Uchaguzi 2020 Mwigulu Nchemba: Rais wetu ni Magufuli, waambieni waliowatuma enyi wenye tamaa ya Madaraka

Uchaguzi 2020 Mwigulu Nchemba: Rais wetu ni Magufuli, waambieni waliowatuma enyi wenye tamaa ya Madaraka

Mbona unayemjibu kaeleweka kwa umma. Anamaanisha nini kuhusu Tume huru. Kipindi cha nyuma maded walikuwa na Uhuru kiasi. Sijui kama unatambua kuwa hao maded ni sehemu ya Tume ya uchaguzi.

Uchaguzi wa serikali za mitaa chini ya hao maded uliharibika. Kipindi cha nyuma haukuwahi najisiwa hivi. Hiyo inatosha kusema kuna haja ya kuurekebisha huu muundo ulionajisiwa ili kuwa huru.
 
Jitu Kama Mwigulu Nchemba ATI Daktari(sijajua ni daktari wa nn)linafikri MAGUFULI atakuwa Rais wa MAISHA na si ajabu ndo kundi la kina Kessy, Ngamia na Ayubu wanaopiga debe Magufuli AONGEZEWE MUDA wa Urahisi mpaka 2040 watakaporudi Bungeni Nov, 2020!! Yajayo ni kichefuchefu!
Nivile wameshajua silaha yakuteuliwa ni kusifia mtawala wao tu!
 
Na kweli wametumwa hao. Sasa watambue kuwa wembe ni uleule uliowanyoa kwenye kueneza taarifa za uongo kuhusu corona, ndio utakaowanyoa oktoba 2020.
 
Mkuu unadhani hapa wanaokomolewa ni CHADEMA?
Tukiharibu kwenye uchaguzi na kupata Viongozi wabovu maumivu hayatakuwa ya CHADEMA,yatakuwa kwa wananchi wote...

Tujikumbushe kwa uchache tu...
Maamuzi mabovu yaliyofanywa kwenye zao la korosho,wanamtwara na Lindi watwambie,waliokuwa CCM waliuza kwa bei kubwa zaidi ya wale wa CUF,ACT NA CHADEMA?

Watumishi wa umma waliochagua CCM wameongezewa mishahara yao kwa miaka 5 ukilinganisha na wale waliochagua UKAWA?

Mawazo Kama ya kwako,(kudhani kwamba kudai haki ni kazi ya kundi fulani),ni hafifu sana, kwani madhara ya kutokuwepo kwa haki hiyo hata wewe yatakupata
Sema ACT Wazalendo Chadema imeshakufa
 
Mbona unayemjibu kaeleweka kwa umma. Anamaanisha nini kuhusu Tume huru. Kipindi cha nyuma maded walikuwa na Uhuru kiasi. Sijui kama unatambua kuwa hao maded ni sehemu ya Tume ya uchaguzi.
Uchaguzi wa serikali za mitaa chini ya hao maded uliharibika. Kipindi cha nyuma haukuwahi najisiwa hivi. Hiyo inatosha kusema kuna haja ya kuurekebisha huu muundo ulionajisiwa ili kuwa huru.
Uchaguzi wa serikali za mitaa uliharibika kutokana na Ujinga wa wapinzani. Kwani walipewa maelekezo kutoka kwa wafadhili wao kuwa wasusie uchaguzi ili endapo Nchi itaingia katika machafuko, uchaguzi Mkuu usiweze kufanyika. Kubalini kuwa hamna hoja na sera za kuwaeleza Watanzania.
 
Ni haki yako kutoa maoni sawa na uonavyo. Hongera kwa hilo.

Lakini pia ni haki ya wengine kuwa na mtazamo tofauti na kile unachoamini wewe.

Ukisema tuna tume huru wengine watakuuliza uchaguzi wa serikali za mitaa ulikuwa huru?

Ukidai vyombo au washirika wa nje wasiiingilie mambo ya nchi yetu wengine wenye mtazamo tofauti na wewe watakuuliza kuwa kuna matukio ya watu kupotea ama kuuawa kutokana na itikadi za kisiasa, je usalama wa mazingira ya leo ama kesho wayajua?

Niseme wazi nakushangaa sana tena sana jinsi ulivyojivika upofu kama vile hujawahi kuwa waziri wa mambo ya ndani ama kuwa mshirika wa haya mambo.

Pole sana. Huenda walioumizwa wasiweze kuchukua hatua yeyote ile, ila KUMBUKA karma is real, nayo yaja upesi sana.

Kesho ni fumbo, vilevile October ni fumbo pia.


Naipenda Tanzania, naiombea amani Tanzania.

Mola tunusuru na wasaka tonge walio wazuri kutetea maslahi binafsi kuliko maslahi mapana ya nchi.


