Wewe unaona hayo ni magumu kueleweka? Umekaa darasani sijui miaka mingapi ukidhani wengine hawawezi kuyaelewa hayo ila wewe mwenye akili tofauti na hao wengine?
Rudi kwenye mada, kwa sababu umesahau hata mada yenyewe inasemaje?
Kama wewe umeyasoma na kuyaelewa, 'trust me' nami ningeingia huko nigeyamaliza tu. Sioni cha ajabu sana hapo.
Mnaposoma, halafu mnashindwa kueleza mmesoma kitu gani na kukieleza kwa wengine wakakielewa kwa lugha rahisi, huo sio usomaji. Mnabaki tu kujipiga vifua muonekane nyinyi ni watu wa kipekee sana!
Actually, hasa kwako, naona huwa una shida sana kuelewa hata kinachoandikwa kwenye hayo unayojibu. Badala ya kujikita na yaliyoandikwa, unarukaruka na kueleza mambo mengine tofauti kabisa na unachotakiwa kujibu.
Tunazungumzia Mwigulu kushindwa kueleza ajuayo kuhusu hoja za wabunge. Badala ya kujibu anakimbilia kwenye 'technical', hiyo technical ni kitu gani kisichoweza kuelezeka kikaeleweka? Sasa na wewe unarudi humo humo kwenye 'technical'; kana kwamba ni nyinyi peke yenu ndio mliivumbua hiyo tecnical' na hamtaki kuieleza kwa wengine.
Bure Kabisa.