Mwigulu: Elimu ya msingi ya lazima kuwa miaka 10

Mwigulu: Elimu ya msingi ya lazima kuwa miaka 10

Anacho Manisha hapa Mr' Guy ni kile kilicho katka mtaala mpya (wa kipumbavu).

Elimu ya Msingi darasa la 1-6 then secondary education form 1-4.

Total inakua miaka 10, walicho fanya ni kuunganisha maana yake Elimu ya secondary imeondolewa badala yake imerudishwa Kuwa msingi
Itakuwa kwa lugha gani? Kiingereza mwanzo mwisho au kiswahili mwanzo mwisho?
 
Kwahiyo utaratibu ni ule ule miaka 6 msingi, miaka 4 o level. A level pia iko pale pale au imefutwa?
Ile nayo wangeifuta ingependeza, mtu akimaliza form 4 aingie chuo kuisaka degree direct. Miaka 13 kwa hizi degree za kawaida inatosha kabisa baada ya hapo kijana akajitafute mapema kama ni ajira au kujiajiri.
 
Ipo hivi, mabadiliko ya mtaala mpya wa elimu unaelekeza kuwa elimu ya msingi iishie darasa la sita na hakutakuwepo na mtihani wa mchujo bali wa upimaji na watoto wataendelea na elimu ya amali kwa maana sekondari kwa miaka minne na watakuwa na mitihani ya mchujo.
Kwa maana nyingine mitihani ya darasa la nne, la saba na form two kitaifa haitokuwepo bali mitihani hiyo imegeuzwa kuwa ya upimaji kama ile ya mock japo itaandaliwa na baraza la mitihani. Hakutakuwepo na mtoto kufeli madarasa hayo bali ule wa form four ndio utakuwa wa mchujo wa kuwapata watakaokwenda vyuoni na kidato cha tano.
Ndio maana mfumo huu ukaitwa elimu ya lazima kwa kila mtoto kama ilivyo kule kisimkazi!
 
Itaitwa elimu ya lazima ambayo inajumuisha elimu ya msingi miaka 6 na elimu ya amali miaka minne.

elimu ya lazima ndiyo elimu gani hiyo? elimu ya msingi ni elimu ya lazima kwa kila mtoto na hii ni dunia nzima hakuna nchi ambayo mtoto anamaliza elimu ya msingi akiwa na miaka 16, isitoshe huo mfano mmeutolea wapi dunia hii ndiyo kazi ya wanu hiyo kama waziri wa elimu? ni nchi gani ambayo umewahi kuskia imefuta elimu ya msingi ukiondoa taliban wa afghanistan? ...
 
elimu ya lazima ndiyo elimu gani hiyo? elimu ya msingi ni elimu ya lazima kwa kila mtoto, isitoshe huo mfano mmeurelea wapi dunia hii, ni nchi gani ambayo umewahi kuskia imefuta elimu ya msingi ukiondoa taliban wa afghanistan? ...
Ni elimu imayojumuisha elimu ya msingi na elimu ya amali. Elimu ya msingi kwa maana primary education ipo na imepunguziwa muda bali ile ya amali ambayo huku bara inajulikana kama elimu ya sekondari imebaki na muda wake.
Elimu ya msingi ipo haijafutwa.
 
Ni elimu imayojumuisha elimu ya msingi na elimu ya amali. Elimu ya msingi kwa maana primary education ipo na imepunguziwa muda bali ile ya amali ambayo huku bara inajulikana kama elimu ya sekondari imebaki na muda wake.
Elimu ya msingi ipo haijafutwa.

hapo sasa nimeelewa ...
 
Hawa jamaa ni wa ajabu sana, kuna sababu kwa nini inaitwa "elimu ya msingi", siajabu hawaelewi hata ni kwa nini inaitwa hivyo vinginevyo wasingekuja na ujiga kama huu, halafu inakuwa miaka 10? i mean, mtoto atamaliza elimu ya msingi akiwa na miaka mingapi?

hata kenya wenyewe wanapunguza miaka ya elimu ya msingi ktk 8 ya sasa hivi mpaka 6 kuna sababu, elimu ya msingi haiwezi kuwa miaka mingi namna hiyo unless labda watoto wana matatizo ya akili na wanahitaji special education.

hivyo elimu ya msingi ilipaswa kupunguzwa na siyo kuongezwa au badilisheni jina na msiite msingi ...
Ni kwaamba elimu ya mfumo wa zamani imebadilishwa watoto wataishia darasa la sita badala ya darasa la saba halafu watafanya mitihani ya kuingia sekondari ambapo ni lazima kila mtoto asome mpaka kidato cha nne.

