Mwigulu Nchemba, hata kama Magufuli hayupo hai ulipaswa kumheshimu

Sijui Kalamaganda Kabugi atajipendekezaje mwaka huu.
Akumbuke yeye, Mwanri na shehe ubwabwa wa Dar walishawshi kumkweza mwendazake kuliko aliyewapa uhai.
Mwanri naona kosa limemsuta Hadi amejifunza uinjilisti.
 
mh, ila yanayomkuta JK kikwete nina hakika hata Nyerere hakuwahi kuyakabili......jamaa anaandamwa sana aisee;

wakati wa utawala wake chadema walihakikisha hafanikiwi kwa lolote, kiubishi ubishi sana akapenya!

anaandamwa kuwa eti alimsaliti lowassa.....yet, hakuna mwenye kuujua undani hadi sasa.

wakati wa utawala wa mwendazake, aliandamwa mno kwa kukosolewa kuwa hakufanya chochote wakati wa utawala wake na hata kunyamazishwa 'kibabe' mbele ya kamera pale aliojaribu kutoa maoni, hilo lilifanywa na mwendazake mwenyewe na 'washikadau' wake.

sasa hivi (wakati huu wa awamu hii ya sita), anaandamwa kwa kila hatua anayoichukua mama.....kwamba eti ndiye anayeongoza nchi sasa. kama hilo halitoshi, anaambiwa kuwa anahusika na kuondoka kwa mwendazake. kivipi? hakuna mwenye jibu.

Mungu ni mkubwa, na mapito haya pia yatapita......pole sana JK Kikwete, tunapokuona na tabasamu lako pamoja na yote haya, hakika wewe ni jasiri sana!!
Mimi binafsi nafarijika sana kuona haya yote yametokea - Karma ni hapa hapa duniani. Huyu ndugu tabasamu ndiye aliyetuletea Hayati Mwendazake, na hivyo kila aina ya maumivu ambayo taifa hili limeyapata katika kipindi cha awamu ya 5. Ndugu tabasamu alimfahamu vizuri sana mwendazake lakini hakujali madhara ambayo angesababishia taifa kwa vile yeye anakula na kulindwa na mafao ya urais. Mwendazake hadi alimpa zawadi ya kumfanya Mama Salma kuwa mbunge, na katika uchafuzi mkuu wa 2020 alihakikisha mtoto na mama wanaendelea kuwa bungeni. Sasa Mungu ni fundi - huyu ameenda zake na huyu pushgang limemvalia njuga. Karma, Karma, Karma.
 
Dah, em vuta picha haya maneno yangekua yanaongelewa kumhusu Baba yako,

Tuihurumie familia yake mazee.
Kweli aisee japo umekosea kidogo; sema 'babu yangu' mimi naona poa tu sasa wewe watu karibia wote familiani wana nafasi ya kula keki ya taifa unadhani wanaumia hapo?
 
Sasa
naweza kuwa unpopular minister of finance ila ni lazima mambo yaende.Nikipendwa na wapiga kura wangu na mashabiki wa Yanga inatosha" -@mwigulunchemba
Hivi ina Maana Petrol Ikipanda Bei kule Singida Haitapanda??? Au Watu wa Yanga watakua na Kadi Maalumu kununua petrol au Diesel kwa bei nafuu???

Mama Samia Nakushauri hii budget ya kuongeza hela kwenye mafuta ni janga kubwa...Hii inaenda kupandisha bei kila kitu na kuwa balaa kubwa...Usikubali hii....

HAWA WATU hawaaminiki watakuingiza chaka
 
Lakini pia kumtaja JK kwa kumuunganisha na Mama Samia kunaleta picha kwamba bila JK uamini Kama Rais aliyepo anaweza kuongoza nchi. Naweza nisiwe sahihi lakini mitandao yote inaandika kwamba JK ndiye anayeongoza nchi kwa Sasa
Kwani ulipoambiwa tunatazama picha lakini remote control ipo Msoga ulielewaje Mkuu
 
sasa Kamugisha kilichokuuma ni kipi hasa maana umedakia kwa JK au kumtakia mabaya Mwigulu kuwa maka huu Mama Samia hatamuacha nakuapia ndoto zako za Kisukuma Gang mkafie mbele huko
Magufuli kwa taarifa yako alimtumbua Mwigulu kwa ajili ya Maaskofu wa KKKT walipomrekebisha Magufuli ndio maana akasema Magufuli hata km hajaona rafu mpirani akiambiwa kitu asikokijua anatoa Red kadi, kweli Magufuli hakuwa Refarii mzuri kabisa
Kikwete mwache atutawale tena kupitia Mama Suluhu kwani hakuwa na Red kadi ila za njano tu
Miaka hii mi5 mtaumia sana na Mwigulu tunamuombea amalize na achkue mitano mingine BAJETI NZURI sana
Kuna ile red card moja ilisababisha kifo cha yule mkurugenzi mmoja.

