Mwigulu Lameck Nchemba, Is The Most Genuine So Far!-Can Make The Best President!-Nimeguswa!

Wengine tunaangalia hizi hotuba zao kama burudani tu, ni sehemu nzuri ya kuinjoi ufundi wa maneno.

Tumsubiri January atatisha zaidi, nategemea atakuja na movie ya miiko ya uongozi.
 
Mkuu, Nafikiri swali ni je unaweza kuthibitisha kwa ushahidi usio na shaka kuhusu hayo machache. Kisha tunaweza kujadili hayo mengi.

Hii ni fursa yetu wapiga kura kuwajua hawa watu vyema


Nikuthibitishie nini juu ya Mwigulu kutukana wapinzani kiasi cha JK kumsifia na kumpa vyeo?

Nikusimulie nini kingine kuhusu sinema ya Mwigulu juu ya ugaidi?

Ndugu unaishi nchi hii? mbona niliyoyasema yanajulikana Sana? usipende kutafuniwa tafuta utajua....

Au wewe ni miongoni mwa watu wanaosubiri kuwajua wagombea wakati Wa kampeni tu?

Kuweni serious ktk kufwatilia mambo ya nchi kwa ukaribu ili msikurupuke Kama hivi....
 


Ahsante mpwa!!

Tutaendelea kufundishana ukweli....

UMASIKINI....UPUMBAVU.....UJINGA..... Wa wananchi Wa TZ ndio silaha kuu ya CCM kutawala mpaka Leo..
 
Ata kwa Lipumba ujaona jipya,maana nae Katangaza
 

Eh! tupeni mipango na sisi tuzipate hizo fedha.

Lakini nakubaliana na wewe huyu mjamaa hana mvuto kwenye kuongea. Aende kwa rafiki yake JK au kwa Obama wakamfundishe kuongea.

Mimi kati ya watatu Mzee Wassira ndiyo ameniconvince kwani alikuwa na vision iliyoeleweka, na ameweka vipaumbele kwenye changamoto na jinsi ya kuvitatua.

Ila Mwigulu bado naona hana experience hata katika kueleza hoja kwani alikuwa akitoa maelezo tu hakuwa focused. Too many priorities hata akipewa miaka 20 hawezi kuzitatua
 
Hata akiwa most genuine tatizo mfumo wa ccm inawenyewe subirini mwicho wa mchakamchaka

Chama kipi hakina wenyewe Tanzania?Chadema yenyewe ina wenyewe kama ilivyo CUf ya wenyewe.

Tuangalie mtu, ukiangalia vyama utapotoka.Kwa nchi za kiafrika ni kiongozi mkuu ndiye anayeweza kubadilisha hali.Ukimtazama Mwigulu unaona kabisa kuwa yupo serious na anakerwa na yanayotukera.
 

Haa ha ha Lowassa kichwani mtupu na mdomo pia ndio hivyo ata kutoa hotuba hawezi.

Yeye Lowassa kampeni anafanya kupitia pesa tu, zaidi ya hayo hakuna lolote.
 
Itakuwa Pasco alitegemea atapewa kazi ya kigawa vibahasha kwa Lowassa akapigwa chini.

Inabidi ajaribu bahati yake kwa Mwigulu.

Tukirudi kwenye mada, ni mapema sana ku judge, ngoja na wengine wote wanaojinadi watakapoisha.

ndiyo maana mtoa mada kasema so far. mkuu Pasco nafikiri tuanze kumwita Mwigulu ex machina. ccm sidhani kama wana mtu mwingine atayewaweza wapinzani kwa hoja zaidi ya mwigulu.
 
Last edited by a moderator:
Mwigulu tatizo ni huo upande aliopo..

"kutokana na umuhimu wa hii hutoba naomba niisome" EL, May 30, 2015 Arusha.

Yule mzee wa jana maskini hata ubongo haumruhusu kukariri tena, akaamua kutusomea maandishi tu teh teh teh
 

Kuguswa ni haki yako, lakini busara kidogo tu ilipaswa kukukumbusha kuwa tangu tupate uhuru Tanzania haijawahi kuwa na uhaba wa wanasiasa wanaojua kuongea nini wananchi wanataka kuskia. Huyu Mwigulu ni mhuni wa kisiasa tu, anacheza na maneno. Where has he been miaka yote hii? Huo uchungu kwa Tanzania ni wakati huu anaoutuzuga kuwa anaweza kutuongoza? Don't be fooled kirahisi hivyo. How many times umewahi kuhudhuria interview kwa employer you hate to death lakini ukauelezea wasifu wake kana kwamba wazungumzia malaika?

Hebu tuhabarishe, ukiweka kando kuguswa na maneno yake, kuna kipi katika CV yake cha kuwapa matumaini Watanzania kuwa 'tumepata sokoine mwingine'?

And by the way, Mwigulu ni Plan B ya Lowassa Raia Mwema - Lowassa kuhamia Ukawa?
 
Chombo Kikubwa cha habari kama JF kinashindwa kutuwekea video clips za hotuba za watiania!!!

Pamoja na kwamba sijapata nafasi ya kusikiliza hotuba za watiania kupitia CCM, sidhani kama kuna anayeweza kudhubutu kua-address ama kuazimia kurejesha mezani RASIMU YA KATIBA MPYA ya Mzee Warioba - ambayo ndio mwarobaini wa matatizo yanayolikabili tiafa hili.
 
Mwigulu tatizo ni huo upande aliopo..

"kutokana na umuhimu wa hii hutoba naomba niisome" EL, May 30, 2015 Arusha.

Yule mzee wa jana maskini hata ubongo haumruhusu kukariri tena, akaamua kutusomea maandishi tu teh teh teh

Haa ha ha...mkutano wa jana badala ya kumjenga ndio kwanza umemvua nguo
 
Pasco ndugu yangu! Hapa suala siyo mtu mzuri! Huyu kijana amegusa wengi lkn msiba wetu upo kwenye mfumo!!! Ataongoza chini ya chama twawala sasa yooote mazuri aliyotugusa nayo ikiwa ni pamoja na kuonyesha u-serious waks wakati wa kutangaza nia ni kazj bure! Tatizo hapa ni mfumo na siyo mtu! Mara ngapi mwigulu amelia na ufujaji wa fedha kwenye sherehe na matukio yasiyo na tija lkn ccm wameendelea kuchezea hela za walalahoi bila hata chembe ya huruma!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…