Mwezi una umri mdogo kuliko tulivyodhani! Je, unaamini?

Hiyo ni scientific hypothesis yenye kuelezea masuala mbalimbali kuhusiana na kufanyika kwa Mwezi ambayo kisayansi, ni lazima ijaribiwe zaidi na zaidi. Hiyo ni kikanuni kabisa katika sayansi.

Nadharia yeyote inasimama kama "scientific" kupitia majaribio na tafiti mbalimbali. Ndio sayansi yenyewe hiyo.
 
Hili tatizo lingine naona unalazimisha mambo kwa lipi huko kuitwe kuumba ? Kinacho umba lazima kiwe na hizo sifa.
Mimi wala silazimishi mambo bali nakujibu kuendana na hoja zako. Hoja yako kuhusiana na "muumbaji" ina mapungufu ambayo mtu yeyote makini anaweza kuyatumia mapungufu hayo kuku-challenge.
Kwa mfano maji huwa tuna sema mathalani "Bonde hili ni matokeo ya mvua kubwa iliyo nyesha wiki iliyo pita" na hakuna lugha inayo kubali ya kuwa Mvua imeumba.
Hilo bonde limetokeaje pasipo kuumbwa na maji? Na kabla ya hapo, kwanini liitwe "bonde" kama si umbo fulani linalopelekea kuitwa jina hilo? Je, hilo bonde limewekwa na kitu chenye zile tabia ulizozitaja pale awali?
Upepo hauwezi kufanya hilo, bali unakuwa ni sehemu ya matikeo ya hicho unacho kidai,ila kuhusu uumbaji lazima kihusike kabla ya kuwepo na kuja kuwepo kitu hicho.
Upepo hauwezi kufanya hilo kivipi? Upepo ndio chanzo cha maumbo hayo ya kijiografia kutokea. Kabla ya upepo kufanya kazi yake, maumbo hayo hayakuwepo. Kweli, si kweli?

Maumbo hayo yamekuwepo kwa sababu yameumbwa na upepo. Je, upepo una zile sifa zote ulizozitaja?
Safi kabisa, onyesha wepesi wa hoja hii.
Ndio! Naendelea kuuonesha huo wepesi.
Sizungumzii chanzo ama kisababishi cha upepo kuwepo..la hasha! Bali nazungumzia chanzo cha maumbo hayo mbalimbali ya ardhini kuwepo.

Je, maumbo mbalimbali ya kijiografia katika ardhi yetu hii yametoka wapi pasipo kuumbwa? Na si hapo tu bali maumbo hayo yamepewa mpaka na majina kuonesha utofauti wa umbo moja na jingine. Je, yameumbwa na kitu gani?
 
Hayo mawazo binafsi hayapokelewi tu bila kupimwa. Nadharia yeyote ya kisayansi ni lazima ipitie majaribio. Ni lazima iruhusu kujaribiwa, kuhojiwa, kupimwa na kufanyiwa utafiti.

Uwepo na mtu wa mwanzo wa kushuhudia jambo sio lazima katika evidence gathering bali ni ushahidi uliopo unaoweza kuthibitisha kutokea kwa jambo fulani hapo zamani. Available facts!
 
Kwa mtazamo wangu, hizi ni nadharia za kisayansi. Kuja kwake ni sahihi katika ulimwengu wa kisayansi kwa sababu ni lazima tuhoji masuala mbalimbali yaliyomo humo. Kuhoji na kuipima nadharia hiyo ni kanuni ya kisayansi.

Nadharia yeyote ya kisayansi inayokubalika ni ile inayoweza kutoa majibu ya masuala mbalimbali na muhimu kuhusiana na jambo fulani. Hiyo ndio starting point. Baada ya hapo ni kuipima nadharia hiyo, ni kuijaribu kisayansi ili kuthibitisha masuala mbalimbali yanayoambatana na nadharia hiyo.

