Labda, kwenye store za dhahabu wataweka malaika maana unaweza kununua dhahabu nzuri alafu baada ya mwezi moja ukienda kukagua dhahabu zile store unakuta zilizoko ni feki. Yani hili jambo hili linahitaji umakini wa kina.Kwa mujibu wa mwingulu, bot itaanza kununua DHAHABU na kuziweka kama akiba, ikumbukwe kwamba kwa mataifa mengine , ni jambo lililoanza zamani. Hata hivyo kwa Tanzania wazo lilitolewa na JPM ambapo alianza kwa kuanzisha maduka ya DHAHABU.
walishatumia madude yote ya laiserSwali langu:
1. Hadi sasa hatuna akiba ya GOLD?
2. TANZANITE iliyonunuliwa na JPM ipo au imeuzwa?
Mpango mzuri. Jamaa huwa wanakuza gharama za uendeshaji ili baadaye faida ionekane ndogo na wewe wanakupa gawio kiduchu. Mkilipana mawe watajitahidi kubana hayo matumizi feki. Maana itakula kwao.Nchi ya Botswana imepata jibu kuwa mfano Tanzania mkataba wa mgodi na mwekezaji wagawane vitofali vya dhahabu na serikali badala ya kusubiri faida ya kwenye balance sheet.
Mgawanyo wa vitofali au almasi au tanzanite inaipa uhuru Tanzania kuhifadhi kitu halisi na kukiuza kwa thamani ya uhakika bila makando kando ya kusubiri mwekezaji asafirishe madini yote nje na mwisho wa siku akuambie faida ni ndogo kama ripoti yake ya katika mahesabu ya mwaka yanavyoonesha .
1 July 2023
Gaborone, Botswana,
Botswana na De Beers Zasaini Mkataba wa Kuendeleza Ushirikiano Tajiri wa Almasi
Chini ya makubaliano mapya ya uchimbaji madini, Botswana itapata mara moja asilimia 30 ya mawe machafu yaliyochimbwa, kutoka asilimia 25, na itapanda hadi asilimia 50 ndani ya muongo mmoja, De Beers na maafisa wa serikali walisema.
Afisa wa serikali ya Botswana na mtendaji mkuu wa De Beers, muungano wa kimataifa wa almasi, walitia saini mikataba ya muda siku ya Jumamosi ili kuendeleza ubia wenye faida, wa miongo kadhaa wa uchimbaji madini ya almasi ambao ulionekana kuvunjika katika miezi ya hivi karibuni.
Dakika chache kabla ya tarehe ya mwisho ya usiku wa manane siku ya Ijumaa, pande zote zilitangaza kwamba baada ya mazungumzo ya miaka mingi, walikuwa wamekubaliana kimsingi juu ya mpango wa kuunda upya ushirikiano ambao unaipatia De Beers sehemu kubwa ya almasi yake na serikali ya Botswana sehemu kubwa zaidi ya mapato yake.
Maelezo ya mpango huo bado yanashughulikiwa, maafisa wa serikali na De Beers walisema. Lakini inashughulikia moja ya matatizo makubwa ya serikali ya Botswana, kuhusu mgao wa almasi ambayo inapokea katika ubia wake wa uchimbaji madini na De Beers.
Chini ya makubaliano ya zamani, Botswana ilipokea asilimia 25 ya mawe machafu yaliyochimbwa, huku De Beers ilichukua mengine. Sasa, Botswana itapata mgao wa asilimia 30 mara moja, na hiyo itapanda hadi asilimia 50 ndani ya muongo mmoja, De Beers na maafisa wa serikali walisema.
De Beers alisema katika taarifa yake kwamba imekubali kuwekeza kiasi cha dola milioni 825 katika kipindi cha miaka 10 ijayo kusaidia kuendeleza uchumi wa Botswana. Makubaliano hayo pia yanajumuisha kuanzisha chuo nchini Botswana ambacho kitafundisha wenyeji ujuzi katika biashara ya almasi, maafisa wa serikali walisema
Source : The New York Times
kuchukua percent ya mawe kwa wachimba vito wote.
Sasa kwani kuna ubaya yeye na Samia si walikuwa wanaongoza serikali moja na sasa hayupo ila mama ndio raisi tena mwema kabisa anaendeleza yale mazuri na kuongezea na yake mazuri na pia ni vizuri kukumbushia yaani wote ni win win tuNa hiyo ndo lilikuwa wazo last JPM navona mnanza kumwelewa sasa
Swali kuu kutoka nchini Ghana kuhusu utaratibu wa kununua dhahabu na nani anamilki migodi je serikali itajikita kununua toka kwa wachimbaji wadogo kwa bei ya kimataifa?
