Mwigulu Nchemba: Tanzania ni mfano mzuri wa kuigwa duniani kwa huduma bora za barabara, maji na umeme

Mwigulu Nchemba: Tanzania ni mfano mzuri wa kuigwa duniani kwa huduma bora za barabara, maji na umeme

Kama barabara zetu ni bora why wao wanakimbizana na V8 kwenye barabara zilizo bora?,watanzania ni mazuzu
 
Mwigulu hafai kuwa kiongozi wa hii nchi,hajui kabisa shida za watanzania yeye anavyoserereka na life basi wote tuko ndio kila siku idea zake kumuongezea hali ngumu ya maisha m TZ kwa kumuwekea mitozo kila sehemu
 
Hii ni kauli ya Serikali kupitia kwa Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba.

----
Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Tanzania imekuwa ikichukuliwa kama nchi ya mfano Duniani ukilinganisha na mataifa mengine Barani Afrika kutokana na hatua kubwa na ya haraka iliyopiga kwenye sekta mbalimbali kama vile afya, nishati hususani umeme, maji na elimu suala ambalo linaashiria kufikiwa viashiria vya malengo iliyojiwekea

Dkt. Nchemba amesema hayo leo, Jumanne Machi 12.2024 wakati wa hafla ya kuweka jiwe la msingi jengo la Taaluma la chuo cha Uhasibu Arusha (Kampasi ya Dodoma) linalojengwa kwenye eneo la Njedengwa, jijini Dodoma ambapo amesema tatizo kubwa linalotukabili hapa nchini ni suala la kujidharau wenyewe kwa vile tunavyofanya, lakini uhalisia ni kwamba Tanzania imekuwa ikichukuliwa kama mfano wa kuigwa miongoni mwa mataifa mengi Barani Afrika

Amesema hadi kufikia sasa asilimia kubwa ya maeneo ya nchi yameunganishwa kwa Barabara za lami, huku ajenda ya umeme sasa inajadiliwa kufikishwa kwenye ngazi za vitongoji na mtu mmoja mmoja, uwepo wa vituo vya afya kwenye kila tarafa, na suala la serikali kubeba gharama za elimu kuanzia ngazi ya awali hadi elimu ya juu ni ushahidi tosha wa kauli yake kwa kuwa bajeti ya elimu ya juu pekee inakaribia trilioni moja kila mwaka

Akizungumzia zoezi la uwasilishwaji wa mpango wa maendeleo ya Taifa na ukomo wa bajeti kwa mwaka ujao wa fedha wa 2024/25 Waziri Dkt. Nchemba amebainisha kuwa katika bajeti hiyo inayofikia trillioni 49 vipaumbele mbalimbali vimezingatiwa ambapo kati ya fedha hizo fedha za maendeleo ni trillioni 16, bajeti kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya mataifa huru ya Afrika (AFCON) inayotarajiwa kufanyika 2027 hapa nchini kwa ushirikiano wa Kenya na Uganda imetengwa shilingi bilioni 200, uchaguzi mkuu wa mwakani (2025) shilingi bilioni 600, wakati uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka huu (2024) ukiwekewa bilioni 300, sambamba na hilo amesema deni halisi la Taifa nje ya riba ni trilioni tano (5) lakini hata ukiweka na riba deni hilo halizidi trilioni 10 ambapo deni hilo linatokana na miradi mikubwa ikiwemo ujenzi wa reli, vivuko ikiwemo kivuko kikubwa cha Kigongo - Busisi, ujenzi wa vyuo vikuu, mabweni nk

Chanzo: Jambo Tv
Tatizo letu tunafurahia Sana uwingi wa vitu pasipo kuangalia ubora wa vitu hivyo. Ni kweli tunazo barabara za lami zinazounganisha sehemu mbalimbali za nchi, lakini je hizo barabara zina ubora unaotakiwa. Nyingi zilijengwa muda mrefu na kwa sasa ni choka mbaya zinahitaji matengenezo. Hatuna utamaduni wa kufanya ukarabati wa miundombinu yetu. Matokeo yake hizi barabara tunazojidai nazo zimejaa mashimo na sehemu nyingine ni mahandaki kabisa.
 
Back
Top Bottom