Hakuna kuridhika hapo bali ni mwendo wa kuhoji na kutafiti.
 
Safi kabisa, jambo ambalo halina ithibati linafanyiwa vipi kazi kisayansi ? Vipi kuhusu hitimisho la jambo hilo ? Rejea hiki ulichokiandika.

Kwahiyo hii ni nadharia ya kisayansi si ndiyo ? Hivi huoni kwamba kwa mtindo huu mtakuwa mnakosea maisha yenu yote ? Kufanyia kazi jambo ambalo kwa vyovyote vile halina ushahidi.
Sahihi kabisa, hivi unafikiri hawa Wanasayansi mpaka kufikia kuhitimisha jambo ubafikiri wali hoji kwa usahihi ? Tatizo siyo kuhoji, tatizo ni je mnahoji kwa usahihi ?

Kwa mfano wewe, uliposikia habari hii kwa mara ya kwanza ulihoji vipi na je hitimisho lake vipi liwe la kweli hali ya kuwa msingi wa habari ni wa kufikirika na usio na ushahidi kwa hali yoyote ile ?
 
Sasa hili jambo mbona linaonyesha wazi kabisa hamja hoji, maana laiti kama mngekuwa mmehoji msingefikia kufanya utafiti juu ya jambo ambalo halina msingi wa ukweli, wala ushahidi zaidi ya mawazo ya mtu tu. Sidhani kama ni kweli nadharia yoyote ya Kisayansi lazima ipitie kwenye majaribio, mathalani unaweza kuniambia ni jaribio gani la kisayansi lililo fanyika na kuonyesha ya kuwa Dunia inazunguka au ipo katika mwendo na jaribio gabi la Kisayansi lililo fanyika na kuhitimisha ya kuwa Jua halipo katika mwendo ?

Au labda unisaidie unaposema "kuhoji" kwa mujibu wa Sayansi huwa mnakusudia nini ?
 
Kwa mtazamo wangu, hizi ni nadharia za kisayansi. Kuja kwake ni sahihi katika ulimwengu wa kisayansi kwa sababu ni lazima tuhoji masuala mbalimbali yaliyomo humo. Kuhoji na kuipima nadharia hiyo ni kanuni ya kisayansi.
Kwa mtindo huu ndiyo maana Sayansi ina sanaa nyingi na kulazimisha mambo.

Kwanini msinge hoji kwanza kwa usahihi, ya kuwa hizi habari amezipata wapi kabla ya kuanza kuzifanyia kazi ? Maana kwa lugha nyepesi huu ni utunzi tu kama utunzi mwingine.

Hivi kwa akili ndogo tu, hivi unafikiri hitimisho litakuwa sahihi kwa jambo ambalo halithibitishiki ? Wakubwa zangu waliniambia ya kuwa "Sayansi inakumbwa na tatizo kubwa sana, la namna ya kufikia hitimisho juu ya mambo yake", huu ukweli uko wazi sana.
Hakuna kuridhika hapo bali ni mwendo wa kuhoji na kutafiti.
Kwa mfano embu tuambie kwa nadharia hii ya umri wa mwezi, wewe ungeanza kuhoji vipi. Embu tuelekeze.
 
Uwepo na mtu wa mwanzo wa kushuhudia jambo sio lazima katika evidence gathering bali ni ushahidi uliopo unaoweza kuthibitisha kutokea kwa jambo fulani hapo zamani. Available facts
Na hii habari lazima iwepo na mtu wa mwanzo ili kuujua ukweli wake, kinyume chake hata nyinyi mnapo ifanyia lazima mkosee katika hitimisho, sababu mwanzo wake kabisa unathibitisha habari hii ni ya UONGO.
 
Jambo lipi hilo ambalo halina asili?
Hili la hii nadharia.
Unaweza kufanya utafiti kwa jambo ambalo halijawahi kuwepo ?