Maana rahisi ni kwamba wameungisha elimu ya msingi na sekondari kuwa kitu kimoja.
 
Hapo mimi sijaelewa. Mpaka sasa ule muongozo ukiotolewa mwaka jana wa elimu ya msingi kuishia darasa la sita hawa waliopo darasa la 5 sasa,tayari hao wa la 5 tayari wameshaanza kucaver masomo mengine ili waishie la 6.

Lakini wakati naendelea kuandika huko juu nimeongea na mwalimu mmoja kubadirishana mawazo. Amemuambia hivi. *WAMEFANYA ELIMU YA MSINGI KUANZIA LA KWANZA MPAKA LA SITA HAPO UNAFANYA TU MTIHANI WA KUJIPIMA SIO UFAURU,THEN LA 7 NI SAWA NA FORM ONE,LA 8 FORM TWO,LA 9 FORM THREE NA LA 10 FORM FOUR.

HIYO YOTE NI KUANDAA WAJINGA WENGI KSBB WATOTO WAO HAWASOMI HIZI SHULE. HAWAFUATA HUU MTAALA MBOVU. HII KUNA HAJA KUBWA YA KUJIKOMBOA SISI WENYEWE. TUKINDELEA.KUWATEGEMEA HAWA TUMEKWISHA
 
Elimu ya msingi ipo kwa wote na ni ya lazima kwa wote.
Elimu ya sekondari ipo na sasa nayo imekuwa ya lazima kwa wote.
Tatizo lako hapo nini?
Haijafutwa elimu ya msingi bali imepunguzwa mwaka mmoja wa darasa la 7.
Kinachokutatiza lugha tu waliyo tumia.
elimu ya lazima ndiyo elimu gani hiyo? elimu ya msingi ni elimu ya lazima kwa kila mtoto na hii ni dunia nzima hakuna nchi ambayo mtoto anamaliza elimu ya msingi akiwa na miaka 16, isitoshe huo mfano mmeutolea wapi dunia hii ndiyo kazi ya wanu hiyo kama waziri wa elimu? ni nchi gani ambayo umewahi kuskia imefuta elimu ya msingi ukiondoa taliban wa afghanistan? ...
 
Kuna binti mmoja wa miaka 16 Canada, anarusha ndege angani. Huku kwetu wa miaka hiyo anafanya nini?
 
Umeanza mwaka huu, wanafunzi ambao wako lasaba na lasita mwaka huu wanafanya mtihani pamoja. sasa sijui mwakani wanaendaje sekondari, na watasoma shule gani sijui

Na hao watakaofika lakumi sijui watasomea madarasa ya wapi kwa hiyo miaka minne ya juu iloongezeka.

Na shule za sekondari zitakua nakazi gani kwenye hiyo miaka minne wanayosubiri intake ya form one wa kwanza kutoka darasa la kumi.

Hivi unajua hivi vitu ukienda kumwambia mtu ambae hafuatilii mitandao na vyombo vya habari atasema unamuongopea. Maana najiona kama naandika pumba saana hadi naona aibu. Lakini ndo waheshimiwa wameamua hivi. INAFIKIRISHA sana
Halafu viongozi bado hawajatoa ufafanuzi vizuri hadi sasa, hii inamaanisha wamekurupuka.
 
SERIKALI YATANGAZA ELIMU YA MSINGI YA LAZIMA KUWA MIAKA 10

Dodoma — Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba ametangaza kuanza kwa utekelezaji wa mfumo mpya wa elimu utakaofanya elimu ya msingi kuwa ya lazima kwa kipindi cha miaka kumi, akisema ni sehemu ya mageuzi makubwa yaliyofanywa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Akihitimisha hotuba yake ya bajeti bungeni, Dkt. Nchemba amesema mageuzi hayo ni ya kihistoria kwani mara ya mwisho mabadiliko makubwa ya mfumo wa elimu yalifanyika mwaka 1967, wakati elimu ya lazima ilipopanuliwa kutoka darasa la nne hadi la saba.

