Mwigulu: Aliyetaka kuwashusha matajiri waishi kama masikini alikuwa na ''Sadist mind''

Mwigulu: Aliyetaka kuwashusha matajiri waishi kama masikini alikuwa na ''Sadist mind''

Johnny Sack

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2017
Posts
8,984
Reaction score
19,288
WAZIRI wa Fedha na Mipango Dk Mwigulu Nchemba amesema serikali haikusudii kuwashusha matajiri ili walingane na masikini kwa kuwa hiyo ni "sadist mind"

na kwamba itaendelea kutekeleza miradi ya kimkakati ili kuhakikisha kila mmoja anapanda.

Akihitimisha mjadala wa Bajeti, Dk Mwigulu amesema nia ya serikali ni kuhakikisha kila mmoja kila taasisi inapata mgao wa keki ya taifa hata hivyo uhitaji ni mkubwa na mpango wa sasa ni kuanza na wachache.
 
Hilo angelisema kipindi kile cha mwendazake ili aone moto wake
Kuna kitu kichwani kinanimbia kuwa Tanzania inakaribia kuona mabadiliko makubwa ya kiuongozi na mfumo ambayo yatakuja bila kutegemea. Viongozi wengi walioko madarakani sasa hivi wameshafikia saturation point ya kufikiri na ni suala la muda tu chochote kinaweza kikatokea.
 
Kweli kabisa muda utajibu!!
 
Ngoja waje waliozimia

Katika_Historia%3A%0APamoja_na_kwamba_ALIZIMIA_baada_ya_kuuona_mwili_wa_mpendwa_wetu_MFUKO_hak...jpg
 
Kuna kitu kichwani kinanimbia kuwa Tanzania inakaribia kuona mabadiliko makubwa ya kiuongozi na mfumo ambayo yatakuja bila kutegemea. Viongozi wengi walioko madarakani sasa hivi wameshafikia saturation point ya kufikiri na ni suala la muda tu chochote kinaweza kikatokea.

Mkuu unaona ninachokiona. Kile kisichotarajiwa kitakwenda kutokea katika hali ya ajabu. Katika dunia hii kuna kitu kufikia ukomo. Ccm kwa sasa ilipofikia imefikia mwisho wa uwepo wake maana wakati ni ukuta.
 
Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
 
Unapoambiwa usiwaamini wanasiasa na hii ndio maan yake!!! While scarf is in the neck all day 😂🤣🤣🤣🤣
 
Kuna kitu kichwani kinanimbia kuwa Tanzania inakaribia kuona mabadiliko makubwa ya kiuongozi na mfumo ambayo yatakuja bila kutegemea. Viongozi wengi walioko madarakani sasa hivi wameshafikia saturation point ya kufikiri na ni suala la muda tu chochote kinaweza kikatokea.
Huo wakati ufike mapema tu.
 
Unafiq tu. Hilo angelisema kipindi kile cha mwendazake ili aone moto wake
Kwann aone wakati katoa maoni yake. Hicho unachokupigia debe ndicho tunakiita "sadist mind". Jiwe alikuwa nacho sana. Mpuuzi yule. Bora kafa
 
Back
Top Bottom