Hili la kwenye mada ni miongoni mwa mambo ambayo hayakuwahi kuwepo, vipi ufanye utafiti zaidi ya sanaa na ubunifu tu ili kuafikiana na mawazo ya mbunifu...!
 
Hilo bonde limetokeaje pasipo kuumbwa na maji? Na kabla ya hapo, kwanini liitwe "bonde" kama si umbo fulani linalopelekea kuitwa jina hilo? Je, hilo bonde limewekwa na kitu chenye zile tabia ulizozitaja pale awali?
Labda nikusaidie hapa, unaweza kunips sifa za muumbaji ? Mathalani kwako wewe unakusudia muumbaji ni "Maji". Yaani mathalani wewe unaweza kumuita 'mchora tattoo" ni muumbaji kisa amekuwa sababu ya kuwepo kwa tattoo kwa mtu husika, na hivi ndivyo ilivyo kwa maji, yaani maji yameleta athari kwenye jambo ambalo lipo tayari, na huku hapaitwi au hakuitwi "uumbaji" ,mathalani tunaposema "Binadamu ameumbwa ujue hapakuwa kabla yake na mfani wake".

Bila shaka kabisa, bonde hilo limewekwa na msabishaji mkuu, ambae ameruhusu maji yawe ni sehemu ya sababu ya kutokea jambo hilo, huku akiwa na uwezo, ufahamu na lengo juu ya kuwepo kwa bonde hilo.

Kabla ya hapo halikuitwa bonde, ila baada ya athari ya kupita kwa maji mara kwa mara pakatokea bonde hilo, na kuitwa bonde.
Mimi wala silazimishi mambo bali nakujibu kuendana na hoja zako. Hoja yako kuhusiana na "muumbaji" ina mapungufu ambayo mtu yeyote makini anaweza kuyatumia mapungufu hayo kuku-challenge
Kwa hili huwezi kuni "Challange" sababu udhaifu wako upi wazi na nimeuona mapema sana, kwa wewe kutokujua maana ya tamko "uumbaji" na ni yapi masharti au sifa za tamko hilo.
Upepo hauwezi kufanya hilo kivipi? Upepo ndio chanzo cha maumbo hayo ya kijiografia kutokea. Kabla ya upepo kufanya kazi yake, maumbo hayo hayakuwepo. Kweli, si kweli?
Wewe nithibitishie tu, ili tuone kwamba hili unalo liandika ni kweli au si kweli.

Upepo wenyewe umeumbwa au haujaumbwa na kipi kinafanya upepo uwepo na uwe sababu ya kuwepo kwa maumbo yote haya ?
Maumbo hayo yamekuwepo kwa sababu yameumbwa na upepo. Je, upepo una zile sifa zote ulizozitaja?
Kaka inakuwaje unafikia hitimisho kabla hujatuthibitishia ukweli wa unacho dai ya kuwa upepo ndiyo umeumba haya maumbo ?
Ndio! Naendelea kuuonesha huo wepesi.
Mpaka muda huu hujaonyesha hilo, sababu kadiri unavyo elezea ndiyo unazidisha maswali ambayo hayana majibu.
Sizungumzii chanzo ama kisababishi cha upepo kuwepo..la hasha! Bali nazungumzia chanzo cha maumbo hayo mbalimbali ya ardhini kuwepo.
Hili haliepukiki, sababu huwezi kuelezea hili bila kujua upepo ni nini na umetokana na nini na kwa lipi uwe chanzo cha uwepo wa maumbile haya. Mathalani nikikuuliza wewe ni ipi kazi ya Milima katika mgongo wa ardhi bila shaka utaniambia, nitakuuliza swali je kwanini au kwa vipi kile ambacho ndiyo sababu kisiwe na malengo na ufahamu wa kufanya milima iwepo ? Kwako wewe hapa una dai ni UPEPO.
Je, maumbo mbalimbali ya kijiografia katika ardhi yetu hii yametoka wapi pasipo kuumbwa?
Mimi sikatai kama hayajaumbwa ila tunapingana juu ya nani ambaye ameyaumba haya maumbile. Wewe unasema ni upepo, na hapa nasubiri unipe ushahidi wa hilo.
Na si hapo tu bali maumbo hayo yamepewa mpaka na majina kuonesha utofauti wa umbo moja na jingine. Je, yameumbwa na kitu gani?
Suala la majina ni suala lingine ambalo kiuhalisia upepo wenyewe ndiyo ungetupa majina ya kile ilicho kiumba, lakini ajabu majina ya hayo maumbo yametolewa na mwanadamu.
 
