Mwigulu Lameck Nchemba, Is The Most Genuine So Far!-Can Make The Best President!-Nimeguswa!

Mwigulu Lameck Nchemba, Is The Most Genuine So Far!-Can Make The Best President!-Nimeguswa!

Kwa kweli kama huyu Mwigulu Nchemba angekuwa nje ya maccm basi angekuwa Rais pekee nchi hii,anaongea bila kumung'unya maneno. Wezi na mafisadi wa mali ya umma ni wa kufilisiwa,kushtakiwa na kufungwa bila mjadala.
 
Imetulia hii Mpwa. Umekaa na kufanya yako kwa hekima na busara kubwa, hongera sana. Baadhi ya Watanzania ni wakurukupukaji kupita kiasi sijui kwanini huwa hawapendi kutafakari kwa kina kabla ya kukurupuka na kuandika yale ambayo hayastahili kuandikwa.

Tutaendelea kufanya makosa ya kuwapa mdaraka wasiostahili mpaka lini!? Kwanini hatutaki kujifunza kupitia makosa yetu ya miaka ya nyuma ili kuinusuru nchi yetu ambayo ilitakiwa iwe na maendeleo makubwa sana lakini inayumba miaka nenda miaka rudi kutokana na viongozi wasio na sifa hata moja ya kuliongoza Taifa letu, wezi, wanafiki, majangili, wauza unga, wapokea rushwa, waongo, wahuni n.k. Dah! inauma sana kuwasoma baadhi ya watu humu kwa jinsi wanavyokurupuka kila siku iendayo kwa Mungu.


Mwigulu hawezi kuwa best president wakati amekua ktk fitina... ghiliba na uongo uliokubuhu!!!

Sijui watu mnatumia criteria zipi kumwita MTU the best president bila kuangalia matendo yake ya kila siku na impact yake kwa jamii....

Nitakwenda kuchambua kidogo Ili uone kwa kutumia akili aliyokupa Mungu uchambue na kuchanganua how Mwigulu is the best!!!

1. Mwigulu amefikaje hapo Alipo? ikumbukwe best president au MTU makini hufikia kwenye kilele cha mafanikio kwa njia na mambo makini yanayofaidisha jamii nzima na yenye kupigiwa mifano... mfano wapo watu waliofikia kileleni kwa ubunifu Wa kisayansi.. kifalsafa na hata kiuongozi mfano kina Nyerere!! Mwigullu amefikaje alipo? ni hivi Mwigullu huyu anayemdhihaki mwenzie kwamba bungeni wanabeza upinzani ndiye huyu huyu aliyepewa vyeo kwa kupaza sauti kubwa kubeza upinzani na kutukana wapinzani kwa nguvu kubwa!!

Ilifikia mahali mwenyekiti Wa chama alimsifia mbele ya mkutano kuwa anaiweza Sana kazi ya kutukana wapinzani na hii ilimpaisha kiasi cha kupata uongozi ndani ya chama na serikali kwahiyo huyu ni MTU makini? ni the best one? kivipi wakati alipata ukubwa kwa kubeza waliopaza sauti zao kuikosoa serikali Leo amekosoa nini sasa?

Mwigullu alipanga njama za kuangamiza CHADEMA na kubambikiza MTU kesi ya ugaidi je ana moyo mzuri ambao Rais anatakiwa kuwa nao? MTU ambaye yupo tayari kupika na kushuhudia uongo ili wengine waangamie ni MTU mzuri toka moyoni? anafaa kupewa urais? itakuwaje akipata madaraka na kuyatumia kwa wale asiowapenda??

Sijui watanzania ukiwemo Pasco afya yenu ya kufikiri ina viwango gani kiasi cha kumwita Mwigulu ni the best wakati alipofikia alifikishwa kwa njia zilizojaa damu na ghiliba nyingi.....

Je mgombea wetu ana kitu gani cha ziada cha kuwezesha kumfanya awe icon ya nchi? atakuwaje bora kwa kubeza uozo Wa sasa Wa serikali yake wakati alishiriki kuwaangamiza waliopaza Sauti zao kuukosoa uozo huo?

Mwigulu is a very cheap person with a simple mind!!!!

