OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,868
- 121,001
Waeleze mtaalamHizi tozo si ndiyo hodi zenyewe!
Daah kweli hii ni uchumi uchumini...Mungu saidia nchi ya TanzaniaSerikali ina jaruba la pesa za kulipa?
ULisikia vyema yaani watu 1mil wapelekewe 161bil alafu watu 61mil wapewe 91bil?Wadau naomba kufahamu kama Tozo ni jambo la Muungano.
Kwani nimemskia Waziri wa Fedha Bw. Mwigulu Nchemba akidai kuwa kwa Mwezi wa Dec 2021. Zanzibar imepelekewa Bil. 161Tshs ili hali Bara Tshs Bil 91. Ina kuweje Pesa za Walipa kodi wa Bara ziende Zanzabar? Zanzibar ina watu wake wa kulipa Tozo. Inakuweje hii? Je ina maana kila mwezi Pesa za Bara zina pelekwa Zanzibar? Au ndio kujipendekeza bila kujali Sheria, taratibu na misingi ya Muungano pamoja na Sera za Fedha?
Dah DR inakuwaje tena uchumi wa wapi huu mlipa deni ni mwananchi kupitia kodi za kila siku.Waziri wa Fedha na Mipango Dr Mwigulu Lameck Nchemba (PhD) leo amewaondoa wasiwasi wananchi wanaolia kwa sababu ya ukubwa wa deni la taifa (Trilion 70+) kwamba hakuna mtanzania hata mmoja atakayegongewa mlango au kutakiwa kutoa mali zake binafsi ili kulipia deni la taifa. Amesema deni hilo litalipwa na serikali yenyewe kwa fedha zake bila mwananchi yeyote kutakiwa kutoa hata senti moja ili kulipia deni. Msikilize wewe mwenyewe kwenye klipu hii hapo chini π π π π π
Dr Mwigulu alisema hayo wakati Rais Samia alipokuwa akihutubia Baraza la Mawaziri ikulu Jijini Dodoma ili kuweka mambo sawa baada ya Spika wa Bunge kuwa mbogo kuhusiana na ukubwa wa deni la taifa ambapo Spika alisema kuwa serikali ya Samia isipokuwa makini kwenye ukopaji, ipo siku nchi hii itauzwa kwa sababu ya ukubwa wa madeni.
MAONI YANGU
Nawaomba wananchi tutulie, tuache kupapalika bila sababu kwa kuwa sasa tumehakikishiwa kwamba hatutahusika hata chembe kwenye ulipaji wa deni la taifa. Nawashangaa sana watu wanaowapotosha wananchi kwa makusudi kuwa watahusika kwenye ulipaji wa deni la taifa huku wakijua fika kwamba serikali itajilipia yenyewe deni lake. Tuache upotoshaji ndugu watanzania. Kuna makundi ya watu wabaya wanaotumia na watu wasioitakia mema nchi hii kuifarakanisha serikali na wananchi wake. Tuwe makini! βοΈ
Kweli kabisa mkuu. Hata MwanaHalisi Online imeandika pia. Swali la Msingi. Tozo ni kodi mpya ya Simu. Wizara ya Fedha siyo ya Muungano. Watu mil1 wa Zenj watozwe zao. Na sisi mil 60 tutozwe kwa maendeleo yetu. Ratio ni ileile. Why pesa za Bara ziende Zanzibar?ULisikia vyema yaani watu 1mil wapelekewe 161bil alafu watu 61mil wapewe 91bil?
Kama ni kweli basi kuna upande mmoja wa Muungano ni .................au basi nsije tukana bureKweli kabisa mkuu. Hata MwanaHalisi Online imeandika pia. Swali la Msingi. Tozo ni kodi mpya ya Simu. Wizara ya Fedha siyo ya Muungano. Watu mil1 wa Zenj watozwe zao. Na sisi mil 60 tutozwe kwa maendeleo yetu. Ratio ni ileile. Why pesa za Bara ziende Zanzibar?
Walikomaa Zanzibar ikope kama nchi. Wameruhusiwa tiyar. Ni kwa nn pesa za Tanganyika Ziende Zanzibar?
Haitakiwi kupewa hata shs1. Hii ni tozo. Ratio ni ileile. Zanzibar ina watu wake sijui mil 2. Bara ina watu wake Mil 60. Why pesa za tozo za simu za Bara ziende Zanzibar? Hii maana yake wao wana faidi mara 2.Kama ni kweli basi kuna upande mmoja wa Muungano ni .................au basi nsije tukana bure
HI ratio ya wapi hii wachache wapewe kingi alafu wengi wapewe kichache