Huwezi kulifanyia kazi jambo fulani bila kujua kuwa unafanya kitu gani. Kisayansi, nadharia ndio starting point katika kuyaelezea masuala mbalimbali yenye utata yanayohitaji ufumbuzi wa kisayansi, kanuni inayofuata hapo ni kuijaribu nadharia. Nadharia haiwezi kukubalika kama haitoweza kujaribiwa na haiwezi kujaribiwa kama hakuna uwezekano wa kuijaribu na kama hakuna uwezekano huo, basi hiyo nadharia si nadharia ya kisayansi.
Usahihi wa kuhoji upo katika majaribio na tafiti. Unahoji kwa facts zinazotokana na tafiti. Tafiti zinapotoa majibu ya kupingana na nadharia husika katika maswala mbalimbali na muhimu ndipo hapo nadharia hiyo inapokosa mashiko na kuwekwa pembeni.
 
Kila jambo la kisayansi ni mawazo ya watu. Hata hicho kifaa unachokitumia hivi sasa kuweza kuingia katika ukurasa huu wa mtandao ni mawazo ya mtu. Hakuna mtu aliyekuwa na ithibati juu ya uwepo wa kifaa hicho hapo kabla lakini wanasayansi walikwisha anza kuyafanyia kazi masuala mbalimbali kuhusiana na kifaa hicho zamani sana.

Nadharia yeyote ya kisayansi ni lazima ipitie katika majaribio, ndio maana ya scientific hypothesis. Fahamu hilo!
 
Hili la hii nadharia.
Kwanini unafikiri halina asili?
Unaweza kufanya utafiti kwa jambo ambalo halijawahi kuwepo ?

Hili la kwenye mada ni miongoni mwa mambo ambayo hayakuwahi kuwepo, vipi ufanye utafiti zaidi ya sanaa na ubunifu tu ili kuafikiana na mawazo ya mbunifu...!
Ni mambo gani hayajawahi kuwepo? Kwanini unasema hayajawahi kuwepo?

Fahamu kuwa, kuwepo ama kutokuwepo kwa nadharia ya namna hiyo hapo kabla haiizui nadharia hiyo kujaribiwa.
 
- Giant impact hypothesis is the best hypothesis so far that explains the moon formation, lakini haimaanishi kwamba ndio hypothesis ya kweli. These things are believed to have been formed about more than 4000 million years ago, hakuna anaeweza kuelezea with certainity.

- Umeelezea sana kuhusu tafiti na evidence ingekua vyema kama ungeviweka vitu hivyo pia. Au ungeweka links kubeba maelezo yako. Mfano umeelezea kuhusu ufanano wa composition lakini hujataja hizo composition.

The first 4 planets have almost the same composition and have an average specific gravity of 4 each. Je ufanano wa composition kati ya dunia na mwezi unatosha kuibeba hypothesis?

- Pia kuhusu Umri wa mwezi

Namna pekee ya kujua umri wa mwezi ni kufanya dating ya rock minerals katika sample zilizotoka mwezini ( na huo umri unapimwa tangu jiwe lilipo ganda in a sea of magma). Kama sijakosea sample za apollo zilionyesha umri kati ya (3000-4000)mys.
Je unaweza kunieleza ni namna gani tunaweza kutetea hypothesis kwa kutumia umri wa mwezi?

