Mishi Zawa
JF-Expert Member
- May 6, 2015
- 1,673
- 2,575
Itakuwa kwa lugha gani? Kiingereza mwanzo mwisho au kiswahili mwanzo mwisho?Anacho Manisha hapa Mr' Guy ni kile kilicho katka mtaala mpya (wa kipumbavu).
Elimu ya Msingi darasa la 1-6 then secondary education form 1-4.
Total inakua miaka 10, walicho fanya ni kuunganisha maana yake Elimu ya secondary imeondolewa badala yake imerudishwa Kuwa msingi
Ile nayo wangeifuta ingependeza, mtu akimaliza form 4 aingie chuo kuisaka degree direct. Miaka 13 kwa hizi degree za kawaida inatosha kabisa baada ya hapo kijana akajitafute mapema kama ni ajira au kujiajiri.Kwahiyo utaratibu ni ule ule miaka 6 msingi, miaka 4 o level. A level pia iko pale pale au imefutwa?
Mkuu wanamaanisha kuanzia la kwanza mpaka form 4 itakua lazima....
Kwani ni jambo baya? Mtoto wa atleast amalize shule na miaka 16....
Mtu atakayeishia drs la 4 na atakayeishia kidato cha tatu wote wawili watahesabika hawana elimu ya msingi.Darasa la kwanza hadi kidato Cha nne ni elimu ya msingi sasa hivi, sawa sio mbaya.
Itaitwa elimu ya lazima ambayo inajumuisha elimu ya msingi miaka 6 na elimu ya amali miaka minne.halafu hiyo shule itaitwaje? bado ya "shule ya msingi" tu mpaka miaka 16?
Itaitwa elimu ya lazima ambayo inajumuisha elimu ya msingi miaka 6 na elimu ya amali miaka minne.
Ni elimu imayojumuisha elimu ya msingi na elimu ya amali. Elimu ya msingi kwa maana primary education ipo na imepunguziwa muda bali ile ya amali ambayo huku bara inajulikana kama elimu ya sekondari imebaki na muda wake.elimu ya lazima ndiyo elimu gani hiyo? elimu ya msingi ni elimu ya lazima kwa kila mtoto, isitoshe huo mfano mmeurelea wapi dunia hii, ni nchi gani ambayo umewahi kuskia imefuta elimu ya msingi ukiondoa taliban wa afghanistan? ...
Ni elimu imayojumuisha elimu ya msingi na elimu ya amali. Elimu ya msingi kwa maana primary education ipo na imepunguziwa muda bali ile ya amali ambayo huku bara inajulikana kama elimu ya sekondari imebaki na muda wake.
Elimu ya msingi ipo haijafutwa.
Ni kwaamba elimu ya mfumo wa zamani imebadilishwa watoto wataishia darasa la sita badala ya darasa la saba halafu watafanya mitihani ya kuingia sekondari ambapo ni lazima kila mtoto asome mpaka kidato cha nne.Hawa jamaa ni wa ajabu sana, kuna sababu kwa nini inaitwa "elimu ya msingi", siajabu hawaelewi hata ni kwa nini inaitwa hivyo vinginevyo wasingekuja na ujiga kama huu, halafu inakuwa miaka 10? i mean, mtoto atamaliza elimu ya msingi akiwa na miaka mingapi?
hata kenya wenyewe wanapunguza miaka ya elimu ya msingi ktk 8 ya sasa hivi mpaka 6 kuna sababu, elimu ya msingi haiwezi kuwa miaka mingi namna hiyo unless labda watoto wana matatizo ya akili na wanahitaji special education.
hivyo elimu ya msingi ilipaswa kupunguzwa na siyo kuongezwa au badilisheni jina na msiite msingi ...
elimu ya lazima ndiyo elimu gani hiyo? elimu ya msingi ni elimu ya lazima kwa kila mtoto na hii ni dunia nzima hakuna nchi ambayo mtoto anamaliza elimu ya msingi akiwa na miaka 16, isitoshe huo mfano mmeutolea wapi dunia hii ndiyo kazi ya wanu hiyo kama waziri wa elimu? ni nchi gani ambayo umewahi kuskia imefuta elimu ya msingi ukiondoa taliban wa afghanistan? ...
