Nitoe mfano ili Polisi waelewe vizuri tunaposema kwamba Mwigulu Nchemba ahojiwe au akamatwe,
Ikiwa Mwigulu angepeleka kiungo cha binadamu (albino) kwamba amekabidhiwa na kijana mmoja ambaye alishiriki kukikata, hawa polisi jambo linalofuata wangemwambia Mwigulu uko chini ya ulinzi na twende ukatuonyeshe huyo kijana. Badala yake Polisi wanaendelea kumsikiliza akitoa ushahidi zaidi kwa ushirikiano na huyo CDM aliyekerwa na Chadema.
Jambo la pili ni kwamba Mwigulu na huyo CDM anayekerwa na Chadema wapo nje kwa ridhaa ya Polisi. Mwigulu kosa alilofanya ni kupokea hicho kithibiti. Kwa kudhani kuwa angeonekana ni jasiri akapokea, alichotakiwa kufanya alitakiwa kumshauri mtoa taarifa wake huyo kukipeleka yeye mwenyewe polisi. Hadi sasa nani ataamini kuwa video haikufanyiwa editing. Tupo tunaendelea kushangaa tunasubiri mwisho wake.
Kuhusu Makinda kuegemea upande mmoja ni ukiukaji wa maadili ya KIONGOZI WA SERIKALI. Kuna wakati kiongozi unayepeperusha bendera ya Serikali aachane kuzungumzia chama chake. Makinda kasahau kuwa ni kiongozi wa MHIMILI wa serikali. Labda nimkumbushe kuwa hata kiti alichokalia hapo Bungeni hakina NEMBO ya CCM bali NEMBO YA SERIKALI (BIBI NA BWANA) Sisi wananchi tunaumia kwa uongozi mbaya wa watendaji tuliowaamini, ifike muda kuwe na kanuni ya kuwaondoa madarakani pale wanapoenda kinyume cha taratibu ambazo ni maslahi ya taifa.