- Umeelezea kua dunia inakiini kikubwa tofauti na inavyotegemewa,

inavyotegemewa na nani? na katika criteria zipi? Na je core iliyotegemewa ina sifa zipi?
 
Sifa kuu ya muumbaji yeyote ni moja tu, nayo ni 'uwezo wa kuumba'. Basi!

Unasema maji yameleta athari kwenye jambo ambalo lipo tayari!! Jambo gani lipo tayari? Hilo bonde lilikuwepo hapo? Kwanini liitwe bonde?

Kuruhusu maji kufanya hivi ama vile ni jambo jingine. Mimi siko huko bali niko hapa; hilo bonde limetoka wapi? Nani kalileta hapo? Kwanini liitwe bonde?

Why "bonde"?
Kwa hili huwezi kuni "Challange" sababu udhaifu wako upi wazi na nimeuona mapema sana, kwa wewe kutokujua maana ya tamko "uumbaji" na ni yapi masharti au sifa za tamko hilo.
Sifa ya muumbaji nimekwisha kukutajia hapo. 'Uwezo wa kuumba'. Kukifanya kitu fulani ambacho hakikuwepo na kukiunda kikawepo katika muonekano fulani ndio huo uumbaji. Hayo maumbo ya kijiografia niliyoyasema hapo awali yenye majina tofauti tofauti kutokana na muonekano wake yameumbwa na kitu gani?
Wewe nithibitishie tu, ili tuone kwamba hili unalo liandika ni kweli au si kweli.

Upepo wenyewe umeumbwa au haujaumbwa na kipi kinafanya upepo uwepo na uwe sababu ya kuwepo kwa maumbo yote haya ?
Mimi sipo hapo kwenye sababu ya kuwepo kwa upepo.

Narudia:
Mimi sizungumzii kuhusu chanzo cha upepo wala chanzo cha kuwepo maji. Ninachokisema hapa ni sababu ya kuwepo kwa hayo maumbo mbalimbali ya kijiografia yenye majina tofauti tofauti na muonekano tofauti tofauti. Hayo maumbo yamekuwepo kutokana na kitu gani?
Kaka inakuwaje unafikia hitimisho kabla hujatuthibitishia ukweli wa unacho dai ya kuwa upepo ndiyo umeumba haya maumbo ?
Unahitaji uthibitisho upi kuhusiana na kuumbika kwa maumbo hayo?
Unafahamu uwepo wa maumbo ya kijiografia? Unafahamu maana ya 'umbo'?
Mimi sikatai kama hayajaumbwa ila tunapingana juu ya nani ambaye ameyaumba haya maumbile. Wewe unasema ni upepo, na hapa nasubiri unipe ushahidi wa hilo.
Ushahidi ni kupitia maumbo ya kijiografia ambayo yapo katika mazingira yetu hayahaya tunayoishi kila siku. Hayo maumbo yanatokea tu papo hapo, out of nowhere?
Suala la majina ni suala lingine ambalo kiuhalisia upepo wenyewe ndiyo ungetupa majina ya kile ilicho kiumba, lakini ajabu majina ya hayo maumbo yametolewa na mwanadamu.
Mtoa majina ya maumbo hayo si hoja bali hoja ni kile kilichosababisha kuwepo kwa maumbo hayo mbalimbali katika mazingira yetu.

Majina yanadhihirisha ule upekee na utofauti kati ya maumbo hayo. Maumbo hayo yenye majina tofauti tofauti yameumbikaje?
 
Sasa kaka, huelewi wapi, haya unayo yaandika unatakiwa uyatumie katika hili unalo tuambia,lakini ukweli ni kuwa halikubali.

Sasa unajuaje kitu fulani kwacho kimejengwa juu ya jambo lisilo na ithibati ? Embu tuonyeshe tuone.
 
