Mwigulu: Mkataba wa EPC+F ni Technical sana

Mwigulu: Mkataba wa EPC+F ni Technical sana

Kuna baadhi ya vitu haviitaji kabisa kuwa na elimu kubwa ili uvielewe...

Nchemba kwakweli hafai ni basi tu sijui ni nini kinambeba kwenye nafasi hiyo.
 
Binafsi si support huo utaratibu wa EPC+F ni very expensivie na kweli ni technical.

Chukulia mfano Mwigulu kaelezea kupata hizo hela za investment, huyo financier wa magumashi (more like a middleman) maana yeye mwenyewe hana hela anategemea kutafuta syndicate (kikundi cha taasisi) kama banks and other investors watakao changia kutoa hiyo hela inayohitajika.

Mambo kama hayo ndio yaliibua mjadala wa kimataifa na mgogoro kati ya donors IMF/WB na Credit Suisse (whilst acting as middleman) in finding a syndicate ambao watachangia mkopo waliopewa Mozambique.

Mzozo uliibuka Kwa sababu kupata hiyo syndicate (taasisi zitakazotoa hela) na interest charged on the loan; hilo ni tatizo bila ya donors kujua ni shida kwa sababu given a nation default risk (na donors ndio wanaongea na wizara ya fedha kupitia kitengo chao cha DMO regularly na ku-asses debt sustainability) kutokana na madeni nchi maskini waliyo nayo tayari wanaweza asses default risks.

Huko Mozambique kupata huo mkopo walifanya siri given their default risk (IMF/WB) a wakijua.

Donors walipojua baadae ndio ukaibuka ugomvi kati yao na Credit Suisse kuwashutumu for being irresponsible kutoa mkopo kama huo.

Mwigulu kaelezea hilo bungeni kuhusu syndicate (not in details, ndio maana akasema ni techinical kwenda mbele) lakini wabunge wengi wameshindwa kuelewa isipokuwa yule dada aliesema au hamkopesheki.

Maana yake nini kauli ya yule mmbunge aliesema au hamkopesheki in practice IMF/WB baada ya assessment zao wakibaini nchi ni heavily indebted ni jukumu lao kuhakikisha awakopi zaidi ya uwezo wao wa kulipa given the cash flow na existing debt commitment. Wakiona too much risk. lazima watie neno.

Sasa kwenye hii move yetu ya EPC+F achana na currency risk na interest risk (that’s just normal financial concerns kwenye mikopo) ambayo inafanya interest set iwe juu au chini; bado kuna default risk.

Hiyo report wanayosifia ya credit rating agency sijui tupo B2 mama anaupiga mwingi it’s nonsense in practice. B rating (any 1 or 2) is just junk ambayo private bank or any other investor kukupa mkopo riba lazima iwe kubwa B2 or B1 maana yake default risk ni kubwa, sasa jumlisha na currency risk and interest risk concerns hapo utapata wa riba ya chini 10% kweli.

Ndio maana ukisikiliza ule mjadala deductively unahitimisha itakuwa walikuwa na MoU tu na pengine IMF/WB wameingilia kati; Ndio maana huko serikalini wameona umuhimu wa ku negotiate a good deal (which is unlikely to get one) na kuelezea factors on getting a good deal is very technical (waziri yupo sahihi).

Mwigulu kajaribu kuelezea kirahisi kama wameshindwa kuelewa aliyosema kuwaelezea technical issue itachukua siku nzima namna ya ku-negotiate hizo riba given our current credit rating status’s

Aliengia hayo makubaliano ya EPC+F ni fisadi; na keshakimbia (chances are baada ya IMF/WB kustuka) wenyewe wametoana wamemtupa huyo poyoyo Bashungwa zigo la lawama liende kwake na Mwigulu sio financier hajui mambo ya ufisadi anayotetea.

Mama mpaka 2030
 
Nyerere alikuwa anahutubia kwa kiswahili rahisi tu, na hakuwahi kushindwa kueleza jambo lolote kwa kudai ni technical sana. Hivi viongozi wenye caliber hiyo wanapatikanaje? Obama na Clinton nao hujua kueleza mambo complex kwa lugha rahisi sana.
wanajificha kwenye kichaka cha trchnicall saana ili kuwahadaa wananchi ambao sio wajinga kama wanavyofikiri.

Kingine ni ulimbukeni kudhani kuwa kuongea "kidhungu"ndio kuelewa mambo technical saana.
 