Kuna yale manyanyaso ya Makonda akifanya mikutano na waliokuwa chini yake.
 
mh, ila yanayomkuta JK kikwete nina hakika hata Nyerere hakuwahi kuyakabili......jamaa anaandamwa sana aisee;

wakati wa utawala wake chadema walihakikisha hafanikiwi kwa lolote, kiubishi ubishi sana akapenya!

anaandamwa kuwa eti alimsaliti lowassa.....yet, hakuna mwenye kuujua undani hadi sasa.

wakati wa utawala wa mwendazake, aliandamwa mno kwa kukosolewa kuwa hakufanya chochote wakati wa utawala wake na hata kunyamazishwa 'kibabe' mbele ya kamera pale aliojaribu kutoa maoni, hilo lilifanywa na mwendazake mwenyewe na 'washikadau' wake.

sasa hivi (wakati huu wa awamu hii ya sita), anaandamwa kwa kila hatua anayoichukua mama.....kwamba eti ndiye anayeongoza nchi sasa. kama hilo halitoshi, anaambiwa kuwa anahusika na kuondoka kwa mwendazake. kivipi? hakuna mwenye jibu.

Mungu ni mkubwa, na mapito haya pia yatapita......pole sana JK Kikwete, tunapokuona na tabasamu lako pamoja na yote haya, hakika wewe ni jasiri sana!!
Waache wachonge midomo hao.Wanamangamanga tu.
 
Nimemsikiliza Mhe. Mwigulu Nchemba akimwagia sifa za umairi Jakaya Mrisho Kikwete, nimeshangazwa sana na kitendo hiki kwa sababu zifuatazo;
Mwiguli alikuwa anawasilisha hotuba ya bajeti ambayo kimsingi haina hoja mahususi inayolazimisha kumtaja JK, Magu Wala Mkapa. Ni Nini kimemsukuma kuweka paragraph hii kwenye hotuba yake? Anamsuta Nani?
Hata Kama JK alikuwa kiongozi, Magufulu pia alikuwa kiongozi. Unapotoa sifa za kiongozi ambazo hazishabiani na kiongozi asiyekuwepo Duniani huku huko nyuma hukuwahi kutoa sifa Kama hizo kwake nikuutangazia umma kwamba huna na ujawahi kuwa na heshima kwake Bali ulikuwa unatafuta madaraka.
Lakini pia kumtaja JK kwa kumuunganisha na Mama Samia kunaleta picha kwamba bila JK uamini Kama Rais aliyepo anaweza kuongoza nchi. Naweza nisiwe sahihi lakini mitandao yote inaandika kwamba JK ndiye anayeongoza nchi kwa Sasa, Waziri wa fedha na timu yako kitendo chakuibgiza sifa za JK nikumdhalilisha Rais kwa kuonyesha umma kwamba wanayosema wanaharakati na watu wengine ni sahihi.
Lakini pia napata mashaka na uwezo binafsi wa mtu huyu katika nafasi hii nyeti, Wizara ya fedha ni nyeti. Aina ya bajeti aliyowasilisha inahitaji elimu kubwa kwa umma iweze kuonekana kwamba ina malengo chanya na kuepusha upotoshaji wakimantiki unaoweza kufanywa na watu wasio serikalini. Kuwasilisha bajeti Kama hii huku ukiweka sifa za JK kumeligawa Taifa na chama pia. Watu wengi wameondoka kuijadili bajeti wamejadili udhalimu na unafiki wakimfumo unaofanywa na wanasiasa kuwasaidia kuendelea kuteuliwa. Madhara yake ni kwamba upotoshaji utakuwa mwingi nakupunguza imani ya wananchi kwa serikali.

Utavuna ulichopanda, na naamini au natabiri hii itakuwa bajeti yako ya mwisho Kama Waziri wa fedha. Soon utajionea labda kama hawataona damage yako kwa macho ya Tanzania mpya
Tawilee!
 
Kimsingi alitakiwa ajikite zaidi kwenye suala la bajeti na mustakabali wake kwa ukuaji uchumi na maendeleo ya inch kwa ujumla. Kuingiza mambo mengine kama ulivyo eleza kumetia dosari taswira ya hotuba nzima ya bajeti.
 