Mawazo haya ni tofauti na hili la maumbile, unatakiwa kujua tofauti kati ya jambo lililo ndani ya uwezo wetu na jambo ambalo lipo nje ya uwezo wetu, suala la kutumia akili au kuleta wazo juu ya jambo ambalo umelikuta tayari ni kupotosha ukweli, lakini kuleta wazo jipya juu ya jambo ambalo halikuwahi kuwepo hili ni jambo kinawezekana, ndiyo maana tunataka uthibitisho wa hayo mawazo kabla ya kujadili hilo, maana sote tumekuta Dunia ipo na Mwezi upo, sasa unaposema habari za Bahari ya Magma, unatakiwa utupe uthibitisho.

Hilo nalifahamu, ila tunatofautiana katika kuhoji juu ya msingi, na hapa ndipo mnapo feli mnao fatilia Sayansi.
 
Kwanini unafikiri halina asili?
Halina asili sababu kinachoelezewa kinapingana na hali halisi, kwani Mwezi na Dunia vipo, ili ujue habari zake inabidi ufate elimu na siyo mawazo yako au nadharia, hapo ni kuchagua kukosea.
Ni mambo gani hayajawahi kuwepo? Kwanini unasema hayajawahi kuwepo?
Hapa kuna nukta mbili, jambo ambalo halikuwahi kuwepo na halijatanguliwa na kuwepo kwake, hili hakuna anae lijua, nukta ya pili ni jambo ambo halipo ba lilitanguliwa na kuwepo, hili ndiyo tunalijadili na lazima litanguliwe na ushahidi.

Halijawahi kuwepo sababu ni wazo la mtu, mtu ambaye alitakiwa kuthibitisha hilo ili tujue ukweli wa mawazo, yako ila kuruka hatua ni kujichagulia kukosea. Wewe umeikuta Dunia na umeukuta Mwezi kwa vipi useme mwezi uliwahi kuipiga Dunia kama ulivyo tuonyesha hapo juu ?

Au ngoja nikuulize swali rahisi sana, unayajuaje mambo ya kale ?
Fahamu kuwa, kuwepo ama kutokuwepo kwa nadharia ya namna hiyo hapo kabla
Naona huelewi unacho kijibu yaani ninacho kiandika, hapa naongelea nadharia yenyewe kwa maana ni ubunifu tu ambao mwanzo wake unatakiwa ithibati, yaani ushahidi. Ukiwa huelewi jambo bora uulize.
 
Sifa kuu ya muumbaji yeyote ni moja tu, nayo ni 'uwezo wa kuumba'. Basi!
Hapa nimecheka kidogo. Uwezo siyo sifa pekee ya muumbaji, kwanza kabisa unatakiwa ujue tamko hili ni maalumu, sababu hakuna anaye umba pasi na Mola muumba, hili unatakiwa ulijue, na ujue namna ya kutumia maneno vizuri. Hapa tamko muafaka tulitumie "kutengeneza au kuunda",sababu maji hayaumbi, binadamu haumbi na mfano wake. Sasa njoo kwenye hali halisi, ili uone ni kwa vipi "uwezo" si sifa pekee, leo hii uba simu, vipi iwepo simu bila msanifu, bila lengo la msanifu bila malighafi ? Sasa usiwe unakataa jambo ambalo huwesi kulithibitisha.
Unasema maji yameleta athari kwenye jambo ambalo lipo tayari!! Jambo gani lipo tayari? Hilo bonde lilikuwepo hapo? Kwanini liitwe bonde?
Bonde haliitwi bonde mpaka liwe limetangiliwa na uwepo wa ardhi. Nilikupa mfano mwepesi sana wa mtu na mchoro na mchora tattoo, ulitakiwa utafakari kwanza juu ya mfabo ule kabla ya kuja kuuliza jambo ambalo laiti ubgelitafakari usingepoteza muda kuliuliza sababu majibu yapo kule kule.

Tuendelee....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…