Mwigulu: Tusijifiche kwenye kichaka cha HAKI bila WAJIBU

Mwigulu: Tusijifiche kwenye kichaka cha HAKI bila WAJIBU

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Waziri Mkuu, Mwigulu Nchemba, leo Desemba 29, 2025, akiwa Bunju B jijini Dar es Salaam, amefafanua mjadala unaoendelea mitandaoni kuhusu HAKI na AMANI.

Amesema kuwa HAKI ni jambo muhimu na linatambuliwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hata hivyo haki haiwezi kutenganishwa na WAJIBU.

Ameeleza kuwa kudai haki bila kuheshimu wajibu ni kwenda kinyume na Katiba, na kusisitiza kuwa kupata haki kunahitaji pia kuheshimu sheria za nchi.

Mwigulu amewataka Watanzania kuzingatia sheria na taratibu kama msingi wa kudumisha Haki na Amani nchini.

PhD za kugawiwa, huwezi kusema TRAT AND TRAB kama source ya mapato ya taifa katika bajeti.... kama mnakumbuka kwenye bunge alipoulizwa na Tulia

These are Tax Revenue Appeals Board (TRAB) and Tax Revenue Appeals Tribunal (TRAT) are quasi-judicial institutions.
 
YOTE , TISA KUMI , TUENDELEE KUMSAPOTI MAMA WA AFRICA , RAIS WETU SAMIA SULUHU HASSAN TANZANIA KWANZA AMANI KWANZA.🇹🇿
 
Polisi waliposhindwa kuwalinda raia kwakuwa ni wajibu wao watu wakaendelea kutekwa na kuuwawa watu wakaamua kuitafuta haki. Haki itakayoilazimisha serikali kutimiza wajibu wa kuliambia jeshi la polisi kulinda raia na Mali zao. Kama mlishindwa kuwalinda raia kama wajibu wa police unavyotaka je mlitaka wananchi wakae kimya? Wasiidai haki ? Baada ya wajibu wenu kufeli? Stupid Madelu.
 
Waliouwawa kwa risasi hawakutimiza wajibu gani?
Sheria ipi ilitoa mamlaka ya kuuwa nje ya taratibu za kisheria (extra judicial killings)?
Ni madai yapi ya waandamanaji hayakuwa ya kweli?
Wale waandamanaji kutoka nchi jirani wameshtakiwa mahakama ipi?
 
Extra judicial killings zinatokea dunia nzima, nani kawapa haki ya kuua raia wasio na hatia wale waasi wa M23 kule DRC?.

Nani anawapa haki ya kuua malefu ya raia kule Sudan na Somalia?, nani anawapa mamlaka ya kuua raia wema kila siku huko USA?.

Hayakuwa maandamano, hakuna maandamano ambapo vituo vya mafuta vinatiwa moto pamoja na miundo mbinu ya mwendokasi,

Hakuna maandamano ambapo watu wanaelekea kutia moto matanki ya mafuta kule TPA.
 
Sijawahi kumuelewa huyu jamaa mwenye mouth diarrhea,preaching water while taking strong wine/alcohol,
the country is under Corrupt leaders,
Biteko was the best for this position
The man has emotional intelligence and eloquent public speaker,
 
PhD za kugawiwa, huwezi kusema TRAT AND TRAB kama source ya mapato ya taifa katika bajeti.... kama mnakumbuka kwenye bunge alipoulizwa na Tulia

These are Tax Revenue Appeals Board (TRAB) and Tax Revenue Appeals Tribunal (TRAT) are quasi-judicial institutions.
Una uhakika kuwa hyo phd aligawiwa?
Una uhakika kuwa alsema kuwa hzo ni sources of income?

Inawezekana mh mwigulu ana madhaifu yake kama binadamu lakini kwenye uchumi syo kilaza kama unavyotaka kupotosha
 
Ni kilaza! Tafuta clip ya bunge usikie alivyokuwa amebugi
Nakutafutia nikipata nitakuwekea.
Pili alisoma wapi muda wa PhD wakati akiwa waziri? Ile inakuwa full time programme...kama Maguguli alivyohoji Ben wakamuua!
Usitetee malpractice katika elimu!
Hata hotuba zake anaonekana kupwaya mno!
 
Back
Top Bottom