Kuna baadhi ya vitu haviitaji kabisa kuwa na elimu kubwa ili uvielewe...

Nchemba kwakweli hafai ni basi tu sijui ni nini kinambeba kwenye nafasi hiyo.
mkuu ni kwa sababu anaelewa vitu technical saana hadi aliyemteua anaona hakunna kama yeye.
 
Watafanya maigizo ya kubana na kuachia kama walivyofanya kwa bashungwa. Kwanini kama bunge lisiagize mkataba huo kuletwa bungeni?
Sio bunge hili!!!! Hakuna watu wa kupinga.
Labda miaka ijayo...
Mungu atupe Viongozi🙏🙏
 
Waziri wa fedha Msomi Dr Mwigulu Nchemba amewaambia wabunge kuwa mkataba wa EPC +F ni " Technical" sana kwa wananchi na wabunge kuweza kuelewa.
Hapa ndipo usomi wa Mwigulu, na wengi wengine unapowaangushia.

Wewe kama msomi, umelielewa barabara jambo unalolisemea, utashindwa vipi kuliewleza kwa wengine na wao waweze kulielewa?

Hiyo 'technical' ni kichaka tu cha kutokuwa na uwezo wa kujieleza kwa wengine wakuelewe unachozungumzia.
 
It can get very technical kwenye kupata hiyo mikopo na kukubaliana riba (you can’t get a fixed rate on long term loans) hasa mikopo ya muda mrefu jumlisha na middle man nae apate faida humo humo; it was a bad idea kwa ujenzi wa barabara.
Sasa si angalau wewe hapa umejipigapiga na kueleza kitu! Kwa mtu mwenye akili ya kutosha tu hata bila kwenda kwenye hizo shule zenu, ukimueleza hizo 'interest zinazo-float' atashindwa kuelewa unaeleza kitu gani?

Sasa hao waliokwenda huko, toka serikalini, ina maana na wao hizi technicalities za mikopo hiyo hawazijui?

Mwigulu usomi wake unamwangusha sana, ndiyo maana sasa anazongwa zongwa sana, hata na watu kama akina Msukuma, watu wasiokuwa na kitu kabisa vichwani mwao; ila wamebahatika tu kujuwa kutembeza midomo yao.
 
Kama kuna currency risk, there must be interest risk na kwenye kuna mbinu za ku-manage risks huko na kuna hadithi za forward rate agreements, interest rate futures, interest rate options, interest rate (caps, floors and collars), interest rate swaps.
Yote haya ni mambo yanayoelezeka, na kwa mtu mwenye akili nzuri yanaeleweka tu.
 
Nchi yako ina mambo technical sana ambayo wewe huwezi kuyaelewa.

Ukitaka kuyaelewa jiunge nao na wewe ufahamu mamno technical ya serikali kukopa fedha na kuipa kampuni tena ya kigeni ijenge barabara na baadaye serikali ilipe mkopo na kampuni wakati Kuna TANROADS, TARURA nk.
Nisaidie.
Najuwa kuna tofauti kati ya mpango huu wa ujenzi wa barabara na mpango tulioutumia kukopa fedha WB na kuboresha Bandari ya Dar es Salaam kabla ya kuwapa DP World waifanyie kazi bandari hiyo na kupata faida; lakini kweli hakuna aina fulani ya mfanano hapa?
Mkopo wa WB tutalipa sisi, siyo DPWorld, na huyu atapata faida kwa kazi atakayoifanya, ingawaje hatumlipi tena.
Majibu nayo ya waziri don’t make sense anaulizwa ume sign vipi mkataba halafu leo hujui interest za madeni au zimebadilika vipi.
Mkuu 'Mayor', hebu na wewe saidia hapa.
 
Yote haya ni mambo yanayoelezeka, na kwa mtu mwenye akili nzuri yanaeleweka tu.
Hapo nimekuwekea options zote, chukulia wewe ndio waziri utatumia risk mitigation strategy ipi na utachagua na kwasababu gani to ensure you get a better deal,

Kwa sababu hayo mambo ni rahisi kuelewa kama unavyodai basi embu tuelezee option yako ingekuwa ipi na kwanini.

Hint kuna hesabu katika kila option to justify your decision, given currency risk issues; mind you we are talking about interest negations.

Kama umesoma maswala ya accounting/finance hayo mambo utakutana nayo mwaka wa nne on ‘advanced financial management’ module trust me it technical and the hardest module in the degree.