Wanakomoa WATANZANIA, wabunge wetu nao vilaza sijui huwa wanadiscuss nini bungeni.Ajira kikomo kuomba ni miaka 45 hao manyang'au wanaopick mwisho 25 mpaka 28 wanaamua kuwakomoa vijana tu hakuna kingine
Warudishwe shule wakasome miaka 10 hakuna namnaWanakomoa WATANZANIA, wabunge wetu nao vilaza sijui huwa wanadiscuss nini bungeni.
Hili nalo wakalitizame
Halafu viongozi bado hawajatoa ufafanuzi vizuri hadi sasa, hii inamaanisha wamekurupuka.Umeanza mwaka huu, wanafunzi ambao wako lasaba na lasita mwaka huu wanafanya mtihani pamoja. sasa sijui mwakani wanaendaje sekondari, na watasoma shule gani sijui
Na hao watakaofika lakumi sijui watasomea madarasa ya wapi kwa hiyo miaka minne ya juu iloongezeka.
Na shule za sekondari zitakua nakazi gani kwenye hiyo miaka minne wanayosubiri intake ya form one wa kwanza kutoka darasa la kumi.
Hivi unajua hivi vitu ukienda kumwambia mtu ambae hafuatilii mitandao na vyombo vya habari atasema unamuongopea. Maana najiona kama naandika pumba saana hadi naona aibu. Lakini ndo waheshimiwa wameamua hivi. INAFIKIRISHA sana
Watoto wake watasoma elimu hiyo?Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba akihitimisha bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu amesema kuwa elimu ya msingi sasa kuwa miaka 10
---
Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba ametangaza kuanza kwa utekelezaji wa mfumo mpya wa elimu utakaofanya elimu ya msingi kuwa ya lazima kwa kipindi cha miaka kumi, akisema ni sehemu ya mageuzi makubwa yaliyofanywa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Akihitimisha hotuba yake ya bajeti bungeni, Dkt.
Nchemba amesema mageuzi hayo ni ya kihistoria kwani mara ya mwisho mabadiliko makubwa ya mfumo wa elimu yalifanyika mwaka 1967, wakati elimu ya lazima ilipopanuliwa kutoka darasa la nne hadi la saba.
Amesema mabadiliko hayo hayaishii kuongeza muda wa masomo pekee, bali yanaambatana na maboresho ya kina yaliyokuwa yakihitajika kwa muda mrefu, ikiwemo kuboreshwa kwa mitaala na miundombinu ya elimu.
"Mheshimiwa Rais ameonyesha ujasiri mkubwa wa kufanya maamuzi haya bila kujali gharama ili kuhakikisha watoto wa Kitanzania wanapata elimu bora," amesema Dkt. Nchemba.
Ameeleza kuwa maandalizi ya utekelezaji wa mpango huo yamefanyika kwa kiwango kikubwa, huku hatua zilizobaki zikiendelea kukamilishwa ili kuhakikisha utekelezaji wake unakuwa wa mafanikio.
Katika kuimarisha elimu ya ufundi, amesema serikali imeongeza kwa kiasi kikubwa idadi ya shule kutoka takribani tano zilizokuwepo awali hadi zaidi ya 300, zikiwemo shule za awali na za ufundi, ambapo nyingi zina mwelekeo wa masomo ya kihandisi.
Aidha, amesema ujenzi wa madarasa 79,000 umeondoa changamoto ya mfumo wa "second selection" uliokuwa ukiwanyima baadhi ya wanafunzi fursa ya kuendelea na masomo.
Kimsingi wapo wanaotaka aoleweKuna binti mmoja wa miaka 16 Canada, anarusha ndege angani. Huku kwetu wa miaka hiyo anafanya nini?