Mwigulu Nchemba: Dr. Slaa na Mbowe wakamatwe kwa ugaidi!

Mwigulu Nchemba: Dr. Slaa na Mbowe wakamatwe kwa ugaidi!

Kwa hiyo mwigulu ana mkanda wa mauaji, Mbona haupeleki polisi?
 
Spika Anna Makinda, ameruhusu Kiongozi wa Upinzani Bungeni kushambuliwa, kuhusu matokeo yake akiwa Shuleni, akaruhusu CHADEMA waitwe wauaji, akakataza waliotaka Mwigulu afute kauli Bungeni, akashangilia pamoja na Wabunge wengine wa CCM waliokubaliana na maneno hayo. Watanzania wanaangalia Bunge, wanajua Bunge linavyoendeshwa. Wanajua Spika unavyofanya, wanaona Unavyopendelea. CCM mmeshangilia sana, hongereni. Mlianza na Udini wa CUF na sasa wa Chadema, Mkaja Ukatoliki wa Slaa, na Uchaga wa Chadema. Mlijaribu Udini suala la Kuchinja limepata busara ya Mwinyi tumepata nafuu ya siku moja. Sasa la Kuchakachua Katiba kunakoendelea mtaani sasa, na kuruhusu ujinga Bungeni kuipendelea CCM kutukana........... mnaharakisha kupeleka nchi kusikovutia wengi.

Kwa hili mimi napingana kabisa na wewe ki msingi spika hana makosa kwani hata jana kwenye hotuba ya Mbowe kama ulifuatilia vizuri alizungumza maneno makali sana na kwa suala hili alimlenga Mwigulu moja kwa moja na Mwigulu alikuwepo alitulia tuli sasa tatizo nini Mwigulu kujibu hoja leo. Mimi nadhani paia Mwigulu kasaidia kasema yupo tayari kutoa ushahidi popote tatizo ni nini? Kama CHADEMA kitaendeshwa kwa kila kitu kuona kuwa kinaonewa ni ngumu sana kukijenga chama na kwa utaratibu huu nina wasiwasi mkubwa kama wakipewa madaraka ya nchi watakuwa ma dictator kwani siku zote dictator hapendi kukosolewa
 
CCM with new shot selection, Target ''BUNGENI" nawasubiria CHADEMA na counter attack!!! Hivi LIVE coverage kama inavyosemeka haijawa edited? nauliza tu huku nikiendelea kufuatilia kwa karibu zaidi na kutarajia mapya toka kwa vyama hivi 2..... jana Mbowe kamtaja Mwigilu na leo Mwigilu kamtaja Mbowe!
 
mkuki kwa nguruwe......... Jana wakati mbowe akiwasilisha malalamiko ya kambi ya upinzani mlishangilia. Leo mmejibiwa mnaanza kutapatapa
kwa akili yako unaona mwigulu nchemba kajibu hoja badala ya viloja??
 
Huu udhaifu na uhuni wote chanzo chake kinajulikana,ogopa na dharau sana kiongozi wa taasisi au chama fulani aneamini kua kwa dunia ya leo,kitengo cha propaganda bado ni muhimu katika chama!mara muhimili mmoja ushikiliwe na mwanamke,hata kama hana uwezo!!ili bunge limekua ni la ajabu kabisa,halina tija tena kwa taifa letu!vinajadiliwa vitu vxa hovyo kabisa,na hii ni kwa kua wengi ya wawakilishi wetu wako hovyo kabisa vichwani mwao!wametuona wananchi ni mazuzu wanapga propaganda za kitoto kwa manufaa ya matumbo yao,kumbe hawajui wananchi wa leo wamesha anza kubaini pumba na mchele
 
Jana iliwekwa thread hapa JF inayosema "KUBWA LA MAADUI LIKAMATWE".

Thread ile ilifutwa baada ya wadau kulalamika.

Kufutwa kwa thread ile kumeinyima JF opportunity ya kujadili au kuyajua mambo in advace - the first to know.

Kimsingi kilichoandikwa kwenye thread ile ndicho kilichosemwa leo Bungeni.

Nadhani tuna haja ya kuongeza degree ya kuvumilia mawazo tofauti. Ile thread ingekuwepo hapa ingeipa JF heshima zaidi na mawazo mengi ambayo yangeongelewa kwenye ile thread yangeweza kutumiwa Bungeni.

Cc: Paw PainKiller Buchanan Cookie Fang

Nakuunga mkono mkuu
 
Mwigulu amesema pia kwamba ndani ya chadema kuna viongozi wasiopenda mauaji
 
Nimemsikia Nchemba alivyokuwa akiongea, katika hali ya kawaida, Nilitegemea Lukuvi angasemama na kusema kuhusu utaratibu, sikumsikia. Mbaya zaid Spika akanogewa na utamu wa mada aliyokuwa akiiwakilisha Mwigulu akaruhusu Mwigulu akamaliza matusi yote tena kwa kutaja jina-Lukuvi anasemaga kanuni zinakataza kabisa, kutaja jina la mtu kwa dhihaka.