Halafu hapo kama waziri wewe ndio waziri wa fedha kutokana na madeni yaliyopo na current payment commitment you have to do explain (portfolio/consolidation ya debt management) it’s technical kwenye negations ya mikopo mipya.

Kwa uwezo wa mapoyoyo yaliyojaa wizara ni concerns za IMF/WB ndio maana hiyo miradi inasua sua, na waliotengeza hayo matatizo washasepa na kuwaachia mziki wengine.

Ndio kama Kafulila na upuuzi wake Mwarabu ataleta mabasi 400 hakuna mtu wa kuleta mabasi mapya kwa volume hiyo on the go; usitete ujinga kwa mambo usiyoyaelewa.

This is where they pay you big bucks as an accountant not tosh issues za hesabu za VAT ambazo wafanyabiashara wabongo zinawasumbua (amazing) beyond me.
 
Nisaidie.
Najuwa kuna tofauti kati ya mpango huu wa ujenzi wa barabara na mpango tulioutumia kukopa fedha WB na kuboresha Bandari ya Dar es Salaam kabla ya kuwapa DP World waifanyie kazi bandari hiyo na kupata faida; lakini kweli hakuna aina fulani ya mfanano hapa?
Mkopo wa WB tutalipa sisi, siyo DPWorld, na huyu atapata faida kwa kazi atakayoifanya, ingawaje hatumlipi tena.
Mkuu 'Mayor', hebu na wewe saidia hapa.
Mkuu.
Mfanano upo, serikali inakopa fedha ambayo italipwa na wasiofahamu mambo technical saana, kisha inayapa makampuni binafsi ambayo ndio wanufaika wa kwanza.

Mambo haya waziri Mbarawa anapaswa kuyajibu kwani ndiye aliyapigia debe kwa kisingizio kuwa ni utaratibu unaofanyika hata kwenye nchi zilizoendelea.
 
Waziri wa fedha Msomi Dr Mwigulu Nchemba amewaambia wabunge kuwa mkataba wa EPC +F ni " Technical" sana kwa wananchi na wabunge kuweza kuelewa.

Akitoa ufafanuzi bungeni baada ya Mbunge Halima Mdee kuzuia shilingi ya mashara wa wàziri wa ujenzi kuhusu kushindwa kutekelezwa kwa mkataba huo wa ujenzi wa barabara zenye urefu wa zaidi ya km 2000.

Akijificha nyuma ya neno technical, waziri huuo ambaye anadai ni msomi, amesema watanzania wengi hawawezi kuelewa mkataba huo kwa kuwa ni technical.

Hata alivyotakiwa na Spika Tulia kuueleza kwa lugha rahisi, msomi huyo alianza kutoa mifano ya mikataba ya SGR kuwa ilifuata utaratibu huo.

hata hivyo maelezo hayo hayakuwaridhisha wabunge ambapo mbunge wa Kisesa alisema wabunge wana elewa hizo technicalities tofauti na anavyodai.

Amesema serikali imetoa majibu matatu tofauti kwa suala hilo na kuwataka kuomba radhi kwa kulidanganya bunge pia amemtaka waziri msomi atoe ushahidi kuwa ujenzi wa SGR lot 3 hadi 5 unafanyika chini ya utaratibu wa EPC+F.

Mbunge mwingine alimwambia waziri huyo msomi kuwa watanzania nje ya bunge sio wajinga kama anavyofikiri na kwamba wanauwezo mkubwa wa kuelewa na kuchambua mambo tofauti na anavyofikiri.

Kimbembe hicho kilitokana na mbunge Mdee kukariri maelezo ya CAG kuwa licha ya kusainiwa mkataba wa miradi hiyo utekelezaji wake umekwama.

Akijibu hoja hiyo waziri wa ujenzi, alisema setikali inatauta fedha za utwkelwzaji wake.

Hali hiyo ilisababisha mjadala mkali kwani EPC+F inamtaka mjenzi kutafuta fedha na kujenga barabara ambapo serikali utamlipa mjenzi huyo.

Badala yake serikali imeamua kutafuta fedha za ujenzi wa barabara na baadaye mje huyo atalipwa na serikali.

Spika alihoji sababu za serikali kumtafutia mjenzi fedha na baadaye mjenzi alipwa badala ya kutumia utaratibu wa sasa wa serikali kutangaza tenda na kumpata mkandarasi wa kujenga barabara husika .

Mawaziri watatu walilazikika kutoa ufafanuzi na kudai kuwa riba ya mikopo katika masoko duniani imepanda tofauti na ilivyokuwa wakati wa kuingia mkataba huo, hivyo serikali imechukua hatua ya kutafuta fedha za mradi huo ili mkandarasi aendelee.

