Mwigulu Nchemba: Dr. Slaa na Mbowe wakamatwe kwa ugaidi!

Mwigulu Nchemba: Dr. Slaa na Mbowe wakamatwe kwa ugaidi!

utaifakwanza

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2013
Posts
14,193
Reaction score
2,815
Akichangia bungeni muda huu Mwigulu Nchemba amesema yupo tayari kutoa ushahidi popote pale iwe polisi, mahakamani bungeni hata mbinguni kuthibitisha video ya Lwakatare jinsi alivyoipata, na kwamba kiongozi wa CHADEMA aliyempa pia yupo tayari kuthibitisha mahali popote. Amewataka viongozi wa chadema wasitafute mchawi kwa kusingizia vyombo vya dola hasa polisi na usalama wa taifa kwamba vinahusika.

Amesema ni vyema viongozi wa chadema popote pale walipo waende kwenye nyumba za ibada zilizopo karibu nao wakatubu na kuungama kujisafisha na matendo maovu ya kigaidi na mauaji wanayoyafanya. amewashangaa kutaka madaraka huku wanawaua wananchi wanaotaka kuwaongoza...awaambia shame on you, look at you chadema!!!!!

Amesema ile ya chadema iliyowasilishwa na Mbowe ilikuwa ni malalamiko ya kambi ya upinzani na sio hotuba ya kambi ya upinzani kwa kuwa haina mapendekezo wala solution ya matatizo pamoja na kwamba ina urefu wa kurasa 70.

Amelitaka Jeshi la Polisi limkamate Mbowe kwa sababu ndiye anayewasiliana sana na LWAKATARE kwa kuwa ni mkurugenzi wao wa ulinzi na usalama, kufuatia maelezo ya Mbowe jana, kwamba anayewasiliana na gaidi naye ni gaidi pia hivyo akamatwe.
 
Mheshimiwa sana Mwigulu Nchemba ameibuka na kile kilichotarajiwa kwa kuongelea suala la Mkanda wa Lwakatare huku akiwaomba Polisi kuwakamata viongozi wa CHADEMA kwa ugaidi.

Comedy ni pale spika alipofunika kombe mwanaharamu apite kwa kuzima miongozo yote juu aliyokuwa anayasema Mheshimiwa huyo. Kasoro Utaratibu kutoka kwa Mheshimiwa Akunay na huku aki rule very politically.

Source; TBC1 Live coverage
 
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Spika Makinda ameendelea kutetea uvunjifu wa kanuni za bunge pale Mwigulu Nchemba aliposimama na kushambulia CHADEMA na viongozi wake hasa Mbowe kwa kumtaja jina na akisema hawa wote ni magaidi hali iliyopelekea Joseph Selasini aombe utaratibu kumtaka Mwigulu kufuta kauli yake ya kumshambulia Mbowe kibinafsi na kumtaka aache kuongele swala lililo mahakamani.

Hili linaenda pabaya kama Makinda hajakoma tabia ya kutetea upuuzi
 
Mwigulu Nchemba amesema bungeni Dr Slaa na Mbowe wakamatwe kwa ugaidi. Alisema Fedha walizolipwa vijana kufanya ugaidi ni fedha za chama, kwa hiyo uongozi mzima wa CDm ukamatwe. Amesema anashirikiana na viongozi wachache CDM wanaokerwa na mambo machafu ndani ya CDM
 
Akichangia bungeni muda huu mwigullu nchemba madellu lameck amesema yupo tayari kutoa ushahidi popote pale hata mbinguni kuthibitisha video ya lwakatare jinsi alivyoipata, kiongozi wa chadema aliyempa pia yupo tayari. Amelitaka jeshi la polisi limkamate mbowe kwa sababu ndiye anayewasiliana sana na LWAKATARE.

Nimemsikia pia akisema kuwa viongozi wa CHADEMA wasihangaike na kuzua uongo kuwa Usalama wa Taifa na polisi wanatekeleza mpango wa kukidhoofisha chama hicho kisiasa. kwamba kiongozi wa chadema aliyempa mkanda huo yupo tayari kutoa ushahidi na yeye (NCHEMBA) yupo tayari kutoa ushahidi iwe Bungeni, Polisi, Mahakamani na hata Mbinguni
 
hili jamaa uwelewa wake ni mdogo sana, atachukiwa sana na jamii kwa siasa zake za kipuuzi na kwa kwendo huu hatafika mbali kisiasa.

Wazee mkeemeeni kijana huyu maana ameivamia siasa kwa pupa.
 
