Kwani hiyo mikopo hailejeshwi na riba juu, maanake schem ya mkopo inajiendesha yenyewe, arguments zake za kitoto sana hazina mashiko, ukweli ni kwamba hizi tozo wanaibia wananchi mshahara mmoja unalipishwa kodi nne, kwa pesa hiyo hiyo.
Yale maelezo kwamba wananchi ndio waliotaka TOZO wenyewe yanatosha. Kama kuna ambaye hataki ashinikize zifutwe au akapinge mahakamani mengine ni porojo tu.
Huyu mtu anawaona Watanzania bado wajinga. Viongozi kama hawa ni mzigo. Kwa nini usifikirie kwenye rasilimali tulizonazo kuwa vyanzo vya mapato?. Hapo na yeye anajiona bonge la mbunifu kuwaza wananchi ndio vyanzo vya mapato