Mwigulu amejipa umasihi wa kuponya mioyo na sasa nchi nzima wanaimba jina lake. Mungu amtangulie afike mbali

Mwigulu amejipa umasihi wa kuponya mioyo na sasa nchi nzima wanaimba jina lake. Mungu amtangulie afike mbali

Katika kipindi hiki ambacho watanzania wanahitaji majibu ya matatizo yao hasa dhuluma, unyanyasaji, unyang'anyi wa mfumo ,maonevu ya kijamii hasa ndugu Mungu amemuinua Mwigulu kuja kuwapa majibu ya haraka na yauhakika wa haki zao papo kwa hapo hapa Mungu anamtumia Mwigulu kuwa masihi wa taifa.

Nimefatilia ziara zake nchi nzima watu wanasafiri wanakesha kumsubiri Mwigulu afike katika wilaya zao ili wapeleke malalamiko yao ambayo hayakuwa na majibu kwa miaka mingi .

Nimefatilia kila sehemu anazopita anaacha faraja, furaha, matumaini, na machozi ya furaha kwa waathiriwa, Mungu ameweka

Katika kipindi ambacho Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan anataka kuacha legacies naona Mwigulu akiwa katika kiwango cha ķuhakikisha alama za serikali ya awamu ya sita zinapatikana kama utawala uliojali hali za watu za kijamii na kuondoa dhuluma moja kwa moja .

Hii inaonekana hata chadema wakianza siasa mikutano yao haitakuwa na mvuto kama hii yenye majibu ya moja kwa moja kwa wananchi.

Mungu aendelee kumuweka Mh Mwigulu aendelee na hizi ziara zake kila anapopata muda ili kurudisha imani ya wananchi kwa serikali yao .

USSR
Hizo ni kampeni. Alitakiwa awashurutishe viongozi ngazi zote serikalini watatue kero na kuwasikiliza wananchi, sio kuzunguja pekee kuuza sura
 
Hizo ni kampeni. Alitakiwa awashurutishe viongozi ngazi zote serikalini watatue kero na kuwasikiliza wananchi, sio kuzunguja pekee kuuza sura
Kwa hiyo ulitaka akae ofisini bila kwenda waliko Wananchi ili awasikilize na kujionea hali halisi? Sasa asipo watembelea Wananchi na kupita kukagua shughuli mbalimbali za maendeleo na miradi inayotekelezwa na serikali atajuaje changamoto zake? Unataka kila kitu afanyie mezani ?

Mheshimiwa Waziri Mkuu Wetu ni mtu wa kazi tu na ambaye anapenda kujionea uhalisia nje ya makaratasi anayopelekewa mezani. Ndio maana anaendelea kuungwa mkono na kupendwa na wananchi kwa Sababu anakutana na wananchi na kupokea kero zao pamoja na kutoa majawabu papo kwa papo
 
Back
Top Bottom