Hakuna kitu hatari Kama kumkabidhi mamlaka MTU mwenye Akili ndogo!!!
 
mwigulu akikaza anaweza kuja kupendwa na watanzania kama anavyopenda zitto, na pengine kupata umaarufu kama alioupata zitto
 
CCM Haina agenda ya Rais kuna agwnda ya CCM ambayo ndio ilani ya chama. Atakwepaje?
Mtu anayemmsikia huyu jamaa kwa mara ya kwanza leo lazima ameguswa. Lakini haya maono yote haya huwa anayo tangu anaanza kupata airtime kwny TV.
Ila alichowahi kufanya ndio hakionekani. Nilitegemea aseme jambo moja dogo alilolianzisha na kulisimamia hadi likaonekana
 
Amenivutia kwa kuwa na vipaumbele vitatu tuu ambavyo akivisimamia kwa dhati bila uoga Tanzania itakuwa imefanya mabadiliko makubwa sana
 
Mwigulukwa maraya kwanza ameni touch . Hotuba yake ndio mambo ambayo watanzania tunayahitaji na nimeshawishika kumuunga mkono. Lowassa na Wassira hotuba zao hazifikii ya Mwigulu hata robo

Umeuzi watu
 
Hizi Hotuba tamu masikioni mwetu tumezizoea, hata Kiwete kwenye hotuba yake ya kwanza Bungeni alitoa hotuba kali yenye ubora, hakuna mtu anaweza kubadili hii nchi kupitia CCM, we need changes, UKAWA ndio mpango

Umeongea vyema tatizo ukawa umungu MTU Na umm
 
Katika hali isiyokuwa ya kawaida leo katika tamko lako la kutangaza nia ya kuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania umeonyesha kuwa uko serious, mwadililifu, mtu usiyependa makuu .....na ki historia wewe umetoka ndani ya familia masikini kwa hali hiyo unawajua walala hoi naamini kwamba ukipata hutasahau ulikotoka tofauti na hao wengine wenye kumwaga mapesa ili kuutafuta urais... hivi mapesa haya wanayomwaga watayarudishaje? kwa kuisema ukweli kati ya Lowassa na Mzee Wassira mimi binafsi nakupa .......... Bravooooo ...... Mwigulu .... Aluta continua
 
Insanity is doing the same thing in the same way over and over again and expecting a different result.

Hivi kuna jipya tunasubiria kutoka ccm? Ukoo wa panya huu hata bakuli ya plastiki wanatafuna! Dah
 
Yale yale! Nakumbuka Kikwete kuitwa "Chaguo la Mungu" Baadhi ya Watanzania ndivyo walivyo!!!! Huyu kawemo ndani ya MACCM kwa miaka 10 iliyopita huku akiona Nchi yetu ikienda mrama. Ufisadi ukishamiri, wauza unga wakiwa hawaguswi, majangili nao wakiendelea kumaliza tembo mbuga za wanyama, thamani ya shilingi ikiendelea kushuka kwa speed ya kutisha, deni la Taifa likiendelea kuwa kubwa kwa kiasi cha kutisha. Rushwa ikishamiri hadi ndani ya Ikulu na Bunge.

Kauchuna kimyaaaa mpaka leo hii eti ndiyo anataka kujibaraguza eti kuna mfumo mbovu ndani ya MACCM!!! Huo mfumo mbovu ndani ya MACCM mbona uko kwa miaka mingi sasa!! alikuwa wapi miaka yote hiyo kutotoa kauli kuwashinikiza viongozi wa juu wa MACCM ili kuachana na mfumo mbovu na kuhakikisha kunakuwa na mfumo mzuri kwa manufaa ya CCM na Watanzania!? Hizi siasa za kinafiki nchini mwetu zitaisha lini? Ni siasa hizi za kinafiki ndizo zinazoangamiza Taifa letu miaka nenda miaka rudi.

Mtu anakaa kimya miaka 10 nchi ikienda mrama kwenye kila kitu na yeye akiwa na nafasi ya juu ndani ya chama ndani ya Serikali lakini anapretend kama kila kitu kiko shwari mpaka wakati "muafaka kwake" pale anapotaka kugombea urais ndio anaanza kutoa blah blah blah zake "nchi haiko shwari" "mfumo wa chama chetu ni mbovu" blah blah blah!!! Baadhi ya Miafrika kweli ndivyo walivyo!

Duh, hv kumbe ni kweli baadh ya Watz wanafikiri kwa kutumia MATAKO...
 
Yani we jamaa ni kama mwanamke malaya kila mwanaume unamtaka. umeshamkana Lowasa tayari.
 
Mwigulu yuko upande wa Lowassa; Pasco knows that. Alichokifanya leo Mwigulu ni utekelezaji tu wa "game plan" ya Lowassa.
 
Wanabodi,

Tuweke ushabiki pembeni, kati ya watangaza nia watatu kati ya jana na leo, Mwigulu Lameck Nchemba is the most bonafide genuine mgombea so far, ukimuangalia huku unamsikiliza, utaiona his genuinity kutoka moyoni mwake ku practice what he preach na kiukweli nadhani kwa kati ya hawa watangaza nia so far, naamini Mwigulu can make the best president this nation has ever had tangu mwalimu Nyerere!.

