi? Je, yana lengo? Uwezo je? (pengine). Hekima je?
Kitu kingine ni kuhusiana na tafsiri wa neno "muumbaji".
Kwa tafsiri ya kawaida, "muumbaji" ni kitu chochote chenye uwezo wa kuumba, haijalishi kitu hicho kina uhai ama kisicho na uhai. Pia, ipo tafsiri nyingine ya "Muumbaji" katika upande wa kiimani. Nafahamu hilo na pengine ndio tafsiri ambayo unaitumia katika hoja yako. Huo ni mjadala mwingine katika upande mwingine kama nilivyosema hapo awali.
Kinachopo hasa katika nadharia ya kisayansi kuhusiana na "kuumbwa" kwa Mwezi ni mchakato wa kufanyika kwa Mwezi katika hali ya utaratibu au kwa lugha nyingine 'gradually' kama nilivyosema hapo awali kupitia mabadiliko mbalimbali katika vipindi tofauti tofauti mpaka kufikia kukamilika kwake.