Mwijaku na Baba Levo wanapata utajiri kwa kujifanya wajinga, huku Wasomi wanalia njaa

Mwijaku na Baba Levo wanapata utajiri kwa kujifanya wajinga, huku Wasomi wanalia njaa

FRESHMAN

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2011
Posts
9,137
Reaction score
34,793
FACT OF LIFE. Hawa Jamaa wamejizima data vichwani lakini ndio maisha yanaenda hivyo, watukane, wakejeli, wakashfu lakini mara leo wameingia mkataba huu mara kesho ule.

Ndivyo dunia ya kibepari ilivyo sio kwamba hawana akili timamu, wanazo. Wameamua tu kuzima data. Wakati mwingine ukijifanya una akili sana maisha hayaendi maana hizi ni zama za Capitalism duniani. Watoto wao ndio watatumia akili nzuri, si wanapelekwa shule nzuri kwa sasa?

Wao Mwijaku na Baba Levo wamejifanya wamezima data kidogo maisha yaende. Kahesabu maelfu ya vijana wanaograduate kila mwaka na kukosa ajira.

Kipato cha mwijaku na baba levo kwa mwaka ni zaidi ya wasomi wengi sana Tanzania
 
Hao wasomi "wakizima data" mnaanza kuwaita wasomi uchwara. Profesa Lipumba alizima data akashambuliwa, Dr Slaa nae alizima data akashambuliwa juzi kati hapa Profesa mmoja alizima data na kutoa ripoti mchongo ya maji ya mto Mara hakukukalika, wapumzisheni basi hao wasomi wakizima data Mwijaku na Baba Levo yatosha!
 
Nchi inahitaji zaidi wataalam
Madokta,walimu,manesi, wanasheria,mainjinia, mafundi,wajasiriamali,wakulima
Etc..
Sasa mnataka wasomi au watu wenye taaluma zao waache wanachokifanya
Wajitoe ufaham nao wafanye kama hao uchawa nk

Ova
 
Kabla ya uchawa walikuwepo wapambe,haya mambo yako tokea zamani
Sema chawa,wapambe wa sasa wanajionesha mpaka kwenye media
Mitandao ya kijamii
Kuna watu mjini walikuwa wanaishi tu kwa kuwatafutia watu fulani maarufu wanawake tu na kuwasifiaaa

Ova
 
Back
Top Bottom