Akihitimisha Mbunge Mdee alitaka setikali kufuta kifungu kinachoeleza mkataba huo kutoka katika hotuba ya bajeti na kuweka kifungu kinachoeleza hali halisi
 
Sasa kama ni technical sana kuulewa yeye alielewaja!
Hivi huyu waziri wa kusaini mikopo anajiona ana akili kuliko wengine?
 
Tunamwomba Mhe. Rais afanye uteuzi mwingine wa Waziri wa Fedha. Mhe. Mwigulu hatoshi katika nafasi aliyo nayo. Maelezo ya EPC+F inamshinda kueleza ili aeleweke.
 
Waziri wa fedha Msomi Dr Mwigulu Nchemba amewaambia wabunge kuwa mkataba wa EPC +F ni " Technical" sana kwa wananchi na wabunge kuweza kuelewa.

Akitoa ufafanuzi bungeni baada ya Mbunge Halima Mdee kuzuia shilingi ya mashara wa wàziri wa ujenzi kuhusu kushindwa kutekelezwa kwa mkataba huo wa ujenzi wa barabara zenye urefu wa zaidi ya km 2000.

Akijificha nyuma ya neno technical, waziri huuo ambaye anadai ni msomi, amesema watanzania wengi hawawezi kuelewa mkataba huo kwa kuwa ni technical.

Hata alivyotakiwa na Spika Tulia kuueleza kwa lugha rahisi, msomi huyo alianza kutoa mifano ya mikataba ya SGR kuwa ilifuata utaratibu huo.

hata hivyo maelezo hayo hayakuwaridhisha wabunge ambapo mbunge wa Kisesa alisema wabunge wana elewa hizo technicalities tofauti na anavyodai.

Amesema serikali imetoa majibu matatu tofauti kwa suala hilo na kuwataka kuomba radhi kwa kulidanganya bunge pia amemtaka waziri msomi atoe ushahidi kuwa ujenzi wa SGR lot 3 hadi 5 unafanyika chini ya utaratibu wa EPC+F.

Mbunge mwingine alimwambia waziri huyo msomi kuwa watanzania nje ya bunge sio wajinga kama anavyofikiri na kwamba wanauwezo mkubwa wa kuelewa na kuchambua mambo tofauti na anavyofikiri.

Kimbembe hicho kilitokana na mbunge Mdee kukariri maelezo ya CAG kuwa licha ya kusainiwa mkataba wa miradi hiyo utekelezaji wake umekwama.

Akijibu hoja hiyo waziri wa ujenzi, alisema setikali inatauta fedha za utwkelwzaji wake.

Hali hiyo ilisababisha mjadala mkali kwani EPC+F inamtaka mjenzi kutafuta fedha na kujenga barabara ambapo serikali utamlipa mjenzi huyo.

Badala yake serikali imeamua kutafuta fedha za ujenzi wa barabara na baadaye mje huyo atalipwa na serikali.

Spika alihoji sababu za serikali kumtafutia mjenzi fedha na baadaye mjenzi alipwa badala ya kutumia utaratibu wa sasa wa serikali kutangaza tenda na kumpata mkandarasi wa kujenga barabara husika .

Mawaziri watatu walilazikika kutoa ufafanuzi na kudai kuwa riba ya mikopo katika masoko duniani imepanda tofauti na ilivyokuwa wakati wa kuingia mkataba huo, hivyo serikali imechukua hatua ya kutafuta fedha za mradi huo ili mkandarasi aendelee.

Akihitimisha Mbunge Mdee alitaka setikali kufuta kifungu kinachoeleza mkataba huo kutoka katika hotuba ya bajeti na kuweka kifungu kinachoeleza hali halisi
Tatizo kubwa la mzee wa scarf na tai ya bendera nikujiona mtaalamu sana kwenye uchumi kuliko mtu yeyote ana Ego sana ila jamaa nichangamoto kubwa katika uchumi wetu huo ndio ukweriiiiiiiii moment tutakapostuka watakua wameharibu sana uchumi na kuja ku repair itatuchukua miaka mingi
 
Naungana nawe lakini, Huu u-mart ya msomi mwenye jufahamu mambo technical sana unatoka wapi?
Wakatti magiufuli akimtimua lwenye uwaziri wa mambo ya ndani alitaja madhaifu yake 11 ikiwemo upigaji.
 
Back
Top Bottom