Atapata wakati mgumu toka kwa nani? Mikataba, mikopo, matumizi makubwa yafanyika na hakuna wa kuzuia. Si wabunge, si wananchi.Kwa hali ilivyo yawezekana Mwigilu atapata wakati mgumu wakati wa kuwasilisha bajeti kuu ya serikali.
Wewe unaona hayo ni magumu kueleweka? Umekaa darasani sijui miaka mingapi ukidhani wengine hawawezi kuyaelewa hayo ila wewe mwenye akili tofauti na hao wengine?Kwa sababu hayo mambo ni rahisi kuelewa kama unavyodai basi embu tuelezee option yako ingekuwa ipi na kwanini.
Kama wewe umeyasoma na kuyaelewa, 'trust me' nami ningeingia huko nigeyamaliza tu. Sioni cha ajabu sana hapo.Kama umesoma maswala ya accounting/finance hayo mambo utakutana nayo mwaka wa nne on ‘advanced financial management’ module trust me it technical and the hardest module in the degree.
Umenena vyema, wasomi wetu hawa wanashangaza, iweje kitu unachokielewa ushindwe kukuelezea na kujificha kwa hii ni technical saana.Wewe unaona hayo ni magumu kueleweka? Umekaa darasani sijui miaka mingapi ukidhani wengine hawawezi kuyaelewa hayo ila wewe mwenye akili tofauti na hao wengine?
Rudi kwenye mada, kwa sababu umesahau hata mada yenyewe inasemaje?
Kama wewe umeyasoma na kuyaelewa, 'trust me' nami ningeingia huko nigeyamaliza tu. Sioni cha ajabu sana hapo.
Mnaposoma, halafu mnashindwa kueleza mmesoma kitu gani na kukieleza kwa wengine wakakielewa kwa lugha rahisi, huo sio usomaji. Mnabaki tu kujipiga vifua muonekane nyinyi ni watu wa kipekee sana!
Actually, hasa kwako, naona huwa una shida sana kuelewa hata kinachoandikwa kwenye hayo unayojibu. Badala ya kujikita na yaliyoandikwa, unarukaruka na kueleza mambo mengine tofauti kabisa na unachotakiwa kujibu.
Tunazungumzia Mwigulu kushindwa kueleza ajuayo kuhusu hoja za wabunge. Badala ya kujibu anakimbilia kwenye 'technical', hiyo technical ni kitu gani kisichoweza kuelezeka kikaeleweka? Sasa na wewe unarudi humo humo kwenye 'technical'; kana kwamba ni nyinyi peke yenu ndio mliivumbua hiyo tecnical' na hamtaki kuieleza kwa wengine.
Bure Kabisa.
Anabaki kwa sababu anafahamu mambo technical saana, hivyo kumwondoa itakuwa ngumu kupata mwingine.Kuna baadhi ya vitu haviitaji kabisa kuwa na elimu kubwa ili uvielewe...
Nchemba kwakweli hafai ni basi tu sijui ni nini kinambeba kwenye nafasi hiyo.