Watanzania mnapenda vya bure.
Wakati wafanyabiashara wanalia na TRA sijui mlikuwa katika usingizi gani.
Sasa jukumu la kodi ni kwa kila mtanzania mnaanza kulia lia utafikiri hampangi biashara kando ya barabara zilizojengwa na kodi.
 
Alafu bei ya mazao inazidi kushuka
 
Embu tuiondoe ccm madarakani tuache kulalamika halafu ikifika siku ya uchaguzi tunaipigia ccm kura.
 
Tatizo lipo kwa watanzania wanafuata mkumbo hawajulikani wanataka nini
 
Ewe mama yetu mpendwa sana SSH, ulituletea furaha pasipo raha, miezi mitatu baadae furaha imegeuka karaha.
Ulipochaguliwa nchi nzima watu waliokua na masononeko kwa miaka 5 walianza kufurahi.
Miezi mitatu baadae Mwigulu anataka kukuingiza chaka maana furaha waliokua nayo Mwigulu katia upupu na sasa ni kilio nchi nzima.

1.Ongezeko bei ya Mafuta kunakopelekea bei ya bidhaa zote kupanda.

2.Tozo ktk mitandao.

Mama yetu tunajua wee u msikivu pitia huku utusaidie
 
mama yupo Burundi huko anaendelea kuupiga mwingi.

akirudi aweke kodi ya kichwa ndio ataupiga mwingi zaidi
 
Tujifunze kuepuka kumpa mtu sifa kubwa kuliko uhalisia. Kila linatokea huyo mama analijua na lina baraka zake, Sasa tukikaa humu mitandaoni kuomba mbariki tatizo alete suluhisho ni sawa ni kujitoa ufahamu tu. La Mwigulu ndio la mama.
Tunajua lakini tunataka ajue ni kwa namna gani jamii imelipokeaje
 
Mwingulu ni masalio ya mwendazake ilibidi aondolewa mapema na Mama, pia ana ambition ya kua Raisi mwingulu ni sumu kwa Mama.
 
Tunajua lakini tunataka ajue ni kwa namna gani jamii imelipokeaje
kila mtoa maamuzi hujua athari ya maamuzi yake. Mpaka kuja na hizo tozo na kuruhusu mfumuko wa bei walishajua kuwa raia watalalamika.
Lakini pia walishajua kama ilivyo kawaida ya Watanzania, tutalalamika mitandaoni mwisho wa siku litapita na wao ya kwao yametimia.
Tatizo sio tozo wala bei ya mafuta, tatizo ni msingi tuliowekewa wa kuwa watiifu kiasi cha kuwa wapumbavu.
 

Na kwenye mbolea je?
 



Ukiona unamsemelea sana kiongozi wako kwa boss wake, halafu boss wake anakuangalia tuu na haongei neno Jiongeze
 
Maendeleo binafsi hayapatikani bila ya kuufunga mkanda....

Na maendeleo ya nchi hayapatikani pia bila ya wananchi kuifunga MIKANDA.....

Dr.Mwigulu yuko sahihi kabisa....

#KaziIendelee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…