Mwigulu: Elimu ya msingi ya lazima kuwa miaka 10

Anacho Manisha hapa Mr' Guy ni kile kilicho katka mtaala mpya (wa kipumbavu).

Elimu ya Msingi darasa la 1-6 then secondary education form 1-4.

Total inakua miaka 10, walicho fanya ni kuunganisha maana yake Elimu ya secondary imeondolewa badala yake imerudishwa Kuwa msingi
 
Mwalimu Nyerere, hatakuwa na lakufanya muhitimu wa la 'kumi' zaidi ya kumwonea wivu kwa kubukua sana .
Hahahahaaa.. Hii kali, natamani na sisi kipindi chetu wangeweka darasa la kumi, ukianza shule unamiaka tisa, ujue unamaliza chuo una miaka 31, ajira zinataka watu kuanzia miaka 18 mpaka 28. Unamaliza shule unarudi kwenu kuchunga mbuzi.
 
Hahahahaaa.. Hii kali, natamani na sisi kipindi chetu wangeweka darasa la kumi, ukianza shule unamiaka tisa, ujue unamaliza chuo una miaka 31, ajira zinataka watu kuanzia miaka 18 mpaka 28. Unamaliza shule unarudi kwenu kuchunga mbuzi.
Enzi zetu unaanza la kwanza ukiwa na miaka 12, miaka hii mtoto anamaliza la saba akiwa na miaka 13 😂.

Ndo maana wameamua mtoto asome hadi darasa la kumi Ili wabalance mambo.
 
Enzi zetu unaanza la kwanza ukiwa na miaka 12, miaka hii mtoto anamaliza la saba akiwa na miaka 13 .

Ndo maana wameamua mtoto asome hadi darasa la kumi Ili wabalance mambo.
Hahahahaaaa.. Waongeze na secondary watuletee form 9, unakuta kijana yupo mwaka watatu chuo na anamjukuu wa miezi mitano.
 
Hivi ule mpango wa shule ya msingi kuishia darasa la sita uliishia wapi? .
Umeanza mwaka huu, wanafunzi ambao wako lasaba na lasita mwaka huu wanafanya mtihani pamoja. sasa sijui mwakani wanaendaje sekondari, na watasoma shule gani sijui

Na hao watakaofika lakumi sijui watasomea madarasa ya wapi kwa hiyo miaka minne ya juu iloongezeka.

Na shule za sekondari zitakua nakazi gani kwenye hiyo miaka minne wanayosubiri intake ya form one wa kwanza kutoka darasa la kumi.

Hivi unajua hivi vitu ukienda kumwambia mtu ambae hafuatilii mitandao na vyombo vya habari atasema unamuongopea. Maana najiona kama naandika pumba saana hadi naona aibu. Lakini ndo waheshimiwa wameamua hivi. INAFIKIRISHA sana
 
Kimsingi wamepunguza mwaka mmoja wa darasa la 7.
Sasa watasoma elimu ya msingi hadi darasa la 6.
Kisha elimu ya sekondari hadi kidato cha 4 na kufanya jumla ya hiyo miaka 10 ya elimu ya lazima.
Tofautisha elimu ya msingi na elimu ya lazima.
Nimekupata mkuu. Tuliosoma zamani tukisikia elimu ya msingi tunajua ni ile ya la 1-7 ambayo ni lazima. Nimekuelewa.
 
Mkuu wanamaanisha kuanzia la kwanza mpaka form 4 itakua lazima....

Kwani ni jambo baya? Mtoto wa atleast amalize shule na miaka 16....
 
Tatizo la elimu ya Tz ni content na quality sio miaka ya kukaa kwenye majengo mabovu yale, common sense is not common to kengez, vijana wamesoma miaka mingi na kugraduate chuo kikuu lakini hawajui hata kuandika barua yake ya kujiombea kazi mwenyewe ndio ataweza mavitu makubwa kama multimillion/billion project writing au designs?

Hata iwe miaka 20 kwa quality hii ya elimu na waalimu wenyewe tutabaki parepare
 
Mfumo wa elimu bongo unazid kandamizwa! Dunia imebadilika elimu ya msingi inapunguzwa muda wake ili kuendana na tec ila bongo inazid kurudishwa nyuma mpaka dunia ya nne!!
 
Mkuu,

Umeongea fact ila hujaeleza chanzo halisi cha hilo tatizo huwezi kusema kijana hawezi kuandika barua ya kuombea kazi ikiwa amepata elimu ya communication skills hii inakua imekaaje kwa mfano?
 
Nilidhani hivi pia ila baadae nikaelewa kuwa ni elimu ya msingi na sekondari hadi kidato cha 4 kuwa ndo imekuwa elimu ya msingi.
Kwahiyo utaratibu ni ule ule miaka 6 msingi, miaka 4 o level. A level pia iko pale pale au imefutwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…