Mwili wa Agnes Gerald 'Masogange' waagwa leo katika viwanja vya Leaders

Mwili wa Agnes Gerald 'Masogange' waagwa leo katika viwanja vya Leaders

BABA mzazi wa Agnes Masogange anayeitwa, Gerald Waya amesema, mwanaye alikuwa nguzo katika maisha yao na kifo chake ni pigo kubwa kwake na familia kwa ujumla.

Waya amezungumza na MCL Digital nyumbani kwake Mbalizi wilayani Mbeya, leo Jumapili na kusema,

Masogange ni mtoto wanne katika familia yake ya watoto sita ambapo wakike ni watano.

Amesema, Masogange amesoma Shule ya Msingi Utengule-Mbalizi na Sekondari ya Sangu akaishia kidato cha pili.

Waya amesema Masogange alipata matatizo hivyo akalazimika kuacha shule. Hata hivyo amesema hataki kuzungumzia mambo mabaya wakati huu anapoomboleza kifo cha mwanaye.

“Aliishia form two (kidato cha pili), akapata matatizo ikabidi aache shule. Tulikosana kidogo lakini tukayamaliza yeye akaenda Dar es Salaam,” amesema.

Waya amesema, “Mwanangu alikuwa nguvu kwangu, alikarabati nyumba hii ninayoishi kwa sasa na nilikuwa nafarijika sana, lakini leo kusikia msiba huu kwa kweli inaniuma sana.”

Amesema Masogange alimpigia simu, “Tukaongea naye akaniambia ‘mimi baba ninaumwa’.Nikamuuliza nini tatizo akasema, “aah! baba niombee tu kwa Mungu’. Na Jumamosi iliyopita nilimpigia simu wakati yupo hospitali kujua maendeleo yake lakini akaniambia ‘baba byee’. Nikaanza kulia, na hapo sikuwasiliana naye tena hadi nilipopata taarifa za kifo chake,”amesema.
Kidato cha pili? itakuwa mimba ya huyo mtoto wake nini?
 
Mkuu mimi sijahudhuria kwa sababu nipo nje ya dsm sasa hali inayinishangaza simuona kabisa belle 9 kwenye social networks zozote ilihali yeye ndiyo aliyempa umaarufu masogange kiufupi nimeishia kuwaona kiba, mondi, shamsa na wengine kibao
Kuuliza sio ujinga wakuu
wewe ulitakaje sasa?
 
Wakuu mlioko dsm na vitongoji vyake na hata wale walioudhuria msiba wa mrembo masogange nilikuwa naomba kufahamishwa kama msanii wa bongo fleva Belle 9 alihudhuria kwenye msiba wa masogange
HUU NDO UCHOCHEZ
 
Hakika sisi ni waja na kwake tutarejea [emoji144]. Pumzika kwa amani Aggy.
 
Back
Top Bottom