Mwezi wa Ramadhani umeingia Masheikh wako Jela

hao sahau kabisa.......sio leo au keshokutwa......tusiache kuwaombea ni wa-TZ wenzetu
May be ugumu ambao watawala wanaouona ni watawaachiaje bila kuwakuta na hatia? , yaani serikali itaonekanajeonekanaje mbele ya umma, kwa hiyo naamini behind the scene wanawalazimisha waconfess baadhi ya makosa ambayo hayapo ili serikali isave face kisha ndo ijifanye imewasamehe
 
nnachokwambia wale hawatakuwa huru kamwe........tukiwa kwenye majukwaa tunawatukana hao tunaowaita ni mabeberu....nyuma ya pazia wao ndio wanaoamrisha wahifadhiwe huko....hakuna rais atakaebatilisha....tusiache kuwaombea....sala zetu zitawapa heri mno....
 
Sio masheikh wa kuombewa kuna watanzania wengi walio jela wanahitaji kuombewa msamaha kusema masheikh tu huo ni ubaguzi!

Hao sio muhimu kama masheikh sawa mkuu. Kuna wezi, majambazi n.k huko gerezani acha wapate fundisho kidogo. masheikh ndio kipaumbele maana hawana hatia.


Babu sea kwa kesi ya ubakaji kama nikweli ama alizushiwa, na alisamehewa na kuachwa huru, na ndio kesi ya ubakaji iyo!!!! Je! Masheikh wanakosa gani!!! Acheni chuki bwana
 


Chief, how old are you?!
 
Hoja yako ingenoga kama ungewasemea wote walio magerezani kwa kubambikiziwa kesi.

Hii kuwatetea mashehe peke yake imekaa kibaguzi sana.

Hebu karekebishe hapo ili nikugongee LIKE.

Kazi iendelee, tusizinguane.

Wakina nani hao waliobambikiwa, ebu wataje na uwaombee wewe kama wewe. Sisi tunadili na masheikh wetu wasio na hatia hawa ndio muhimu zaidi, na kesi yao haijasikilizwa hadi waleo
 

If you still think that the government “Need to save face ” for any operation they do, then You still need to grow up and face reality!!!

...
 
Mnao waoneaga huruma hawa magaidi hivi hamfuatilii kinachoendelea Msumbiji jinsi majitu type hii yanavyo chinja wenzao. Kuweni serious bhana

Kuwa na hekma na busara wewe.. ukiombwa ushahidi kama wao ni magaidi utaleta!!! Hao wa msumbiji wana uhusiano gani na hawa masheikh!!!! Au hujui nini maana neno Masheikh uelekezwe!!! Viumbe kama ninyi mngelikuwepo kipindi cha ottoman empire/Ertugrul mngefyekelewa mbali kwa uropokaji na kubambikia watu kesi.
 
Kama Samia & Hussein Mwinyi wanataka vipindi vyao vya uongozi viwe vigumu zaidi basi wajihusishe na issue za mashehe (including wa uamsho)

Tulia mzee mama samia afanye yake, wanaotaka masheikh watolewe ni wengi kuliko mnaopinga ambao hata nusu yenu hamfiki.
 
Tatizo watu wanawafanya masheikh ni agenda zao za kisiasa tumeona kipindi cha uchaguzi kila mmoja aliitumia masheikh kutaka kuingilia!
 
Kesi ya babu seya na wenzie usiichukulie kama reference yako mkuu, kesi yao ilikuwa ni ya kupika, kuna namna flan ilikuwa inatafutwa.
 
Kesi ya babu seya na wenzie usiichukulie kama reference yako mkuu, kesi yao ilikuwa ni ya kupika, kuna namna flan ilikuwa inatafutwa.

Na kesi ya hawa mashehe ni yakubambikiwa, haina ukweri wowote. Viongozi waliopita walikua na lengo gani kwa awa ndugu zetu! Kikwete na uislamu wake kalikalia kimya swala hili huku akijua masheikh hawa hawana wa kuwasikiliza, na wakiendelea kuteseka, huku yeye akila bata na familia yake, lakini atambue kuwa atakuja kuulizwa na Mola wake.


Tunamuomba mama huyu awatoe wakafunge ramadan na familia zao nao wafurahie kama familia zingine.
 
Hoja yako ingenoga kama ungewasemea wote walio magerezani kwa kubambikiziwa kesi.

Hii kuwatetea mashehe peke yake imekaa kibaguzi sana.

Hebu karekebishe hapo ili nikugongee LIKE.

Kazi iendelee, tusizinguane.
👊👊
 
Kwahiyo Abubakari hana ushawishi kwa serikali kwa nafasi aliyonayo?
Ushawishi wa mambo mengine sio kumuweka mtu ndani; au labda niseme hivi; hivi enzi za JPM masheikh hao kina ZUberi, Abubakari nk si walikua vipenzi wa JPM? Wao wanafurahia kuwaona wale masheikh wa uamsho kua ndani miaka yote hiyo bila kuwaombea msamaha? Anyway labda na wao wanaunga mkono wale masheikh wa uamsho kua ndani
 
Siwezi amini haya,,,Kikwete Sheni sijui kama walijua walifanyalo,,maana watu hatari kuna namna ya kuwadhibiti,,,Ila mie Ombi langu kwa Mh Mama SAMIA SULUHU,,,namuomba sana,,,hao watu wamewekwa ndani kipropoganda tu,,riport yao imeandikwa ki-propoganda.Awaonee huruma ALLAH atamjazia kheri nyingi sana,,ukizingatia huu ni mwezi wa ramadhani.
 
Hizo Dua za Watu waliodhulumiwa Uhuru wao na kufungiwa nyuma ya Kuta ndefu na Nondo ndio zinazoliangamiza hili Taifa mpaka Misiba ya Rais tunaiona zamani kulikuwa hamna kitu kama hii
 
Poleni sana, sema najiulizaga inawezekanaje marais wawili wamepita na bado wako jela kama hawana hatia? kuna kitu hatukijui na inawezekana hao jamaa walikua na agenda mbaya sana kwa nchi yetu.. sitaki kuamini kwamba wanaonewa, anyway mola awape faraja kama kweli hawana hatia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…