MJADALA WA BIASHARA YA DHAHABU KWA MAFUTA WAPAMBA MOTO NCHINI 🇬🇭
Mjumbe wa kamati ya migodi na nishati ya Bunge nchini Ghana, Dr. Kwabena Donkor amesema hizi ni sarakasi zinazochezwa na serikali ambazo ni kiini macho kwani haziwezi kutekelezeka.
Kujaribu biashara ya mali-kwa-mali (barter trade) ya kubadilisha dhahabu kwa mafuta ya petroli / dizeli kimataifa ni dalili ya serikali kushindwa kusimamia uchumi anasisitiza mbunge na mjumbe huyo wa kamati ya bunge Dr. Kwabena Donkor ambaye aliwahi kufanya kazi ktk sekta ya petroli.
Dr. Kwabena Donkor akishiriki ndani ya mjadala exclusive wa kituo cha JoyNews amekwenda ndani zaidi kwa kuhoji ni nani anayemiliki migodi hiyo, na inajulikana ni makampuni makubwa ya kigeni hivyo watawalipa nini wenye migodi je ni kwa pesa za madafu yaani sarafu ya cedis ya Ghana au dollars za Kimarekani ambazo serikali ya Ghana haina fedha hizo za kigeni.
Anaongeza hoja Dr. Kwabena Donkor, pia kama serikali italenga kununua kwa wachimbaji wadogo wadogo itaweza kushindana na bei ya dhahabu ya soko la dunia? Maana itapelekea wachimbaji hao wadogo kutorosha dhahabu kupitia njia za panya za mipakani.
Hii ni kutokana na serikali itashindwa kuwalipa bei nzuri wachimbaji wadogo au kuwalipa kwa dollar za marekani wachimbaji wadogo kulingana na bei ya soko la dunia kwani serikali haina hifadhi ya kutosha ya fedha za kigeni.
Kimsingi katika mada hii moto ya kituo cha TV JoyNews pia mtendaji mkuu (CEO) wa chemba ya migodi ya Ghana, Dr. Sulemanu Koney naye ktk mahojiano ametoa kauli juu ya changamoto ya jinsi ya uhalisia wa uwezekano wa sera hiyo mpya ya biashara ya mali-kwa-mali kuweza kutekelezeka, kwani kuna mengi ya kuyafanya kabla ya sera hiyo kuweza kutekelezeka ingawa chemba hiyo milango yake ipo wazi kwa majadiliano na serikali ya Ghana.
Source : JoyNews
Swali kuu kutoka nchini Ghana kuhusu utaratibu wa kununua dhahabu na nani anamilki migodi je serikali itajikita kununua toka kwa wachimbaji wadogo kwa bei ya kimataifa?
Wosia kwa Mwigulu
Kukosa uhakika ni, kweli, na ndiyo kesho yako . Nani anajua nini kitatokea? Lakini kutokuwa na uhakika pia ni wakati uliopita? nani anajua kilichotokea - Antonio Machado
Sitaki kuponda. Ila ukweli tumechelewa sana. Na hatujuwi tuna dhahabu kiasi gani mpaka Sasa...Waziri Mwigulu Nchemba amesema kuwa Serikali imekamilisha taratibu za kununua dhahabu kupitia Benki Kuu ya Tanzania kwa ajili ya kuanzisha akiba ya dhahabu hapa nchini.
Pia soma Tanzania tuhifadhi akiba yetu kwa Dhahabu badala ya Dollar
“Kutokana na kukamilika kwa ujenzi wa viwanda vya kusafishia dhahabu, Serikali itaendelea kuweka vivutio kwa viwanda hivyo ili vipate malighafi ya kutosha na ili kukamilisha hilo Serikali imepunguza mrahaba wa madini yanayouzwa kwenye viwanda hivyo kutoka 6% hadi 4%”
“Nafurahi kulijulisha Bunge kuwa Serikali Serikali imekamilisha taratibu za kununua Dhahabu kupitia Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwa ajili ya kuanzisha akiba ya dhahabu hapa nchini (Gold Reserve)"
“Tunataka tunapotaja akiba ta fedha za kigeni tutaje na akiba ya dhahabu tuliyonayo, hatua hii itawapatia Wachimbaji bei nzuri na kuimarisha sarafu ya Nchi yetu, hii ni baada ya kupokea maelekezo ya Mh.Dkt. Samia na michango ya Waheshimiwa Wabunge”