Tatizo kubwa ni maneno yake dhidi ya raia wenzake kwamba wahamie Burundi.
Katika jamii ya wastaarabu, mashinikizo ya kujiuzulu yasingekoma hadi aachie ngazi.
Hajui tukienda Burundi tutajifunza nini, na tukirudi tutarudi na nini! Wale 'waliokimbia' kule kusini wako wapi?
 
Na kibaya zaidi anawaambia wananchi kuwa lazima walipe hiyo kodi kwa kuwa imeamriwa na Bunge la CCM na kwamba asiyeweza kulipa eti akahamie Burundi. Sijawahi kuona waziri wa ovyo hapa duniani kama Mwigulu Nchemba . Na mama naye amezungukwa na washauri wachumiatumbo wakubwa vinginevyo huyu jamaa hakutakiwa kuwa kwenye baraza la mawaziri. Ana nini kipya hasa mbona kila wizara anayopelekwa anafeli? Kama alishindwa kuongoza wizara ya mambo ya ndani hii ya fedha ndiyo ataiweza? Ebo! Tuacha masikhara jamani.
 
Kwahiyo unataka mteule a resign au mamlaka ya uteuzi ndiyo ijitathmin❓😭
 
Hana tofauti na kingwangala vyeti vimeshindwa kuwasaidia.Heri apewe kishimba angepewa wizara hio.
Wanaachwa watu smart kama kina Dr Kimei,huyu msingida alaaniwe kabisa
Nime "dislike" post yako kwakuwa unampigia debe Kimei ambaye hajawahi kuonesha performance yoyote ya kiuchumi
 
Wee jamaa ndio niliyekuona hapa unapanda mtumbwi ziwa tanganyika kuelekea burundi? Kila lanheri
 
Hahaha chadema walikunaniiii nini maana watu tunajadili km taifa ww unaleta mambo yako uliyomwagiwana chadema....kajifute uleee mi.
Chadema mmeacha madai ya katiba mpya sasa mmehamia kwenye tozo za kodi ya kizalendo, kamwe hamto fanikiwa mnacho kitaka.
 
Hajui tukienda Burundi tutajifunza nini, na tukirudi tutarudi na nini! Wale 'waliokimbia' kule kusini wako wapi?
Ni muhimu tujenge taifa la kistaarabu ambapo viongozi wataheshimu raia na pia wananchi waweze kuwawajibisha inapobidi.
Viongozi kuwa na kiburi cha madaraka hadi kusema hivyo si sawa.
 
Oh he will go, just a matter of time...
 
Mnamuonea Mwigulu. Mchakato wa mswada wowote unaopelekwa bungeni unaanzia kwa Rais na kuishia kwake. Maana yeka ni nini? Kabla Mwigulu hajapeleka pendekezo la tozo hizi za kipumbavu ni lazima alimpelekea kwanza Rais ambaye alibariki. Rais anatakiwa awe na uwezo wa kupima madhara ambayo yanaweza kutokea kufuatana na uamuzi fulani. Kama Rais hakupima na akaruhusu sula liende bungeni, likapitishwa halafu akaja akatia saini, sasa wa kulauniwa ni nani? The buck stops at the President's feet!
Mwigulu aachie madarakaaaa
 
Moderator
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…