Mwigulu: Rais aelekeza fedha za Muungano zikarabati miundombinu

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Rais, Samia Suluhu ameelekeza fedha zilizokuwa zimepangwa kugharamia maadhimisho ya Sherehe za Muungano mwaka huu, zitumike kukarabati miundombinu ya barabara iliyoharibiwa na mvua zinazoendelea kunyesha nchini.

1776683104818.png
Ameyasema hayo, Jumatatu, Aprili 20, 2026 Ofisini kwake Mlimwa jijini Dodoma alipokuwa akiuarifu umma kuhusu maadhimisho ya Miaka 62 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yatakavyofanyika.

“Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 62 ya Muungano yatafanyika katika ngazi ya Mikoa yote nchini ambapo Viongozi Wakuu wa Kitaifa watafanya shughuli za kutembelea, kuweka mawe ya msingi na kuzindua miradi ya maendeleo,” Amesema Dkt. Mwigulu.

Aidha, Dkt. Mwigulu amesema imeelekezwa kuwa Wakuu wa Mikoa watembelee, waweke Mawe ya Msingi na kuzindua miradi ya maendeleo pamoja na kushiriki shughuli za usafi wa mazingira, kupanda miti na kufanya mashindano ya michezo mbalimbali.

Shughuli nyingine zitakazoambatana na Maadhimisho haya ni Pamoja na mashindano ya michezo na sanaa mbalimbali; mashindano ya uandishi wa insha kwa shule za msingi na sekondari; mahojiano maalum na wazee maarufu; midahalo na makongamano kuhusu muungano na hatua ya maendeleo iliyofikiwa hadi sasa.

Kaulimbiu ya maadhimisho hayo ni: “MIAKA 62 YA MUUNGANO: AMANI, UMOJA NA MSHIKAMANO NI MSINGI WA MAENDELEO ENDELEVU.”

​
 
Siku ya muungano ilipaswa kuangukia Jumatatu.
Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Rais Samia Suluhu Hassan ameelekeza fedha zilizotenga kugharamia maadhimisho ya Miaka 62 ya Muungano wa Tanzania zitumike kukarabati miundombinu.
 
Hizi siasa za kipumbavu! Ziliasisisiwa na Magufuli,

Mnakuwa mnajua sherehe hazitafanyika, mnajifanya kutenga fedha, ili mfanye siasa kuwa raisi kaziruhusu zifanye kitu fulani

Hivi wanatuonaje hawa kenge viongozi?
 
Kwahio sikuhizi tunategemea pesa za Sherehe kufanyia kazi, zile fedha zilizopangwa kwa maendeleo zinaenda wapi?
 
Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Rais, Samia Suluhu ameelekeza fedha zilizokuwa zimepangwa kugharamia maadhimisho ya Sherehe za Muungano mwaka huu, zitumike kukarabati miundombinu ya barabara iliyoharibiwa na mvua zinazoendelea kunyesha nchini.

Ameyasema hayo, Jumatatu, Aprili 20, 2026 Ofisini kwake Mlimwa jijini Dodoma alipokuwa akiuarifu umma kuhusu maadhimisho ya Miaka 62 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yatakavyofanyika.

“Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 62 ya Muungano yatafanyika katika ngazi ya Mikoa yote nchini ambapo Viongozi Wakuu wa Kitaifa watafanya shughuli za kutembelea, kuweka mawe ya msingi na kuzindua miradi ya maendeleo,” Amesema Dkt. Mwigulu.

Aidha, Dkt. Mwigulu amesema imeelekezwa kuwa Wakuu wa Mikoa watembelee, waweke Mawe ya Msingi na kuzindua miradi ya maendeleo pamoja na kushiriki shughuli za usafi wa mazingira, kupanda miti na kufanya mashindano ya michezo mbalimbali.

Shughuli nyingine zitakazoambatana na Maadhimisho haya ni Pamoja na mashindano ya michezo na sanaa mbalimbali; mashindano ya uandishi wa insha kwa shule za msingi na sekondari; mahojiano maalum na wazee maarufu; midahalo na makongamano kuhusu muungano na hatua ya maendeleo iliyofikiwa hadi sasa.

Kaulimbiu ya maadhimisho hayo ni: “MIAKA 62 YA MUUNGANO: AMANI, UMOJA NA MSHIKAMANO NI MSINGI WA MAENDELEO ENDELEVU.”

Rais yupi?
 
FEDHA ZA MUUNGANO ZITUMIKE KUKARABATI MIUNDOMBINU YA BARABARA

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ameelekeza fedha zilizokuwa zimepangwa kugharamia maadhimisho ya Sherehe za Muungano mwaka huu, zitumike kukarabati miundombinu ya barabara iliyoharibiwa na mvua zinazoendelea kunyesha nchini.

Ameyasema hayo, Jumatatu, Aprili 20, 2026 Ofisini kwake Mlimwa Jijini Dodoma alipokuwa akiuarifu umma kuhusu maadhimisho ya Miaka 62 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yatakavyofanyika.

“Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 62 ya Muungano yatafanyika katika ngazi ya Mikoa yote nchini ambapo Viongozi Wakuu wa Kitaifa watafanya shughuli za kutembelea, kuweka mawe ya msingi na kuzindua miradi ya maendeleo” Amesema Dkt. Mwigulu.
 
Attachments

  • VID-20260421-WA0035.mp4
    13.8 MB
Hakuna mtu selfish kama Mzanzibari.
Tukakatwe kodi na TRA ili wao wakishi kwa neema ilhsli wana ZRAnya kwao
 
Back
Top Bottom