Wananchi tunahitaji kujua kama Kauli ya Waziri wa fedha Bwn. Mwigulu kwa wananchi wanaolalamikia makali ya tozo kuwa kama wanahisi wanaonewa wahamie Burundi ni ya serikali au ya kwake binafsi.
Tunataka kufahamu hivyo ili tuweke rekodi zetu sawa.
Kwakua Waziri ni sehemu ya Serikali na anaingia kwenye vikao vya baraza la mawaziri.
Kama baraza zima lilibariki tozo basi pia limebariki na kauli hii ya kuhamia Burundi.
Maana kama hukubaliani na tozo basi unapaswa kuhamia Burundi na wananchi wengi tu hawakubaliani nazo.
Serikali itufafanulie kuhusiana na hili jambo ili ukweli ufahamike maana kauli ya serikali ni amri kwa wananchi.