Kwa nini hataki kuisaidia polisi.Ningekuwa kwenye nafasi ya Mwigulu toka siku ya kwanza aliyopewa mkanda huo angeukataa na kumwambia huyo kiongozi auwasilishe mwenyewe kwenye kituo cha polisi kilicho karibu.Vinginevyo amejiweka mahali pabaya sana.Mbowe lazima awasiliane na Lwakatare kwa nafasi yake ,hivyo hicho alichokisema kuwa akamatwe sababu anawasiliana na Lwakatare halina mshiko.Ila kama kaburi amejichimbia refu mno.
 
Kwa hiyo Makinda alifanyaje baada ya Joseph Selasini kuomba muongozo
 
Huyu mwehu huyu ...eti Ma engineer wakafundishe shule za kata...alaf walipwe acccordingly...wakati hao tu walimu wameshindwa kuwalipa...

Ati Viongozi wa CHADEMA ndio Magaidi na wauaji ...na yupo tayri kutoa ushahidi na pia aliyerecord video ile yupo na yupo tayari kusema chochote..
Ati "You look Messless,shameless...look at you "
 
Katika hali isiyokuwa ya kawaida,Spika makinda ameendelea kutetea uvunjifu wa kanuni za bunge pale mwigulu nchemba aliposimama na kushambulia chadema na viongozi wake hasa mbowe kwa kumtaja jina na akisema hawa wote ni magaidi hali iliyopelekea Joseph Thelathin aombe utaratibu kumtaka mwigulu kufuta kauli yake ya kumshambulia mbowe kibinafsi na kumtaka aache kuongele swala lililo mahakamani.hili linaenda pabaya kama makinda hajakoma tabia ya kutetea upuuzi

Wabunge wa TZ wanapoteza muda mwingi kujibizana kuliko kujadiri hoja.. Mh Nchemba amenisikitisha sana maana ameidharau mahakama na amevunja kanuni za bunge huku spika akisema "mkuki kwa nguruwe"😡
 
Akichangia bungeni muda huu mwigullu nchemba madellu lameck amesema yupo tayari kutoa ushahidi popote pale hata mbinguni kuthibitisha video ya lwakatare jinsi alivyoipata, kiongozi wa chadema aliyempa pia yupo tayari. Amelitaka jeshi la polisi limkamate mbowe kwa sababu ndiye anayewasiliana sana na LWAKATARE.

hebu tujuze vizuri mkuu kweli kasema yuko tayari? basi ukweli utajulikana na muongo lazima anaswe make huu ndiyo mwisho wa mbichi na mbivu za ugaid ktk nchi yetu
 
Spika Anna Makinda, ameruhusu Kiongozi wa Upinzani Bungeni kushambuliwa, kuhusu matokeo yake akiwa Shuleni, akaruhusu CHADEMA waitwe wauaji, akakataza waliotaka Mwigulu afute kauli Bungeni, akashangilia pamoja na Wabunge wengine wa CCM waliokubaliana na maneno hayo.

Watanzania wanaangalia Bunge, wanajua Bunge linavyoendeshwa. Wanajua Spika unavyofanya, wanaona Unavyopendelea. CCM mmeshangilia sana, hongereni. Mlianza na Udini wa CUF na sasa wa CHADEMA, Mkaja Ukatoliki wa Slaa, na Uchaga wa CHADEMA.

Mlijaribu Udini suala la Kuchinja limepata busara ya Mwinyi tumepata nafuu ya siku moja. Sasa la Kuchakachua Katiba kunakoendelea mtaani sasa, na kuruhusu ujinga Bungeni kuipendelea CCM kutukana........... mnaharakisha kupeleka nchi kusikovutia wengi.
 
Katika hali isiyokuwa ya kawaida,Spika makinda ameendelea kutetea uvunjifu wa kanuni za bunge pale mwigulu nchemba aliposimama na kushambulia chadema na viongozi wake hasa mbowe kwa kumtaja jina na akisema hawa wote ni magaidi hali iliyopelekea Joseph Thelathin aombe utaratibu kumtaka mwigulu kufuta kauli yake ya kumshambulia mbowe kibinafsi na kumtaka aache kuongele swala lililo mahakamani.hili linaenda pabaya kama makinda hajakoma tabia ya kutetea upuuzi
Mwigulu anasema atatoa ushahidi kwamba cdm inahusika na kupanga mauwaji....
Ana mpaka maandishi ya huyo alierekodi..
anasema CHADEMA iko kama mchawi..! kwamba inaloga alafu inakuwa wa kwanza kulia kilioni
 
wafu hao, wacheni wachangieni siku zilizobakia kubakia madarakani.
 
Sasa kama yuko tayari kutoa ushahidi,tatizo likwapi?
Mwacheni akatoe popote anapotaka kama ni fake itajulikana tu.
 
Back
Top Bottom