Wengi wanaochangia humu tayari wameshawahukumu hao masheikh kuwa ni magaidi, kwamba ni watu wabaya, watu hatari
Lakini mpaka sasa mwaka wa nane hakuna ushahidi wa Ugaidi wao, kesi yao inapigwa danadana.
Iko hivi, Endeleeni kuwaweka Jela, Kama walivyowekwa Jela watu wengine wa Mungu in the past!. Na wenye kuunga mkono dhulma hii endeeleeni kushangilia na kusapoti uonevu huu
Ukisoma comment wengine wanasapoti uonevu huu kwa sababu tu wanakomeshwa "Waislamu", kwao hiyo ni burudani kwao maana it seems kwa comment zao wana chuki kali sana vifuani mwao dhidi ya muslims (Wana Islamophobia) .
Ni kweli waliwekwa ndani na utawala wa rais Muislamu ndugu Kikwete, lakini mjue tu mwanasiasa ni mwanasiasa, wengine wako tayari kutenda dhulma bila hata kujali consciousness yao ya ndani, wao wanangalia power tu. Kikwete alikosea, aluwadhulumu hawa Masheikh bila haki, Dhulma hiyo ikaendelezwa na Magufuli dhidi ya hao watu, Na sasa mwezi mmoja mbele dhulma hiyo imeendelezwa na utawala wa Samia.
Ila kitu kimoja nawaambia hawa watawala wakumbuke Aya ya kwenye Qur'an
"Siiru fil ardh, fandhuruu kaifa kaana aakibatul'mujrimiin"
Maana yake "Tembeeni katika ardhi muone mwisho wa madhalimu"
Endeleeni tu kuonea watu wa Mungu tuje tuone Mwisho wenu!
Na nyie wenye kucomment kwa kebehi na dharau na chuki bila empathy wala utu kwa wenzenu kisa tu wao ni "waislamu wacha waumizwe" nanyi endeleeni kufurahia tu huu uonevu kisha tuone nanyi katika life cycle hii mtafika wapi