Amesema mabadiliko hayo hayaishii kuongeza muda wa masomo pekee, bali yanaambatana na maboresho ya kina yaliyokuwa yakihitajika kwa muda mrefu, ikiwemo kuboreshwa kwa mitaala na miundombinu ya elimu.

“Mheshimiwa Rais ameonyesha ujasiri mkubwa wa kufanya maamuzi haya bila kujali gharama ili kuhakikisha watoto wa Kitanzania wanapata elimu bora,” amesema Dkt. Nchemba.

Ameeleza kuwa maandalizi ya utekelezaji wa mpango huo yamefanyika kwa kiwango kikubwa, huku hatua zilizobaki zikiendelea kukamilishwa ili kuhakikisha utekelezaji wake unakuwa wa mafanikio.

Katika kuimarisha elimu ya ufundi, amesema serikali imeongeza kwa kiasi kikubwa idadi ya shule kutoka takribani tano zilizokuwepo awali hadi zaidi ya 300, zikiwemo shule za awali na za ufundi, ambapo nyingi zina mwelekeo wa masomo ya kihandisi.

Aidha, amesema ujenzi wa madarasa 79,000 umeondoa changamoto ya mfumo wa “second selection” uliokuwa ukiwanyima baadhi ya wanafunzi fursa ya kuendelea na masomo.

Amesisitiza kuwa upanuzi huo wa miundombinu utahakikisha kila mtoto anapata nafasi ya elimu na kuweka msingi wa kuzalisha wataalamu na viongozi wa baadaye.

“Mageuzi haya yataingia katika historia ya nchi yetu na yatakumbukwa kuwa yamefanyika chini ya uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan,” amesema.

KWA WAZAZI WOTE, KABLA HUJACHAGUA SHULE YA KUSOMA MWANAO, KAMA UTACHAGUA ASOME PRIVATE SCHOOL, MZAZI UJIANDAE KUMLIPIA ADA KWA MIAKA 10 YA ELIMU HIYO YA MSINGI
 
Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba akihitimisha bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu amesema kuwa elimu ya msingi sasa kuwa miaka 10

---
Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba ametangaza kuanza kwa utekelezaji wa mfumo mpya wa elimu utakaofanya elimu ya msingi kuwa ya lazima kwa kipindi cha miaka kumi, akisema ni sehemu ya mageuzi makubwa yaliyofanywa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Akihitimisha hotuba yake ya bajeti bungeni, Dkt.

Nchemba amesema mageuzi hayo ni ya kihistoria kwani mara ya mwisho mabadiliko makubwa ya mfumo wa elimu yalifanyika mwaka 1967, wakati elimu ya lazima ilipopanuliwa kutoka darasa la nne hadi la saba.

Amesema mabadiliko hayo hayaishii kuongeza muda wa masomo pekee, bali yanaambatana na maboresho ya kina yaliyokuwa yakihitajika kwa muda mrefu, ikiwemo kuboreshwa kwa mitaala na miundombinu ya elimu.

"Mheshimiwa Rais ameonyesha ujasiri mkubwa wa kufanya maamuzi haya bila kujali gharama ili kuhakikisha watoto wa Kitanzania wanapata elimu bora," amesema Dkt. Nchemba.

Ameeleza kuwa maandalizi ya utekelezaji wa mpango huo yamefanyika kwa kiwango kikubwa, huku hatua zilizobaki zikiendelea kukamilishwa ili kuhakikisha utekelezaji wake unakuwa wa mafanikio.

Katika kuimarisha elimu ya ufundi, amesema serikali imeongeza kwa kiasi kikubwa idadi ya shule kutoka takribani tano zilizokuwepo awali hadi zaidi ya 300, zikiwemo shule za awali na za ufundi, ambapo nyingi zina mwelekeo wa masomo ya kihandisi.

Aidha, amesema ujenzi wa madarasa 79,000 umeondoa changamoto ya mfumo wa "second selection" uliokuwa ukiwanyima baadhi ya wanafunzi fursa ya kuendelea na masomo.
Watoto wake watasoma elimu hiyo?
 
Back
Top Bottom