Mwigulu: Mkataba wa EPC+F ni Technical sana

Mwigulu: Mkataba wa EPC+F ni Technical sana

Huko kwenye EPC+F ni kwenda kujitafutia matatizo tu. Sio tu kwamba bank zina riba kubwa na middleman juu apate faida hapo hapo making the whole thing too expensive.
Hatuhitaji vitu technical saana, kwa sentesi yako ya mwisho imemaliza killa kitu yalikuwa maamuzi mabovubkutumia njia hiyo.

Lakini wao watajificha kwenye kichaka cha nchi nyingine wanafanya. Inapokuja suala la upigaji ndio tunataka kujilinganisha na nchi nyingine lakini ukiwaambia tuwauate hao pia katika masuala kama ya utawala wa sheria na uwajibikaji hawataki!
 
Hivi hawa watawala hawajisikii aibu! Maana hata mtu mjinga anaona kabisa hawa watu ni wezi waliopitiliza.
Umetumia neno zuri "Watawala" maana hawa sifa zao sio matumizi ya akili hizi zisizokuwa technical, wanakwiba mchana kweupe huku mnaona wakijua hamna cha kuwafanya.
 
Eti yule mwingine akaambiwa futa au badilisha hayo maneno yaliyoko ukurasa wa 34,Yeye akakubali haraka haraka "nafuta,nafutaa ni ajabu lakini ni kweli.
Ni baada ya kibano kuwa kikubwa hali iliyomlazimu kuwa mdogo kama pirton.

Inaonekanaa waziiri wa ujenzi ameingizwa chaka na mawaziri wasomi Dr Madelu na Prof. Mbarawa.
 
Kuna ufisadi mkubwa sana umetokea kwenye miradi inayo endeshwa kwa mfumo wa EPC+F.
Hela imewekwa lakini vigogo wamezichota miradi inakwama mitaani.
Mdee na ufala wake wote hoja yake ilikua ya msingi sana.
Mwigulu aache kutisha watu na Elimu yake ya hapa na pale, ajibu maswali anayoulizwa.
Ifike hatua TAKUKURU iwahoji Mwigulu, Prof Mbalawa alie kua waziri wa ujenzi na uchukuzi.
Kuna mambo hayapo sawa.
 
Kuna ufisadi mkubwa sana umetokea kwenye miradi inayo endeshwa kwa mfumo wa EPC+F.
Hela imewekwa lakini vigogo wamezichota miradi inakwama mitaani.
Mdee na ufala wake wote hoja yake ilikua ya msingi sana.
Mwigulu aache kutisha watu na Elimu yake ya hapa na pale, ajibu maswali anayoulizwa.
Ifike hatua TAKUKURU iwahoji Mwigulu, Prof Mbalawa alie kua waziri wa ujenzi na uchukuzi.
Kuna mambo hayapo sawa.
Labda TAKUKURU ya mbinguni, hii ambayo haiwezi hata kumkamata DC
 
Kwa hiyo Libajaji, Msukuma na wenzao
Waziri wa fedha Msomi Dr Mwigulu Nchemba amewaambia wabunge kuwa mkataba wa EPC +F ni " Technical" sana kwa wananchi na wabunge kuweza kuelewa.

Akitoa ufafanuzi bungeni baada ya Mbunge Halima Mdee kuzuia shilingi ya mashara wa wàziri wa ujenzi kuhusu kushindwa kutekelezwa kwa mkataba huo wa ujenzi wa barabara zenye urefu wa zaidi ya km 2000.

Akijificha nyuma ya neno technical, waziri huuo ambaye anadai ni msomi, amesema watanzania wengi hawawezi kuelewa mkataba huo kwa kuwa ni technical.

Hata alivyotakiwa na Spika Tulia kuueleza kwa lugha rahisi, msomi huyo alianza kutoa mifano ya mikataba ya SGR kuwa ilifuata utaratibu huo.

hata hivyo maelezo hayo hayakuwaridhisha wabunge ambapo mbunge wa Kisesa alisema wabunge wana elewa hizo technicalities tofauti na anavyodai.

Amesema serikali imetoa majibu matatu tofauti kwa suala hilo na kuwataka kuomba radhi kwa kulidanganya bunge pia amemtaka waziri msomi atoe ushahidi kuwa ujenzi wa SGR lot 3 hadi 5 unafanyika chini ya utaratibu wa EPC+F.

Mbunge mwingine alimwambia waziri huyo msomi kuwa watanzania nje ya bunge sio wajinga kama anavyofikiri na kwamba wanauwezo mkubwa wa kuelewa na kuchambua mambo tofauti na anavyofikiri.

Kimbembe hicho kilitokana na mbunge Mdee kukariri maelezo ya CAG kuwa licha ya kusainiwa mkataba wa miradi hiyo utekelezaji wake umekwama.

Akijibu hoja hiyo waziri wa ujenzi, alisema setikali inatauta fedha za utwkelwzaji wake.

Hali hiyo ilisababisha mjadala mkali kwani EPC+F inamtaka mjenzi kutafuta fedha na kujenga barabara ambapo serikali utamlipa mjenzi huyo.

Badala yake serikali imeamua kutafuta fedha za ujenzi wa barabara na baadaye mje huyo atalipwa na serikali.

Spika alihoji sababu za serikali kumtafutia mjenzi fedha na baadaye mjenzi alipwa badala ya kutumia utaratibu wa sasa wa serikali kutangaza tenda na kumpata mkandarasi wa kujenga barabara husika .

Mawaziri watatu walilazikika kutoa ufafanuzi na kudai kuwa riba ya mikopo katika masoko duniani imepanda tofauti na ilivyokuwa wakati wa kuingia mkataba huo, hivyo serikali imechukua hatua ya kutafuta fedha za mradi huo ili mkandarasi aendelee.

Akihitimisha Mbunge Mdee alitaka setikali kufuta kifungu kinachoeleza mkataba huo kutoka katika hotuba ya bajeti na kuweka kifungu kinachoeleza hali halisi
Kwa hiyo Kibajaji, Msukuma na wenzao wataelewa kitu gani hapo? Sifa ya mgombea ubunge aubunge ya kujua kusoma na kuandika tu itamsaidiaje kuchangia kwenye hili!?!
 
Huyo jamaa ana dharau ya asili asee. Kama alishaweza kuwaambia watanzania wahame nchi unamchukuliaje huyo?
 
Waziri wa fedha Msomi Dr Mwigulu Nchemba amewaambia wabunge kuwa mkataba wa EPC +F ni " Technical" sana kwa wananchi na wabunge kuweza kuelewa.
ali kufuta kifungu kinachoeleza mkataba huo kutoka katika hotuba ya bajeti na kuweka kifungu kinachoeleza hali halisi
Nyerere alikuwa anahutubia kwa kiswahili rahisi tu, na hakuwahi kushindwa kueleza jambo lolote kwa kudai ni technical sana. Hivi viongozi wenye caliber hiyo wanapatikanaje? Obama na Clinton nao hujua kueleza mambo complex kwa lugha rahisi sana.
 
Kwani wakati wa kusaini huo mkataba hawakujua riba hupanda kushuka? Hao wakandarasi watafute pesa wajenge, otherwise na sisi twenda ICSID tukawashtaki, mbona wao wanatushtaki kila siku na kushinda matrillion?
10% mkuu...
 
Back
Top Bottom