Yaani hadi aibu. Ametumia muda mwingi kusifia tu. Kwa ubadhirifu wa pesa za umma uliyokuwa wizara yake sijui ndo alikuwa anajipendekeza apewe yellow card. Shame on you Mr. Minister.
Aaaargh, yaani mapambio yalianza mara baada ya Kipyenga cha mchezo kuwasahaulisha pesa iliyochotwa hazina, kulingana na maelezo ya PM wiki iliyopita... kaazi kwelikweli...
 
Nawaonya wote mnasema jk ni mshauri wa mama, ushauri upokelewa toka kokote na kwa watu unaowaamini, swala la kuufanyia kazi ndio lipo juu yake, hivyo si dhambi kuomba ushauri, ila mnatia chumvi mno na mnamfanya kama taasisi ya Urais haina majukumu wakati si kweli, najuwa lengo lenu sio zuri, pamoja na yote mnataka kuwagombanisha, bila sababu, acheni kauli hizi!
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Nimemsikiliza Mhe. Mwigulu Nchemba akimwagia sifa za umairi Jakaya Mrisho Kikwete, nimeshangazwa sana na kitendo hiki kwa sababu zifuatazo;
Mwiguli alikuwa anawasilisha hotuba ya bajeti ambayo kimsingi haina hoja mahususi inayolazimisha kumtaja JK, Magu Wala Mkapa. Ni Nini kimemsukuma kuweka paragraph hii kwenye hotuba yake? Anamsuta Nani?
Hata Kama JK alikuwa kiongozi, Magufulu pia alikuwa kiongozi. Unapotoa sifa za kiongozi ambazo hazishabiani na kiongozi asiyekuwepo Duniani huku huko nyuma hukuwahi kutoa sifa Kama hizo kwake nikuutangazia umma kwamba huna na ujawahi kuwa na heshima kwake Bali ulikuwa unatafuta madaraka.
Lakini pia kumtaja JK kwa kumuunganisha na Mama Samia kunaleta picha kwamba bila JK uamini Kama Rais aliyepo anaweza kuongoza nchi. Naweza nisiwe sahihi lakini mitandao yote inaandika kwamba JK ndiye anayeongoza nchi kwa Sasa, Waziri wa fedha na timu yako kitendo chakuibgiza sifa za JK nikumdhalilisha Rais kwa kuonyesha umma kwamba wanayosema wanaharakati na watu wengine ni sahihi.
Lakini pia napata mashaka na uwezo binafsi wa mtu huyu katika nafasi hii nyeti, Wizara ya fedha ni nyeti. Aina ya bajeti aliyowasilisha inahitaji elimu kubwa kwa umma iweze kuonekana kwamba ina malengo chanya na kuepusha upotoshaji wakimantiki unaoweza kufanywa na watu wasio serikalini. Kuwasilisha bajeti Kama hii huku ukiweka sifa za JK kumeligawa Taifa na chama pia. Watu wengi wameondoka kuijadili bajeti wamejadili udhalimu na unafiki wakimfumo unaofanywa na wanasiasa kuwasaidia kuendelea kuteuliwa. Madhara yake ni kwamba upotoshaji utakuwa mwingi nakupunguza imani ya wananchi kwa serikali.

Utavuna ulichopanda, na naamini au natabiri hii itakuwa bajeti yako ya mwisho Kama Waziri wa fedha. Soon utajionea labda kama hawataona damage yako kwa macho ya Tanzania mpya
Lakini si kamsifia na mwendazake.binafsi najua mwiguli anafit kwa nafasi,hizo zingine alikuwa anapiga vijembe kama yanga timu bora
 
Kikwete aliharibu sana nchi hii kuanzia 2005 na ndiyo maana effort zozote za kuinyoosha tena kurudi kwenye njia iliyoachwa na Mkapa zimekuwa ni ngumu kwa sababu raia walishapinda mno kwa kusihi kwa njia za mkatomkato tu. Kuinyoosha nchi iliyoachwa na kikwete kunahitaji nyundo nzito sana na pia nchi yenyewe ipashwe moto mkali kabla ya kuanza kunyooshwa; Magufuli alikuwa kaanza kidogo lakini sasa tunarudi kule kule pole pole
1625774606837.png
 
Kuhusu kumsifia JK sijui kafanya hivyo kwenye mazingira yapi kama yalimlazimu kufanya hivyo.

Lakini kwa tabia za kujipendekeza za hao jamaa sitashangaa kama amefanya hivyo kwa lengo maalum akijua fika JK kwa sasa ndie remote ya ikulu yetu, na yeye Mwigulu hastahili kuwepo kwenye hiyo wizara hasa baada ya ile kashfa ya kupotea bilioni tatu kwenye wizara yake.
Anautamani sana urais na anajua Jk ana ushawishi kwenye vikao muhimu.
 
Back
Top Bottom