Spika ameombwa atoe utaratibu kuhusu kitendo hicho cha kumruhusu Mwigulu kuvunja kanuni, Spika kasema kwa kuwa jana alimruhusu Mbowe asome na amalize speech yake iliyojaa lugha kama alizotumia Mwigulu ndo mana leo kamruhusu Mwigulu, ila baada ya tukio hili la Mwigulu, wabunge wote sasa waobserve kanuni. Huu ni upuuzi kabisa!

Kama Spika aliona Mbowe anapotoka kwanini hakumzuia na kumtaka afute kauli??? Inaleta tija gani kuona mbunge anaenda nje ya mstari then unamuacha ili uruhusu baadaye mbunge mwingine aje kuvunja kanuni ili kurevenge?? Uendeshaji huu wa bunge hautatufikisha mahali.
 
kumbe mambo yaliyoko Mahakamani yanaruhusiwa kuongolewa Bungeni?
 
Suala la Ugaidi (kupanga mauaji ya mtu/watu) na uvunjifu wa amani ya nchi ni kitu kibaya sana, mimi nashangaa kwa nini serikali yetu makini na jeshi la polisi makini mara tu baada ya mwigulu kusema anao mkanda wasimuite kumhoji kwanza kwa kuzingatia nafasi ya mwigulu katika jamii, na zaidi nazidi kushangaa, bado mwigulu anaendelea kusema anao ushahidi kwa nini polisi wasimalize kazi kwa kumuhoji huyu?
Amesha fikisha kile alichonacho mahakamani (tape, notes)
Mi nashangaa sana CHADEMA kuwasilisha hoja hili bungeni
Hata kama wanataka kumsaidia, wamsaidie tu, bunge la nini?
 
"Pili, kwa mujibu wa Sheria ya Ugaidi, mtu yeyote anayefanya mawasiliano na gaidi au magaidi, yeye pia anahamasisha ugaidi, hivyo naye anastahili kuunganishwa katika tuhuma hizo za mashtaka ya ugaidi," alisema Mbowe.

Hakutaja huyo anayejihisi mwenyewe.
 
Mwigulu akapimwe akili isije ikawa ana mtindio wa Ubongo na Makinda awe fair kuendesha kikao cha Bunge japokuwa yeye ni kada wa CCM na amewekwa na Mafisadi.
 
Leo wakati akichangia hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu,Mbunge wa Iramba Magharibi Mh. Mwigulu Nchemba amewambia viongozi wa CDM wakatubu Kanisani na Misikitini kwa kuwa wanahusika na Utekaji na Mauaji ambayo yamekuwa yakitokea katika shughuli za kisiasa Yupo tayari kutoa ushahidi popote atakapohitajika,viongozi wa CDM wanajifanya wazalendo kumbe nyuma ya pazia ni wauaji na magaidi.
 
Mkuki kwa Nguruwe......... jana wakati mbowe akiwasilisha malalamiko ya kambi ya upinzani mlishangilia. leo mmejibiwa mnaanza kutapatapa
huwezi kusonga mbele kisiasa bila kuwa na nguvu ya kujenga hoja, kijana gani anayejiita msomi anakuwa na mambo ya kizamani ya kinafiki, fitna, kujipendekeza kwa watawala namna hiyo? eti uzalendo, upi kila siku kuasisi udini kuwatenganisha watanzania kisa tamaa ya madaraka; niamini mimi CCM makini huyu jamaa hawezi kuwa na nafasi yoyote!. CCM chini ya mwalimu huyu asingefaa hata kuwa katibu wa tawi.
 
Leo ndio nimeona live lile jambo ambalo nilikuwa nasibiri alitamke huyu jamaa kuhusu Sakata la Rwakatare na nione ataongea akiwa ktk mood gani, yaani kakiuka kanuni za bunge wazi wazi kwa kuongelea mambo ambayo yapo mahakamani na mh. Spika hajfanya au kusema lolote kuhusu ukiukwaji huu even kusema " Kauli ifutwe" kama ilivyo kawaida pale mbunge akikosea jambo hasa upande wa kauli. Kuna mbunge kanukuu kanuni aliyoikiuka nchemba na spika kaishia kusema" kanuni zizingatiwe na wabunge wote". Jingine aliloongelea nchemba kuhusu elimu kuwa ili kunusuru kufeli kwa vijana wa sekondari hasa kwa lililotokea mwaka jana eti wahitimu wa vyuo vikuu wote isijalishe fani aliyosomea waajiliwe kuwa walimu kwa mishahara ambayo inafanana na wenzao wanaofanya sehemu nyingine wenye equivalent education. Anahoji je mwanasheria mwenye degree atashindwa kufundisha english form I? Au engineer ashindwe kifundisha maths 4m II? Najiuliza huyu jamaa ni mwehu au ana tatizo ? Yaani yupo kishari sana na waliomchagua wanamuona na kumsikia anachosema huyu jamaa?
 
Kila la kheri Mwigulu Nchemba, bila shaka unajua unachokifanya na matokeo yake kisiasa na kijamii.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom