Mwigulu Lameck Nchemba, Is The Most Genuine So Far!-Can Make The Best President!-Nimeguswa!


Pasco kuna muda mwingine unatakiwa ukae kimya tu,huku kuongea ongea/kuandika andika kila ukiskiacho/ukionacho kuna siku unaweza kuficha uso wako kwa aibu isiyo mfano!
 
Last edited by a moderator:
Pamoja na kwamba Mwigulu ameongea mipango mizuri kwa mfumo wa chama anachofanyia kazi hawezi kufika popote.Naamini kabisa mgombea atakayesimamishwa na ukawa atawabeba watanzania na kuwainua.
 
Mwigulu yuko upande wa Lowassa; Pasco knows that. Alichokifanya leo Mwigulu ni utekelezaji tu wa "game plan" ya Lowassa.
kweli wewe uko nyuma sana.watanzania wamemsikiliza Lowasa wameambulia kusikiliza diamond na kula pilau.bado wewe unamuwaza.najuwa saa hizi lowasa anaumwa.
 
Its easy drafting sweet words and give it to the people. Mwigulu sijawahi kumkubali hasa wakati yupo bungeni anafanya siasa za maji taka. I discredited him as clean law maker.

Kati ya hao waliotangaza nia so far hakuna anaye na uwezo wa kututoa hapa tulipo kwenda mbele.

Watanzania tuache kuwa wasahaulifu, matatizo yote tuliokutana nayo miaka ya nyuma bado tunawachagua walewale waliotupa matatizo hayohayo.
 
Mbio za kwenda ikulu ni "Power and politics" first you use the people to get at the top, then you hurt and exploit them to stay at the top. That is the physics of political power and that is typical MONARCHY" tuchukue tahadhali na wanaojinadi kuwa na nia na uchu wa kufika ikulu
 
Sorry, he has not impressed me at all:
  1. He has said nothing on the constitution (to me, this is the foundation of everything!)
  2. He's shown lack of experience (Ikama ya leo inayowapa wazee contracts ni matokeo ya kupokea ushauri wa wazungu kama ndondocha. Ajira za serikali zikasimamishwa kuanzia 1992 mpaka 2002.)
  3. He still belongs to the same flock (CCM). They will steal money to get him elected and use that to blackmail him as a president.
  4. We have heard all this before decade after decade and now 50+ years we are retrogressing rather than progressing.
  5. His love for obsolete communist policies makes him a danger to Democracy. I have not forgotten his red star outfit he fondly adorned few years ago.
I will not make up my mind until I hear from all the aspirants (including the opposition)

Thanks
 
Dr ndio mtu anayeweza kutuvusha na Mwigulu a copy speech za Dr, hakuna jipya laweza tokea ccm.
 
Ni kujitoa akili tu,huyu huyu ndo alitupa speech ya Mbowe mwaka jana,na haya haya ndo yaliyolalamikiwa.Haya haya ndo wabunge wa upinzani wamekuwa wakilia na yeye kaja nayo wakati tunakumbuka matusi na kashfa zake kwa upinzani akiyakataa haya. Pasco hawezi tena kufikiria
 
Last edited by a moderator:
Hata hivyo huyo Mwigulu mbona mwanzo tu wa hotuba yake alianza kujihami kuhusu umri unaokubaliwa wa kikatiba kuhusu mgombea Urais?

Naamini hiyo inatokana na ile thread iliyowahi kuwekwa humu jamvini kuhusu genuinity kama yeye ndiye Mwigulu Nchemba original.

Kwa kuwa inasemekana kuwa Mwigulu Nchemba 'original' ni msukuma fulani aliyeko mkoani Shinyanga, bali yeye alilazimika 'kulipora' jina hilo baada ya kufeli mtihani wa darasa la saba na kuamua kuchukua jina hilo na kuanza upya darasa la 6.

Inasemekana jina la Mwigulu 'original' ni Lameck Madelu, ambaye hadi ifikapo mwezi Oktoba mwaka huu atakuwa hajafikisha umri wa miaka 40 unaotakiwa kwa mujibu wa katiba.

Inasemekana pia ukoo mzima wa Mwigulu hakuna ndugu yake yeyote anayetumia ubini huo wa Nchemba.

Kwa kuwa nafasi hiyo ya Urais ni ya juu sana hapa nchini, ni vyema vyombo vya dola vianze uchunguzi kujua kama kweli huyu Mwigulu siye huyo anayedaiwa kuwa ni Lameck Madelu.
 