Jee wewe mwenzangu ulibahatika kumsikia, unamuonaje?!.

NB Ku make the best president ni jambo moja, mgombea anayependwa zaidi so far ni Edward Lowassa, na mgombea the most experieced so fat ni Stephen Wasira, nikichukulia mchakato wa 2005 wakati JK alipochaguliwa, kama reference, assuming hawa watatu ndio wameingia tatu bora, Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM wakipewa choice ya kuchagua between "the most loved", "the most experienced" and the "the best president", watachagua mtu anayependwa na watu, mtu atakayechagulika kwa urais na kuwatupa the rest, na hivi ndivyo JK alivyochaguliwa ile 2005 kwa sababu kwenye the finalist watatu, kulikuwa na "the most experienced" Dr. Salim, "The best Brain", Prof. Mwandosya, na "the good looking" Jakaya Kikwete, akapitishwa kwa hoja kuwa ndiye anayependwa na watu, as if mapenzi ya watu ndio uongozi wa nchi!.

JF has a role to play kuwaelimisha wananchi wetu waweze kufanya informed decisions kwenye choice of president, ili ifike mahali chaguo la mgombea wa CCM sio lazima ndio automatikally awe rais, wakituletea ule ujinga ujinga kama wa 2005, tunapiga tuu chini only if huko kungine kuna the better alternative!.

Ushauri wangu wa kwanza kwa wana JF, Mwingulu Nchemba is the man to keep watching seriously!.

NB. Kwa walionidhania mimi niko kambi fulani, uzi huu ni uthibitisho kuwa Pasco wa jf, hana chama, hana kambi, hana mtu, ila kuna watu anawakubali akiwemo yule 'jamaa yetu', hivyo sitarajii kuulizwa kama nimehama kambi kwa sababu sijawahi kuwepo kambi yoyote!.

Kiukweli mimi Pasco wa jf, nimeguswa na Mwigulu Nchemba!.

Vipi wewe?.

Pasco
Nakupata Pasco! Jamaa anajua anachokiongea na anajua kuongea kwenye public! Leo kaongea very authoritative na kutoa picha kwamba if he is selected, he can make a best president of United republic of Tanzania! Ki ukweli sina imani na mgombea yoyote toka CCM to date kwa sababu najua Mwigulu kaanza kuongea kwa style ya kuwa upande wa wananchi pale alipoteuliwa kuwa naibu waziri, kabla ya hapo sura yake halisi tulikuwa tunaijua! Sema watanzania ni wepesi sana wa kusahau!
Kifupi speech yake plus appearance, anaonekana kuwa the best president to be, sema moyo wake hatujui umeficha nn!
Ila namsubiri Magufuli ( endapo atatangaza nia kama fununu zilivyo) tuone naye ataongea nn kwani huyo kupitia what He has already done to this nation. Pia uwezo wake wa kuchukua maamuzibila kujali wanaccm wenzake tunaujua! May be that one can make the best president!
Ngoja tuona game hii inaendaje!
 
Last edited by a moderator:
Hauwezi kumpima mwasiasa kwa kuongea tu! Ninafahamu amekuwa naibu waziri wa fedha kwa muda mfupi lakini amefanya nini mpaka sasa kwenye hiyo wizara?

He talks the talk but he doesn't walk the walk, pesa zimechotwa Stanbic Bank under his watch na shilingi inaporomoka kula kukicha lakini hakuna chochote anachofanya.
 
Mimi pia nimeisikiliza hotuba ya Mwigulu Nchemba leo wakati anatangaza nia ya kugombea Urais kwa tiketi ya CCM.

Wakati naendelea kuisikiza hotuba yake nilikuwa naona kama namsikiliza mgombea wa Ukawa, kwa kuwa almost yote aliyoyaongea ndiyo hayo ambayo viongozi wa upinzani wamekuwa wakiyapigia kelele sana kwenye majukwaa ya kisiasa na hata bungeni.

Mkuu Pasco umeeleza kuwa Mwigulu wakati anatoa hotuba hiyo ameonyesha genuinity.

Hilo naweza kupingana nawe kidogo, kwa kuwa ni Mwigulu huyo huyo ambaye wakati wa sakata la Escrow alidai bungeni kwa nguvu sana kuwa atahakikisha wale wote waliopewa mgao na Rugemalira, atahakikisha kuwa wanalipa kodi kwa pesa hiyo chafu waliyopata.

Hata hivyo ile ilikuwa danganya toto tu kwa kuwa mafisadi wale hadi leo hawajalipa kodi ile hata shilingi 10 pamoja na tambo zote zile za Mwigulu!

Sasa hapo genuinity ya Mwigulu iko wapi?

