Mwigulu Nchemba kuongoza Wizara ya fedha ni pigo kubwa kwa Wafanyabiashara na Walipa kodi

Mwigulu Nchemba kuongoza Wizara ya fedha ni pigo kubwa kwa Wafanyabiashara na Walipa kodi

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Wakuu naomba kutangaza kwamba ninayo maslahi kwenye suala hili maana mimi ni mfanyabiashara wa ndani na nje ya nchi , ni mlipa kodi

Kwa takribani miaka sita sasa Sisi wafanyabiashara wa nchi hii tunahenya , makadirio ya kodi kubwa , vitendea kazi tunavyoagiza kutoka nje ya nchi zikiwemo matirio za kutengenzea bidhaa kodi tunayotwangwa kwenye bandari ya Dar es Salaam haina urafiki wowote ule , kwa ujumla Wafanyabiashara wakubwa kwa wadogo ambao ndio walipa kodi wa kutegemewa kwenye nchi hii Wamegeuzwa kuwa maadui , hakuna asiyeelewa hiki ninachoandika hapa , hela zetu zimeng'olewa kwenye akaunti za benki bila hata maelezo yoyote .

Kwa mtu katiri na mwenye mihemko na visasi kama Mwigulu kupewa Wizara hii ni pigo kubwa kwa wafanyabiashara , wenye viwanda , wazalishaji na wasambazaji wa bidhaa nchini , kuna hatari ya vyuma kukaza zaidi .

Wizara hii muhimu ilihitaji Waziri msikivu asiyejikweza kwa kiburi cha madaraka , inahitaji waziri atakayekaa na wafanyabiashara na anayeamini katika majadiliano , ingekuwa vema Waziri wa fedha atokane na Walipa kodi wanaofahamu ugumu na umuhimu wa kulipa kodi , huyu Mwigulu hajui lolote kuhusu mambo haya , ataleta shida zaidi .

Itaendelea ........
 
Vipi ule waraka wa chadema kuwa raisi anatakiwa kuvunja Baraza? Katibu aliwaingiza Chaka?
Acha kubeza. Corona bado ipo. Tutaendelae na maombi yetu kisha Mungu wetu atasikia kilio chetu.

Dr. Bashiru hajalamba hata mshahara wa mwezi mmoja kwa nafasi yake ya Katibu Mkuu Kiongozi. Mwigulu yeye ni nani Mungu asitende kazi yake??
 
Back
Top Bottom