Pasco umeona vema, nimekuja JF ili niweze kutoa maono yangu ambayo umeyatoa.
Mwigulu hakuwa sana kwenye niliyemtamani. Ni ni kwa vile tu niliona hajakomaa, ila Mwigulu mwenyewe amenijibu swala la kutokukomaa na nimeridhika kabisa, na kwa aliyoyafanya kwa kipindi hiki kifupi kimenidhirishia kwamba anaweza kwa kiwango kikubwa sana kulinganisha na Edo na Wasira, yamkini hata na waliobaki for sure.
Kwanza aliyoyasema tayari alikuwa ameshaanza kuyasema na kuyatekeleza ikiwemo mishahara hewa, na mengine ambayo unaona kabisa hayafurahii anashindwa kuyatekeleza kwa sababu ya serikari butu.
Wakati wa bunge la katiba alidiriki kutoa hoja kwamba ... tunapoteza pesa bure tu katiba haitapatikana ....
Wakati wa Escrow akasema mafisadi na hasa wanaotajwa wamuogope Mungu na kwanza wajiuzuru wakiwemo wa wizarani kwake.

Horuba yake leo imenikosha natamani kusubiria utekelezaji, Tz ya leo inahitaji Raisi wa kutukimbiza, wa kutuwajibisha, aliyemkali kwa kila anayeenda kinyume na atabuliwe kwa hilo, nilikuwa natamani Edo atupeleke mchaka mchaka huu, lakini harufu mbaya ya matumizi ya pesa imenichefua, hapakuwa na ulazima wa kuwa na mkutano mkubwa kivile pesa ikitumika kupeleka watu, hivyo kwake nasema NO na nam delte!

Wasira hana kashfa kihivyo japo hatujaona chakula na chochote cha maana toka wizarani kwake, hata hivyo at 75 tumshukuru tu kwa utumishi mzuri kadri ya uwezo wake. Hivyo kwa masikitiko naye mdelete.

Kama umefanikiwa kuwaangalia wote, lazima uta vote for Mwigulu, speech zao ni tofauti kabisa, Wazee Edo na Wasira wote wamekodolea makaratasi wanasoma, wapi uzoefu hapo? kwa karne hii hatuhitaji viongozi wa makaratasi, Mwigulu yeye Hajaconcentrate kusoma, nahisi alikuwa na kinote kwa ajili ya dondoo tu na muda wote anawaangaliwa watu wake na kusema kinachotoka kwenye moyo.

Hata wanaokuja, Prof Mwandoswa Kichwa sana na Msafi msafi ila umri na afya ningemuomba apumzike akae kwenye ushauri zaidi, Membe .. pole kwani hawezi, Nyarandu na Makamba sijui, labda tuwasikie lakini mhh hawana jipya na record kwenye wizara zao, Makamba hadi sasa bado tunachajiwa gharama za matumizi ya simu ambazo huduma ambazo hatutumii, ninunue bando na simu yangu ya touch upewe MB8 for what? kelele zote hizi kaziwekea pamba. Ukawa ngoja tuwasilikize japo Presential material ni wa kumulika kwenye 500m tunnel kwa touch ya simu yangu ya touch! Nawaombeni tuchague wabunge wa ukawa kwa wingi.

Kweli tukiacha Siasa, naungana nawe Pasco kuwa Dogo, Mwigulu ndio Rais Bora wa Tano.
 
Huyu pasco hovyo kabisa kila cku UKAWA wanaongelea hayo labda ana ajenda, Mwungulu bungeni ana mchango gani na anachokisema?
 
Mwigulu has talked the facts sio kama yule babu jana anayetetemeka tu, tatizo hofu yangu ni kwenye hicho chama alichopo kimeoza balaaa
 
Kanifurahisha alivyokua anajilazimisha kutabasamu baada ya kuona hajaja political icon kum support na mfuko umeshamtoboka na fedha ndiyo hazirudi, uwaziri na ubunge kashaachia yaani he looked quite uneasy. You could see it in his face and his spouse's as well.
 
Insanity is doing the same thing in the same way over and over again and expecting a different result.

Hivi kuna jipya tunasubiria kutoka ccm? Ukoo wa panya huu hata bakuli ya plastiki wanatafuna! Dah

Hili ndio tatizo pekee ninaloliona analo. Kutoka kwenye shimo la ukoo ule ule ni vigumu kubadili system
 
Kaka Pasco, ujanja wote na utoto wa mjini ulionao inakuwaje mtu kama Kibonde akunyanganye tonge?,
 
Last edited by a moderator:

Well said mkuu, hili ni tatizo kubwa mno - baadhi ya wabunge wanafanya usanii tu hawajali mstakabali wa Taifa letu zaidi ya kujali vyama vyao - hawana msimamo kabisa!!! Si ajabu usanii huu ukatumika ndani ya NEC kumpendekeza Rais, wakifanya kosa hilo basi Taifa letu litafanana URUSI wakati wa utawala wa Rais Yeltisin iliyokuwa unaedeshwa na Russian oligarchs by romote control - tukifikia hatua hiyo tumekwisha!!!
 
Hamna kitu ni uwongo uleule tu tuliouzoea kila siku.
CCM wameamua kuwa majambazi live nothing else they can tell us
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…