Mfano wa pili ni pale Mwigulu alipokuwa kwenye BMK ya maccm watupu, ambapo alitahadharisha kuwa wabunge waliopo mle bungeni baada ya kutoka Ukawa, hawataweza kupata 2/3 inayotakiwa ili katiba hiyo ipite.

Hata hivyo mwisho wa siku tulishuhudia maccm hao wakiipitisha katiba yao pendekezwa, kwa kupigiwa kura hata kwa njia ya 'sms'kwa wabunge ambao hawakuwemo bungeni, jambo lilioonyesha kuwa katiba hiyo pendekezwa ilipitishwa kwa uchakachuaji mkubwa uliofanywa na wabunge hao wa Sisiem watupu kwenye hiyo BMK.

Ni kwa nini Mwigulu hakuonyesha genuinety yake kwa kukemea uharamia huo wa hali ya juu?

Ni dhahiri basi kwa mfumo wa CCM ulivyo hata atokee mtu clean kiasi gani, hatakuwa na uwezo hata chembe wa kutekeleza yale anayokusudia, iwapo watu wanaomzunguka na kumpa ushauri ni hawa wafuatao:

1. King maker RA
2. Yule mzee mvaa Chou en lai, ambaye jana aliushangaza ulimwengu kutokana na yeye kujulikana kuwa ni die hard Socialist, lakini jana alionekana kama ndiye mpiga debe mkuu wa 'Capitalist' mzee wa mamvi!
3. Nyoka mwenye makengeza msaka pesa

Conclusion yangu ni kuwa hata kama leo atashushwa 'Malaika' toka mbinguni aje ajoin chama hicho cha magamba, hataweza kufanya muujiza wa kubadilisha mfumo wa chama hicho wa kukumbatia rushwa, ufisadi na mafisadi wake.
 
Wanabodi,

Tuweke ushabiki pembeni, kati ya watangaza nia watatu kati ya jana na leo, Mwigulu Lameck Nchemba is the most bonafide genuine mgombea so far, ukimuangalia huku unamsikiliza, utaiona his genuinity kutoka moyoni mwake ku practice what he preach na kiukweli nadhani kwa kati ya hawa watangaza nia so far, naamini Mwigulu can make the best president this nation has ever had tangu mwalimu Nyerere!.

Jee wewe mwenzangu ulibahatika kumsikia, unamuonaje?!.

NB Ku make the best president ni jambo moja, mgombea anayependwa zaidi so far ni Edward Lowassa, na mgombea the most experieced so fat ni Stephen Wasira, nikichukulia mchakato wa 2005 wakati JK alipochaguliwa, kama reference, assuming hawa watatu ndio wameingia tatu bora, Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM wakipewa choice ya kuchagua between "the most loved", "the most experienced" and the "the best president", watachagua mtu anayependwa na watu, mtu atakayechagulika kwa urais na kuwatupa the rest, na hivi ndivyo JK alivyochaguliwa ile 2005 kwa sababu kwenye the finalist watatu, kulikuwa na "the most experienced" Dr. Salim, "The best Brain", Prof. Mwandosya, na "the good looking" Jakaya Kikwete, akapitishwa kwa hoja kuwa ndiye anayependwa na watu, as if mapenzi ya watu ndio uongozi wa nchi!.

JF has a role to play kuwaelimisha wananchi wetu waweze kufanya informed decisions kwenye choice of president, ili ifike mahali chaguo la mgombea wa CCM sio lazima ndio automatikally awe rais, wakituletea ule ujinga ujinga kama wa 2005, tunapiga tuu chini only if huko kungine kuna the better alternative!.

Ushauri wangu wa kwanza kwa wana JF, Mwingulu Nchemba is the man to keep watching seriously!.

NB. Kwa walionidhania mimi niko kambi fulani, uzi huu ni uthibitisho kuwa Pasco wa jf, hana chama, hana kambi, hana mtu, ila kuna watu anawakubali akiwemo yule 'jamaa yetu', hivyo sitarajii kuulizwa kama nimehama kambi kwa sababu sijawahi kuwepo kambi yoyote!.

Kiukweli mimi Pasco wa jf, nimeguswa na Mwigulu Nchemba!.

Vipi wewe?.

Pasco

Umekula maharage ya wapi??

Huwa napenda kusoma post zako, lakini naanza ku-doubt uwezo wako kwa kumsifia Mwigulu. Ananini Mwigulu??
Msanii tu huyo.
 
The guy is simply the best, ana majibu na maswali yote..ni kipindi cha vijana sasa..apewe nafasi. Look T at Kenya Vijana wanavyofanya wonders....ushabiki pembeni the guy is Good.
 
Back
Top Bottom