#Fitina kwangu ni mwiko, nitasema kweli daima. (Ahadi #8 TANU)
Mwambie hata Gambo alijiona mfalme ssa tuko nae mtaani
 
"Kumi Mwigulu Yatosha" nasikia hii ndiyo kampeni iliyopo Iramba Magharibi, Mwigulu anapumulia mashine! Lazima ujikombe kwa jiwe ili angalau upenye kwa vitu maalum!
 
NCHI YETU HATUJAWAHI KUFANYA UCHAGUZI BILA TUME HURU YA UCHAGUZI.
Mkuu Mhe. Mwigulu Nchemba, asante sana kulizungumzia hili la Tume huru ya uchaguzi.

Tupo pia tuliolizungumza sana lakini Watanzania wanahitaji kuelimishwa kikamilifu kuhusu hili ili lieleweke vizuri, na hata Watanzania wenyewe kwa ridhaa zao na kwa ujumla wao, kwenye uchaguzi wa October, waki amua kuichagua CCM tuu and only CCM katika uchaguzi Mkuu huru na wa haki na bila waangalizi wowote kutoka nje, hivyo CCM ndio pekee ikachaguliwa naomba tuu watuelewe.

Hili la Tume huru tumelijadili sana humu

Kuna swali hujalijibu ila pia you are free kutoyajibu depending on how busy you are.
P
 
Ifike wakati Wazungu waweke limits za education awards kwa Waafrika, sure.
Hivi Doctor anaandika vitu kama hivi kweli?
Huu Doctor wa Madelu kaupata toka Chuo gani? Itakuwa Udaktari uleule wa Mteuzi wake Mr. Jiwe aliyeghushi Udaktari wake na kina Ben Saanane walipohoji wakapelekewa Chatu.....!!!
 
Iko siku Mwigulu nae atakuja humu kulilia tume huru.

Wazungu Wana msemo, " what goes around comes around"! Mwigulu anajiona yuko salama Sana ndani ya Utawala wa Jiwe.....yaani jamaa kesha sahau kuwa Kuna kipindi Jiwe alimtumbua kwenye nafasi ya Uwaziri Internal Affairs!
 
Huu Doctor wa Madelu kaupata toka Chuo gani? Itakuwa Udaktari uleule wa Mteuzi wake Mr. Jiwe aliyeghushi Udaktari wake na kina Ben Saanane walipohoji wakapelekewa Chatu.....!!!
Mambo ya hovyo sana.
Aibu imfikie mtoa post.
Cheo chake ni kikubwa tofauti na maandishi yake
 
Akiwa waziri wa mambo ya ndani huyu kulikua na utekaji mwingi sanaaa. Wakati huo Tundu lisu alipigwa risasi mchana, Azory na Ben saanane walipotezwa , watu wengi sana walitekwa na kuumizwa. Huyo jamaa ni shetani zaidi ya shetani mwenyewe.
 
Dah, Mwigulu anatafuta njia Kitila atafutiwe namna nyingine, akina Mwigulu wameshajua kula na kipofu.

Elimu sio vyeti maanake hata Bashite anavyo vyeti vya Makonda, elimu ni kichwa.

Akina Mwigulu ndio wanaoshikilia portfolio nyeti kama ya sheria halafu mtu anasubiri atapata haki chini ya serikali anayoitumikia...!!

We better tell Mwigulu that "We Can't Breath".
 
Mkuu Mwigulu Nchemba, asante kwa hoja hii, naunga mkono hoja, Tume ya Uchaguzi ni Tume huru
Pascal Mayalla: NEC ni Tume huru ya uchaguzi kama lilivyo bunge na mahakama kwa sababu vyote hivi msingi wake ni Rais

Ila naomba siku ukipata muda au nafasi, urejee kwenye bandiko lako hili,
Ana kwa ana na Mwigulu Nchemba: Kuelekea Uchaguzi Mkuu 2020
Kuna swali hujalijibu ila pia you are free kutoyajibu.

P

Mhe. P,
Sifa moja ya Wasukuma ni unafiki, umbeya na kujikomba kwa Sana!
Hivi kwa akili yako ukiwa tena mwana Habari(by profession) unathubutu kusema Tanzania na TUME HURU? Really? You must be joking seriously!
Yaani NEC iliyojaa wateule wa Mhe. Rais wa CCM, kuanzia Mwenyekiti, Mkurugenzi na Wasimamizi wote( Wakurugenzi wa Halmshauri na Majiji ) halafu useme hiyo Ni NEC HURU?
Je, unaweza kuilinganisha Tume ya Uchaguzi Tanzania (NEC) na Tume Huru ya Uchaguzi Kenya(IEBC) na utuambie hapa kama ziko sawa?
 
Back
Top Bottom