Sildenafil Citrate
JF-Expert Member
- Jan 29, 2021
- 577
- 2,595
Waziri wa fedha Mhe. Mwigulu Nchemba amesema Serikali imesikia kilio na malalamiko ya wananchi wake kuhusu vipengele kadhaa vinavyohusiana na tozo.
Mfano wa mapendekezo hayo ni uwepo wa makato mara mbili kwenye miamala ya simu wakati wa kutuma na kutoa. Kupitia mkutano wake na waandishi wa habari amesisitiza kuwa muda si mrefu hatua stahiki zitachukuliwa.
Kuhusu tozo za benki, serikali itakaa na watoa huduma hiyo ili kujadiliana tena kwa mara nyingine.
Kuhusu kodi ya pango, waziri amebainisha kuwa mpangaji siyo mdaiwa bali yule mwenye nyumba hivyo haitawahusu wao. Hata hivyo ili kuondoa mgogoro kati ya wapangaji na mwenye nyumba, serikali itazingatia maoni ya watu waliopendekeza kuwaondoa wapangaji kwenye kadhia hii ili serikali idai moja kwa moja kwa wamiliki wa nyumba.
Waziri amekiri kuwa lengo la kodi hii (ya pango) ni zuri lakini kulikuwa na upungufu kwenye mkakati wa ukusanyaji wake hivyo wao kama serikali watajitathimini kuona wanafanyaje.